Novels Community

Novels Community tunasoma hadithi kupunguza gharama za maisha

MAISHA YANGU SEHEMU 1Ni katika nyumba moja ya mzee Donald ambapo sauti ya mzee uyo ilisikika ikisema "Bora shule zifungu...
20/07/2023

MAISHA YANGU
SEHEMU 1

Ni katika nyumba moja ya mzee Donald ambapo sauti ya mzee uyo ilisikika ikisema
"Bora shule zifungue tu sipendi tunavyopishana katika nyumba Yangu".
Alikuwa akimwambia mwanae wa kiume kwa jina la Emmanuel ambae alikuwa kidato cha 4 kwa mwaka huo. Mzee Donald alibahatika kupata watoto watatu wote wa kiume kwa mke wake wa kwanza ambaye alifariki miaka mingi iliyopita..
Baada ya mke wake kufariki Donald aliwapeleka wanae wote kwa mama yake mzazi kwani asingeweza kuwalea wote watatu kwa Sababu walikuwa wadogo sana.Baada ya miaka mingi kupita Donald alifanikiwa kuoa mke mwingine ambaye alikuwa akiishi nae mjini katika nyumba yake mpya hivyo alimfuata mwanae wa kwanza aweze kuishi nae pamoja.
Yule mama wa kambo alikuwa mpole sana kwa siku za mwanzoni na alimlea vizuri Emmanuel k**a mwanae wa kumzaa...Emmanuel alijisikia fahari sana kuishi na mama huyo ambaye alikuwa akimnunulia zawadi mbalimbali k**a vile nguo pamoja na mahitaji madogo madogo. Baada ya miezi kupita..Maisha yalibadilika kwa kiasi kikubwa kwani manyanyaso yalianza kwa Emmanuel baada ya yule mama wa kambo kuzaa mtoto wa kike.Donald alikuwa ni mkulima mkubwa sana hivyo mwanae alikuwa muda wote shambani kufanya kazi mbalimbali..kwenda shambani na kurudi ilikuwa ni takribani kilometa 12 ambapo Emmanuel alikuwa akienda na baiskeli ndogo..Baada ya kutoka shambani Emmanuel alitakiwa kufanya usafi k**a vile kudeki,kuosha vyombo na vilevile kupika chakula cha jioni ilhali mama wa kambo alikuepo hapo hapo nyumbani..hali hii ilipelekea maisha yawe magumu kwani Emmanuel alikuwa akichoka sana shambani kulingana na kazi ambazo alikuwa akipewa bila ya mpangilio maalumu..wakati hayo yakiendelea Donald hakuwa akifahamu kinachoendelea katika nyumba Yake kwani muda mwingi hakuepo nyumbani na Emmanuel alikuwa mkimya sana na alijitahidi kuwa mchangamfu k**a kawaida,hali hii ilimfanya akonde ghafla kwa mawazo akihofia k**a baba yake akijua itapelekea ugomvi mkubwa na mama yake wa kambo na hakutaka ifikie huko. Muda huo ilikuwa ni likizo.
********
Baada ya likizo kuisha Emmanuel alikuwa akijiandaa kwenda shuleni na aliorodhesha mahitaji ya msingi k**a alivyoelekezwa afanye na baba yake... Alimpa gharama zote pamoja na pocket money ilikuwa ni Tshs. 35,000/= cha ajabu na cha kushangaza Donald alisema pesa hiyo ni kubwa sana hivyo angempa Tshs. 25,000 /= kwa sababu tu mwanafunzi hakupaswa kuwa na pesa nyingi,kitu hicho kilimuumiza sana Emmanuel akitegemea angepewa zaidi ya pesa hiyo kwani maisha ya shule anayosoma yalikuwa magumu sana. Hakuwa na wa kumwambia tatizo hilo alidhamiria kuwa akifika shule hatopiga simu yoyote kuomba pesa ya matumizi.Wakati akiwa stendi akisubiri gari alimwona baba yake mzazi akimpa mtoto wa Dada yake wa hiari aliyeitwa Elisa Tshs.15,000/= ikiwa ni pesa ya kula na akimtaka akazane kusoma, kitendo hicho kilimfanya Emmanuel apate maumivu makali ya moyo na akagundua kuwa baba yake mzazi anajitoa sana kwa watoto wasio wake kwa kuwapa pesa akiacha watoto wake wa damu bila mahitaji yanayojitosheleza.
Emmanuel alipata gari na kuanza safari yake kwenda shule na njiani alikuwa na mawazo akikumbuka mateso aliyopata kwa mama yake ya kambo na vile baba yake mzazi anamfanyia alizidi kuchoka akili na roho. Baada ya muda wa masaa 4 alifika shule na kabla ya kuingia ndani ya shule aliingia katika maduka yaliyokuwa nje ya shule hiyo ambapo kulikuwa na barabara iliyotengenisha shule na maduka hayo.. Emmanuel alipomaliza kununua mahitaji yake alivuka barabara hiyo bila kuangalia k**a kuna gari. Gari aina ya Nissan patrol ilimgonga na kumtupa mbali na begi lake na...

Emmanuel atakuwa salama??


Usikose sehemu ya pili

kupata muendelezo wa simulizi hii bofya hapa 👇👇
wa.me/+255757443633

Karibuni tusome hadithi kupunguza gharama za maisha ya kila siku.tufurahi kwa pamoja
20/07/2023

Karibuni tusome hadithi kupunguza gharama za maisha ya kila siku.
tufurahi kwa pamoja

tunasoma hadithi kupunguza gharama za maisha

Address

Iringa

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 00:00 - 18:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255757443633

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Novels Community posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Novels Community:

Share