Liganga & Co. Advocates.

Liganga & Co. Advocates. Aimed at proving timely and professional legal services. With us,you are assured of achieving the be

Masters Degree(LL.M) in Corporate & Commercial Law, UDSM🙏🙏💪💪
30/11/2022

Masters Degree(LL.M) in Corporate & Commercial Law, UDSM🙏🙏💪💪

26/11/2021
07/06/2019
11/01/2016

Habari za jioni ndugu zangu,
K**a ambavyo tuliahidi kuwa tutakuwa tunatoa tafsiri ya sheria inayoshughulikia shughuli na makosa yanayofanyika mtandaoni, The Electronic Transactions Act, 2015.
ANGALIZO: Tafsiri itakayokuwa inatolewa hapa si ile ya kutoka lugha ya kiingereza kwenda katika lugha ya kiswahili, la hasha. Bali tutakuwa tunatoa maelezo ya jumla ili kila mtu aielewe sheria hii kwa urahisi zaidi.

Katika kutoa tafsiri hii, hatutojihusisha na kutafsiri kifungu cha 1,2 na 3 ambavyo kimsingi ni k**a vifungu vya utangulizi tu. Kutokana na hilo, tutaanza na kifungu cha nne ambacho husomeka k**a ifuatavyo:-

Section 4: RECOGNITION OF DATA MESSAGE. 'A data message shall not be denied legal effect, validity or enforceability on the ground that it is in electronic format'.

Hii ina maanisha kuwa taarifa zote zilizotumwa, zilizohifadhiwa au hata kusambazwa kwa njia za ki elekroniki k**a vile ujumbe mfupi wa maandishi, instagram, WhatsApp n.k zinatambulika kisheria na zinaweza tumika hata katika utoaji wa ushahidi katika kesi endapo tu kile kinachobishaniwa mahak**ani au lile kosa linash*takiwa mahak**ani limetendeka katika moja ya njia tajwa hapo juu au njia nyingine yoyote inayofanana na hizo.

Na msisitizo ni kwamba ushahidi wa aina hii hauwezi kupingwa eti kwa sababu tu uko katika mfumo wa ki elekitroniki.

Imekuwa kawaida sana siku hizi watu kutukanana kwa njia ya simu, au hata mitandao ya kijamii, watu wanaingia makubaliano mbalimbali kupitia simu za mkononi au hata kupitia mitandao ya kijamii. Utapeli mwingi hufanywa kupitia mitandao ya kijamii lakini watu tumekuwa hatujui nini cha kufanya kwa kuamini kuwa hatuna ushahidi wa kile kilichotendeka. Na hii yote inatokea kwa sababu tu tunadharau ujumbe unaotumika katika kufanya utapeli, n.k

Naomba nitoe mfano. Yuko mtu (jina.kapuni) alikuja ofisini kwangu akilalamika kuwa katapeliwa. Kwa mujibu wa maelezo yake, alimkopesha mtu hela kiasi cha Tshs. 45,000,000/=. Lakini mazungumzo yote juu ya kukopeshana kwao yalifanyika kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia simu ya mkononi. Katika kutoa maelezo yake mwishoni ak**alizia kwa kulalamika kuwa hana jinsi kwa sababu hana ushahidi wa
maandishi wa kumbana yule alomtapeli.

Hii inamaanisha kuwa hakujua kuwa hata ule ujumbe walokuwa wanachati ungetosha kabisa kutumika k**a ushahidi katika madai yake dhidi ya yule mtu.

Kwahiyo ndugu zangu, tusijidanganye na wala tusidharau michakato mbalimbali inayofanyika mitandaoni au katika njia za kawaida za simu.

Ukitukanwa kwa njia yoyote ya kimtandao, ukikopwa hela kwa njia ya mtandao au sms za kawaida, ukiingia makubaliano yoyote kwa njia ya mtandao, au kitu chochote unachohisi kinaweza leta mgogoro, hakikisha hufuti huo ujumbe iwe ni katika sms, facebook, instagram, twiter n.k kwani itakusaidia sana.

ANGALIZO. Ili uweze kutumia ujumbe wako kisheria, ni lazima iwe imekidhi vigezo kadhaa ambavyo tutavielezea taratibu katika utaratibu wetu huu.

Kwa yeyote mwenye swali, maoni au hata hoja ya kuongeza ili kufanya hiki kifungu kieleweke vizuri anakaribishwa kuchangia.

Ahsanteni

10/01/2016

Habari ndugu zangu,
kutokana na kushamiri kwa matukio yasiyo ya kiungwana katika mitandao ya kijamii, team nzima ya wanasheria wa Liganga & Co Advocates, imeona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa elimu ya bure juu ya uwepo wa sheria inayoshughulikia makosa yanayotendeka mitandaoni, The Electronic Transactions Act, 2015.
Uamuzi huu umekuja kutokana na ukweli kwamba wengi wetu tumekuwa tukitoleana lugha chafu mitandaoni aidha kwa kutojua kuwa kufanya hivyo ni kosa au kwa makusudi kabisa.

Vilevile tumegundua kuwa wale wahanga wa matusi hayo au vitendo hivyo viovu mitandaoni wamekuwa hawajui.wapi pa kuanzia katika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wanaowatendea uovu.

Pamoja na utoaji wa elimu hiyo, Liganga & Co Advocates pia itakuwa inajibu maswali mbalimbali ya kisheria kwa kadri ya uwezo tulokua nao. Kwa hiyo tunakaribisha swali au hata hoja yoyote inayohitaji ujuzi fulani wa sheria.

Ahsanteni sana na Mungu awabariki.

01/01/2016

Liganga & Co. Advocates celebrates one year and a half since its establishment. The firm consists of young but very skilled lawyers who are always there to provide the best legal services at the speed which every client would demand.

The firm has managed to handle a good number of cases some of which involved reputable institutions in the Country such as PUMA ENERGY (T) LTD and RUBY ROADWAYS LTD. The firm has also managed to retain a good number of companies on a retainer basis and all have highly appreciated our services.

In this modern world, in which every transaction involves legal complications, it is highly recommended that you seek lawyer's advice before embarking into any act or entering into any business. Liganga & Co. Advocates is there to provide you with legal safety to any transaction you think of being a party to it.

Lastly, the firm is highly grateful to those who in one way or another made the firm survive, particularly Hon Judge Samuel Karua and Hon Judge Mlay for their considerable advice
to the firm.

We wish you all a happy and prosperous new year, 2016

Fikiri Liganga
Managing Partner
0714 359 175/0759 448 045
[email protected]

Address

RITA TOWER, 11th Floor Suite, Simu Street/Makunganya Road. P. O. BOX 76013 Dar Es Salaam, Tanzania. Tel: 0714 359 175/0759 448 045. Email: Fikiriligangab@gmail. Com
Dar Es Salam

Opening Hours

Monday 07:30 - 18:30
Tuesday 07:30 - 18:30
Wednesday 07:30 - 18:30
Thursday 07:30 - 18:30
Friday 07:30 - 18:30
Saturday 11:00 - 04:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Liganga & Co. Advocates. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Liganga & Co. Advocates.:

Share