Polisi Ruvuma

Polisi Ruvuma USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA POMBE (VIROBA)Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limepokea taarifa kutoka kwa wasili wetu kuwa ka...
02/12/2014

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA POMBE (VIROBA)
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limepokea taarifa kutoka kwa wasili wetu kuwa katika kipindi cha kuelekea mwisho wa mwaka 2014 bidhaa nyingi hasa pombe zinazofungwa au kuhifadhiwa katika naironi (maarufu kwa jina la viroba) nyingi zimepita muda wake, na pia kumekuwepo na watu wanaojitafutia ridhiki kwa kuokota naironi hizo zilizokwisha tumika na kujaza pombe aina gongo kisha kuzipeleka sokoni tena, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi. hivyo mnatahadharishwa kwamba kwa wale wanaotumia vinywaji hivyo (vilevi) ni vyema wakawa makini kabla ya kuvitumia kwa kuangalia uhalali wa bidhaa hizo. au kuacha kabisa kutumia vilevi hivi ambavyo vimetajwa kuwa ndio chanzo kikuu cha saratani ya koo na kansa ya Ini.pia k**a utanunua bidhaa hiyo na kuitilia shaka toa taarifa haraka katika kituo cha Polisi kilichopo karibu.

Kila mwananchi anao wajibu wa kusimamiana kutii kikamilifu sheria za nchi.Usalama barabarani ni jukumu la kilammoja wetu...
26/11/2014

Kila mwananchi anao wajibu wa kusimamia
na kutii kikamilifu sheria za nchi.
Usalama barabarani ni jukumu la kila
mmoja wetu, hivyo kutii sheria za barabarani
iwe ni utamaduni kwa wananchi
wote hususan madereva kwa lengo la
kulinda maisha ya watu na mali zao.
Tujijengee utamaduni wa kutii sheria bila
kushurutishwa.
Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana
ya kusimamia sheria. Lazima
kushirikiana nao, isipokuwa k**a
wanatenda kinyume na sheria.
Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo
wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare
anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni
wakati gani anakusimamisha uwapo barabarani.
Unaweza ukapenda kukata
maelezo haya na kuyaweka kwenye gari
lako – lakini kumbuka kwamba ni
mwongozo tu.
Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha
gari lako – k**a atakupa ishara ya
kusimama, punguza mwendo kwa
usalama na utoke barabarani – pia
anaweza kukuuliza jina na anwani yako
na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya
Usalama Barabarani (RTA), s.78).
Leseni ya kuendesha gari: Ofisa wa
polisi anaweza kuomba kuona leseni yako
ya kuendesha gari – anaweza kukataa
fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua
kupeleka leseni yako ndani ya siku tatu
kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa
na ofisa. Ili kuepuka matatizo, wakati wote
tembea na leseni yako kwenye gari (RTA
s.77).
Hati ya usajili: Ofisa wa polisi ana haki
ya kukagua maelezo ya usajili k**a
yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha
usajili – gari lazima liendane na maelezo
ya kwenye kibandiko, lakini vitu vidogo
k**a rangi iliyofifia au iliyobanduka
haijalishi (RTA s.13).
Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua k**a
umebandika leseni halali ya barabarani na
kibandiko cha bima kwenye kiwambo cha
upepo cha gari lako (kioo che mbele).Kunyang’anywa: Ofisa wa polisi HANA
haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua
leseni isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
Matumizi ya taa nyakati za usiku:
Sheria ya usalama barabarani inakutaka
kupunguza mwanga wa taa za gari lako
unapopishana au kutaka kulipita gari la
mbele yako ili kumwezesha dereva
mwenzako kuyaona vizuri mazigira ya
barabara anayotumia (RTA s.39).
Kuendesha baada ya kunywa pombe:
K**a ofisa wa polisi anakuhisi
umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti
gari ipasavyo, anaweza kukutaka upimwe
(kipimo cha kupumua au kipimo cha
damu) kuona k**a kiasi cha pombe
kwenye damu yako ni zaidi ya kiwango
kilichoelezwa. K**a ukikataa utakuwa na
hatia ya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).
Kutumia simu ya mkononi wakati
unaendesha: ingawa sheria haikatazi hili
mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona
kuwa unatenda kosa la “kuendesha kwa
uzembe” (RTA, s.42, s. 50).
Mwendo kasi: Unapaswa kuzingatia
kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa ni
pamoja na km 50 kwa saa katika maeneo
ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na
alama) – ofisa wa polisi anaweza kupima
mwendo kasi wako kwa namna
mbalimbali - hata hivyo, unaweza kupinga
ushahidi wake mahak**ani (RTA s.51,
s.73(2)).
Kustahili kuwepo barabarani: Ofisa wa
polisi ana haki ya kukagua k**a gari lako
liko katika hali ya usalama kiufundi.
Matairi, breki, taa, indiketa na usukani
lazima viwe vinafanya kazi vizuri –
unaweza kutakiwa kupeleka gari mahali
litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa
magari wa polisi (RTA, s.39.1, s.81).
Unashauriwa kupeleka gari lako
kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata
stika ya usalama barabarani, cheti cha
ubora wa gari, au barua kutoka polisi
k**a ushahidi kwamba gari lako
limekaguliwa.
K**A OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU
KWAMBA UMEFANYA KOSA:
Mara nyingi utapewa uchaguzi wa
kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 30,000
kwa ofisa wa polisi, au kwenda mahak**an
ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika
maelezo kwenye Fomu ya Polisi ya PF
101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe
usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu
iliyotiwa saini. Unaweza kwenda na ofisa
kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo.
K**a unakubali kosa, lakini huwezi kulipa
faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya
kutuma malipo kwa k**anda wake wa
eneo (RTA, s.95).
K**A UNAFIKIRI OFISA WA POLISI
AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU
AMEKOSEA KWA NJIA YOYOTE
UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO:
Muulize ofisa jina lake, cheo na namba,
na anwani ya kituo cha polisi anakofanyia
kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha
peleka malalamiko ya maandishi kwa
Mkuu wa Polisi wa eneo husika au kwa
K**anda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, S. L. P 1712, Dar es salaam –
ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa
polisi wetu kuwa waaminifu –
usitoe rushwa na usipokee
rushwa.
Said A. Mwema
Inspekta Jenerali wa Polisi
10/6/2011
Jeshi la Polisi Tanzania na Wizara ya
Ujenzi – wanashirikiana kwa ajili ya
usalama zaidi wa barabara.

