PATA Msaada WA Sheria

PATA Msaada WA Sheria Tunatoa msaada/ushauri wa sheria bure kabisa.

Yajue Mambo muhimu kuhusu Talaka//Essentials for Divorce//
12/03/2023

Yajue Mambo muhimu kuhusu Talaka
//Essentials for Divorce//

KUTOKA KWA MDAU:"Niliolewa mwaka 2013 kwa ndoa ya kikristo, Tumeishi na mume wangu kwa amani kabisa na kwa upendo wa hal...
22/12/2022

KUTOKA KWA MDAU:

"Niliolewa mwaka 2013 kwa ndoa ya kikristo, Tumeishi na mume wangu kwa amani kabisa na kwa upendo wa hali ya juu. Tumefanikiwa kupata watoto wawili wote wa kiume. Mwaka 2019 mume wangu alipata ajali na kuvunjika uti wa mgongo na miguu yote miwili hivyo akawa ni mtu wa kukaa ndani na nimemuuguza mpaka October 2022 alipopata mauti na kututoka. Wakati wa uhai wake tulifnikiwa kuchuma mali nyingi ambazo siwezi kuzitaja hapa lakini zote zimesajiliwa kwa majina ya marehemu
NAOMBA UNISAIDIE UTARATIBU WA KUFUATA ILI KUWEZA KUBADILI DOCUMENTS ZA MALI NA KUSAJILI KWA MAJINA YANGU"

USHAURI WANGU:

Kwanza pole sana kwa kuondokewa na mpendwa wako.

1. Mnatakiwa kukaa kikao cha ukoo na kumteuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu.

2. Kwenye hicho kikao cha ukoo mnatakiwa kiandika Muhtasari wa hicho kikao ambao pia utaorkdhesha mali za marehemu.

3. Msimamizi wa mirathi ya marehemu atakayeteuliwa, alazimika kufuatilia cheti cha kifo cha marehemu mme wako.

4. Kwakuwa marehemu alaikuwa mkristo, msimamizi wa mirathi ataenda kwa mwasheria, akiwa na cheti cha kifo pamoja na muhtasari wa kikao cha ukoo.

5. Mwanasheria atamuandalia documents za kisheria ambazo ataenda kuzisajili katika mahak**a ya Wilaya aliookuwa akiishi marehemu.

6. K**a hakuna pingamizi lolote, mahak**a itamthibitisha na kumteua msimamizi wa mirathi ambaye atawajibika kuzikusanya na kuzigawa mali za marehemu. Pia k**a marehemu alikuwa na deni, basi msimamizi wa mirathi itabidi alipe madeni ya marehemu.

7. Msimamizi wa mirathi atatengeneza mgao wa mali za marehemu na kuwagawia warithi wote. (Kwakuwa wewe una watoto wawili, k**a marehemu hakuwa na wategemezi basi hizo mali utazigawa kwa watoto wiwi nawewe pia mjane wa marehemu)

8. Mahak**a itathibitisha na kuupitiaha mgawo huo wa mali.

9. Kwa kila mtu aliyerithi mali ya marehemu, kwa amri ya mahak**a atakuwa na haki ya kubadilisha jina na kusajili kwa jina lake.

Karibu tukuhudumie:
0744558776
0652197636

22/11/2022

JE, UNATAKA KUJUA SHERIA ZA MIRATHI?

LEO SAA NANE KAMILI MCHANA TUTATOA ELIMU JUU YA SHERIA ZA MIRATHI NA TARATIBU ZAKE

Tunatoa msaada/ushauri wa sheria bure kabisa.

MDAU ANAULIZA:"Mimi niliolewa kwa ndoa ya kikristo, ndoa yetu imedumu kwa miaka 5 ila baadaye ikaanza kuwa na migogoro y...
07/11/2022

MDAU ANAULIZA:

"Mimi niliolewa kwa ndoa ya kikristo, ndoa yetu imedumu kwa miaka 5 ila baadaye ikaanza kuwa na migogoro ya mara kwa mara, baada ya migogoro kutokea na kusuluhishwa na ndugu wa familia bila mafanikio niliamua kutoroka kwa mume wangu . Sasahivi ninaishi na mwanaume mwingine lakini hatujafunga ndoa.
Najaribu kumuomba Mume wangu (ambaye nilimtoroka) talaka lakini hataki kunipa talaka anadai nimrudishie mahali yake kwanza ndo aniandikie talaka. Nimechoka kias kwamba nashindwa nifanyeje. TAFADHALI NAOMBA UNISHAURI NIWEZE KUPATA TALAKA YANGU KWASABABU MIMI SINA TENA UPENDO NAYE NA SIITAKI TENA HII NDOA" naomba ufiche jina langu.

JIBU:

1. kwanza mpaka hapo ulipo unaishi kimakosa na huyo mwanaume. Mume wako anaweza kukuwash*taki kwa kosa la "ugoni", kwahiyo nakushauri usiishi na huyo bwana mpaka utakapopata talaka yako.

2. Tambua kwamba Talaka inatolewa na Mahak**a, wala haitolewi na mtu (mume/mke)
3. Ili kupata talaka kuna njia na taratibu za kufuata ili udai talaka, njia ni:

a) inabidi uende kwenye Bodi ya usuluhishi awa masuala ya ndoa. Hiyo bodi itawaita wewe na mume wako ili kuwasuluhisha na kupata suluhu.

b) ikitokea bodo imeshindwa kuwasuluhisha na kuwapatanisha, basi itaandika document ya kuelezea kushindikana kwa suluhu hivyo ndo hiyo hairekebishi tena.

c) Kwakuwa ndoa yeni ni ya kikristo, basi utaenda mhakana ya Wilaya ili kufungua maombi ya kudai talaka.

