10/10/2022
SEMA, NIFANYE/NITENDE
Je! Ulishawahi kusikia watu wakisema kuwa "kusema ni dawa?". Jibu ni ndio, mara nyingi huwa tunataman vitu vingi na vikubwa ila huwa hatusemi, tunatumia bidiii na nguvu kubwa ktk kuvitafuta bila kusema eti tu unaamini kuwa hicho kitu ni huenda kikawa kidogo ukakimalisha mwenyewe, lakini matokeo yake huwa sivyo. Kitabu cha Mwanzo 7:7 kiaelezea kabisa juu ya kusema. "Ombeni mtapewa..." kwa lugha rahisi ni kwamba, usiposema hutopewa. Fikiria tu ktk maisha ya kawaida, je mtu anaweza kuja na kukupa hitaji la moyo wako bila ya kumuomba/kusema? Jibu ni hapana. Hivyo hata kwa Mungu yatupasa kusema/kuomba ndipo tupate. Unaposema unatengenez jambo jipya ambalo ulitaka litokee ama liwepo. Ikiwa Mungu Ali ufanye ulimwengu kwa kusema/neno, basi yatupasa na sisi tuseme siku zote wala tusikate tamaa, ili tupate haja za mioyo yetu. Mungu Akubariki sana.