UMESIMAMISHWA NA POLISI WAKATI UKIENDESHA?
ZIJUE HAKI NA WAJIBU WAKO!

14/02/2014
Ndugu wajumbe tunapenda kuwajulisha kwamba, kwa sasa tunapatikana pia kwenye ukurasa wa Twitter. andika Polisi Ruvuma ki...
27/01/2014

Ndugu wajumbe tunapenda kuwajulisha kwamba, kwa sasa tunapatikana pia kwenye ukurasa wa Twitter. andika Polisi Ruvuma kisha Follow.

KILA MTU ANA SABABU YA KUSEMA ASANTE MUNGU.NAJUA NI VIGUMU SANA BINADAMU WA LEO KUSEMA ASANTE MUNGU KWA HIKI KIDOGO/KIKU...
15/01/2014

KILA MTU ANA SABABU YA KUSEMA ASANTE MUNGU.

NAJUA NI VIGUMU SANA BINADAMU WA LEO KUSEMA ASANTE MUNGU KWA HIKI KIDOGO/KIKUBWA NILICHONACHO.

AMINI NDUGU YANGU LEO NAKWAMBIA UNAPASWA KUMSHUKURU MUNGU KWA HICHO ULICHONACHO LEO AU HAPO ULIPO KWANI WAPO WENGI WANAOTAMANI KUWA K**A WEWE LEO LAKINI WAMESHINDWA NA HATA K**A WAKIWEZA/AKIWEZA BASI ITAKUWA SIYO LEO.

SIYO VIBAYA KUTAMANI KUWA NA KITU FULANI AU KUWA MTU FULANI.

NINACHOZUNGUMZIA HAPA NI KILE KITENDO CHA KUMSHUKURU MUNGU KWA ULICHONACHO LEO.

HAYA NI BAADHI YA MATAMANIO YA BAADHI YA WATU WALIVYO SASA NA WANAVYOTAKA KUWANAVYO:-

YUPO ANAYETAMANI KUWA NA GARI, LAKINI ANA BAISKELI MSHUKURU MUNGU KWA HILO.

YUPO ANAYETAMANI KUWA KIONGOZI FULANI LAKINI TAYARI NI KIBARUA AU MWAAJIRIWA WA TAASISI AU KAMPUNI FULANI MSHUKURU MUNGU KWA HILO.

WAPO WANAOTAMANI KUWA KWENYE NDOA LAKINI TAYARI ANA MCHUMBA MSHUKURU MUNGU KWA HILO.

YUPO ANAYETAMANI KUWA NA ELIMU FULANI LAKINI TAYARI AMESHA JIUNGA/KUANZA KUSOMA MSHUKURU MUNGU KWA HILO.

HAPO ULIPO NI NGAZI YA KWENDA KATIKA MAFANIKIO.

JIFUNZE KUSEMA
"ASANTE MUNGU KWA HIKI NILICHONACHO"

03/01/2014

Maandalizi ya Sherehe ya Kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 yameanza hivi sasa, taarifa kamili inafuata.

Address

Box 19 Songea
Songea
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Polisi Ruvuma posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share