13/01/2025
FAHAMU KUHUSU VIAPO (AFFIDAVITS) NA HATI YA KUBADILI JINA (DEED POLL)
Nuaraka zote hizi hutayarishwa na Wanasheria ili kumsaidia mtu mwenye tatizo la jina au sahini.
HATI YA KUBADILI JINA (DEED POLL)
Hii hutumika k**a mtu anataka kubadili jina kabisa. Mfano k**a mtu amebadili dini na kupewa jina jipya na anataka kutumia jina hilo kwenye masuala yake yote rasmi. Hizi Mara nyingi huitajika sehemu za kazi au Uhamiaji nk au k**a Jina la NIDA limekosewa.
KIAPO CHA KUZALIWA.
Hiki ni kiapo cha kuthibisha mahali na mwaka ulipozaliwa . Mara nyingi huitajika idara ya uhamiaji wakati wa kuomba PASSPORT ili kujua ni lini na wapi alipozaliwa mmoja wa wazazi
KIAPO CHA KUTHIBITISHA JINA/SAHIHI.
Hiki ni kiapo kinachotumiwa na mtu mwenye jina au sahihi zaidi ya moja na na vyote vinamtambulisha yeye. Mara nyingi hutumika kwenye INTERVIEW au Benki wakati wa kufungua au kuuhisha Akaunti.
KIAPO CHA KUBADILI SAHINI.
Hutumika pale ambapo mtu amesahau sahihi yake aliyoitumia mwanzoni na juhudi za kukumbuka zimekwama. Mara nyingi hutumika Benki au Uhamiaji.
KIAPO CHA KUTOAJIRIWA (UNEMPLOYMENT)
Hiki hutumika kuthibitisha kuwa tangu ulipoachishwa kazi hujabahatika kupata kazi tena. Hii hutumika NSSF wakati wa kulipa mafao ya kukosa kazi (Unemployment benefits) baada ya kuachishwa kazi.
NB.
Zipo aina nyingi sana za viapo kulingana na uhitaji na mazingira husika.
HATI YA KUBADILI JINA (DEED POLL) inapaswa kusajiliwa ofisi ya Msajili wa Hati.