Cc:
Neema Lasi
Abdallah Matanza
FURAHA NA HAKI KISIASA.
Amiri Addy

29/09/2022

Talaka ni haki aliyonayo kila mwanandoa. K**a ilivyo haki ya kufunga ndoa ndivyo ilivyo haki ya talaka pia. Yeyote kati ya wenye ndoa anaweza kuomba talaka. Awe mwanamke au mwanaume. Lakini hii ni katika sura ya 29 ya Sheria ya ndoa na si katika imani ya dini yoyote.

1.TALAKA NININI.

Talaka ni amri /tamko maalum la mahak**a linalotamka kuhusu kuvunjika kwa ndoa. Hii ndio maana ya talaka lakini kwa mujibu wa sheria.
Katika maana hiyo twapata kujua kuwa talaka ni lazima itolewe na mahak**a.

Mahak**a ndicho chombo chenye dhamana kuu katika kubatilisha ndoa kwa namna ya talaka.

2. JE UNAWEZA KUOMBA TALAKA MUDA GANI BAADA YA KUFUNGA NDOA.

Ili uweze kuomba talaka ni lazima ndoa itimize miaka iwili . Huwezi kufunga ndoa mwezi huu halafu mwezi ujao ukakimbilia mahak**ani ukitaka talaka. Ndoa ikifikisha miaka miwili basi haki ya talaka inafunguka.

3. TOFAUTI YA KUTENGANA NA TALAKA.

Sio kila kuachana ni talaka. Aina nyingine za kuachana zina sifa za kutengana na sio talaka. Kutengana ni hatua ambapo wanandoa wanaacha kuishi chini ya paa au dari moja. Wanaweza kuishi nyumba moja lakini vyumba tofauti.Halikadhalika wanaweza kuishi nyumba tofauti na hata pakawa mbali ya nchi kwa nchi, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya,kijiji kwa kijiji n.k.

Tofauti kubwa kati ya talaka na kutengana ni kuwa katika talaka kunakuwa na tamko maalum kutoka mamlaka maalum linalositisha mahusiano ya ndoa, wakati katika kutengana hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka linalotangaza kuisha au kusitishwa kwa mahusiano ya ndoa.

Kutengana kupo kwa aina mbili. Kwanza ni kutengana kwa hiari ambapo wanandoa kwa hiari yao wanatengana, na pili ni kutengana kwa kuiomba mahak**a kuwatenganisha. Yapo mazingira ambapo kumtenga mwenza kunaweza kuwa kugumu kutokana na mazingira kadha wa kadha na hapo ndipo unapoweza kuiomba mahak**a iwatenganishe.

4. UNAPOHITAJI TALAKA FUATA HATUA HIZI.

( a ) Hatua ya kwanza kabisa kabla ya kwenda mahak**ani lazima upeleke ombi lako baraza la usuluhishi wa migogoro ya ndoa. Kwa waislamu baraza hilo ni BAKWATA na wengine baraza hilo ni ustawi wa jamii . Kila makao makuu ya wilaya ustawi huu upo ukiuliza utaelekezwa.

Baraza hili litajaribu kusuluhisha na likishindwa litakuandalia fomu maalum kuhusu kushindwa kwake kusuluhisha. Fomu hiyo inaitwa fomu namba 3.

( b ) Hatua ya pili utakapokuwa umepewa fomu hiyo utatakiwa kuandaa maombi ya kisheria ya kutaka kuvunja ndoa huku ukiambatanisha hati hiyo.

Katika maombi hayo utatakiwa kuthibitisha uwepo wa ndoa halali, sababu inayokupelekea kuomba talaka, watoto mlionao k**a wapo, na mali mlizonazo k**a zipo. Mahak**a itasikiliza na itatoa uamuzi.

5. JE NIENDE MAHAKAMA IPI KUDAI TALAKA.

Shauri la talaka ni shauri la ndoa. Na mahak**a zenye mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ndoa ni Mahak**a ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi na mahak**a kuu. Unaweza kufungua shauri lako katika mahak**a yoyote kati ya hizi. Isipokuwa ni lazima iwe mahak**a ile iliyo katika wilaya yako na mahak**a kuu iwe katika kanda yako.

Imeandaliwa na:
Amiri Addy
0744558776
[email protected]

Tunatoa msaada/ushauri wa sheria bure kabisa.

26/09/2022

Ili jamii iwe na amani lazima haki iweze kutendeka. Tumejipanga kuhudumia jamii kwa kuisaidia kupata meaada pamoja na ushauri wa masuala ya kisheria ili wanajamii waweze kupata haki.
K**a unahitaji kupata ushauri, au unahitaji msaada wa sheria lakini hujui uanzie wapi, basi usisite kufollow page yetu na kutuma ujumbe wako ili uhudumiwe. HUDUMA ZETU NI BURE KABISA

Tunatoa msaada/ushauri wa sheria bure kabisa.

Address

Dodoma
SLP60

Telephone

+255744558776

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PATA Msaada WA Sheria posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to PATA Msaada WA Sheria:

Share