01/05/2017
Kesho tarehe 2 mwaka huu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi atazindua *Mpango Kabambe wa Mji wa Mtwara* (Master Plan). Zoezi hili litafanyika katika ukumbi wa Boma Mkoa ulioko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuanzia saa 2 asubuhi.
Kukamilika kwa Mpango huu ni hatua muhimu katika kuweka mazingira mazuri na kuruhusu uwekezaji katika Mkoa wa Mtwara hasa katika kipindi hiki ambacho Mkoa uko katika kampeini kubwa ya kuvutia wawekezaji.
Mpango huu ambao unakusudia kuupanga mji wa Mtwara kwa miaka 20 kuanzia 2015 – 2035 unajumuisha hekta 95,117 ambazo ni eneo lote la Manispaa ya Mtwara Mikindani na kata 9 za Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Mpango umezingatia idadi ya watu walio kwenye eneo hilo ambalo kwa sasa ni watu 170,000 huku ikitarajiwa kuwa Katika kipindi cha miaka 20 mpaka 2035 idadi ya watu itaongezeka na kufikia milioni 1.7.
Maono na malengo ya mpango huu ni kuhakikisha hadi mwaka 2035 Mtwara kinakuwa kituo muhimu cha *UWEKEZAJI* na kitovu cha huduma na shughuli muhimu za usafiri na usafirishaji katika ukanda wa mikoa ya kusini mwa Tanzania hususani mikoa ya Lindi, Mtwara Ruvuma na Njombe na ukanda wa maendeleo wa Mtwara ambao unahusisha nchi za Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia na Afrika ya kusini. Pia kuifanya Mtwara kuwa Jiji lenye ustawi wa maisha shindani na majiji yaliyo kwenye ukanda wa bahari ya hindi, mashariki na kusini mwa Afrika.
Mpango Kabambe umeainisha maeneo ndani ya mradi k**a ifuatavyo;
*Eneo mahususi la Kisasa la Mjini Kati:* Kitovu cha shughuli za kisasa za biashara, huduma za kibenki, Makao Makuu ya Taasisi Mbalimbali, Hoteli, majengo marefu na ya kisasa.
*Eneo Mahususi la Naumbu:* Kitovu cha ajira kwa wakazi wa mji hasa zitokanazo na shughuli za viwanda vikubwa Hekta 10-20, Makazi yaliyopangika na kuratibiwa kwa ustadi na maeneo ya mahoteli ya kitalii.
*Eneo Mahususi la Mjimwema:* Kitovu cha huduma za elimu ya juu hasa vyuo vikuu na makazi yaliyopangwa na kuratibiwa kwa ustadi wa hali ya juu.
*Eneo mahususi la Nanguruwe:,* Kitovu cha huduma za kisasa za Afya, Viwanda vya ukubwa wa kati ya Hekta 5-9, Eneo la makazi ya kisasa yaliyopangwa na kuratibiwa kwa ustadi pembezoni ya mji, maene