30/04/2021
UGONI NI NINI
Na wakili Asajile Baraka
✅kujamiiana kwa hiari kati ya mwanamume na mwanamke ambao hawajaoana lakini angalau mmoja wao ni mtu aliyeolewa/kuoa. Kwa tanzania ni kosa la madai. Ni muhimu kuwa na ushahidi kuwa mkeo au mumeo alijamiana na mwanaume au mwanamke mwingine. Sms tuu hazitoshi lakini kuwe na ushahidi kuwa walifanya mapenzi
MAMBO MUHIMU KUDHIBITISHA KWA KOSA LA UGONI/ELEMENTS TO ESTABLISHED.
✅1) kwamba mwanamke ameolewa au mwanaume kaoa;
✅ 2) kwamba anafanya ngono na mwanaume sio mumewe au mwanamke asiye mkewe
✅ 3) kwamba kwa habari ya mwanamume ambaye alifanya tendo la ndoa naye, lazima amjue kuwa ameolewa.
,✅4.) Kupewa mimba na mume wa mtu na kumpa mimba mke mtu
✅5.) Magonjwa ya zinaa
✅6.) Fumanizi la papo kwa papo
UTETEZI WA UGONI/DEFENSES FOR ADULTERY.
✅Kuna utetezi wa aina tatu unaweza kutumika katika kesi za ugoni
1.Fumanizi la ugoni la kupanga,
Hii hasa kwa wale ambao wanapanga na mke wake anatafute buzi then ajifanye anamfumania mke wake.
Huu unaweza kuwa utetezi k**a jamaa akagundua kuwa kumbe mlipanga fumanizi la ugoni dhidi yake.
2.k**a mume au mke tayari mmepeana talaka.
K**a mmeshaachana kwa talaka huwezi msh*taki mwanandoa mwenzako kwa ugoni hata umfumanie.
3.K**a mwanaume alikuwa hajui kuwa anayejamiana naye ni mke wa mtu, au mwanamke alikuwa hajui kuwa aliyekuwa anafanya naye mapenzi ni mume wa mtu huu unaweza kuwa utetezi.
Soma S.72 of LMA RE 2019.
It is not exhaustive, mcheki mwanandishi kwa elimu zaidi au wasiliana na Mwanasheria wako.
Mwandishi hatahusika na matumizi mabaya ya elimu. Hii ni mwongozo
0755845107
0784745645
Zote zipo WhatsApp.