College of Business Education - CBE

College of Business Education - CBE The origin of the College of Business Education (CBE) is closely linked to the history of the Nation itself. His Excellency, J.K.

It was soon after Independence on 9th December 1961, that the newly independent state found itself in need of trained personnel to Commercial and It was soon after Independence on 9th December 1961, that the newly independent state found itself in need of trained personnel to Commercial and Industrial activities. At that time there were very few nationals with commercial education and expertise. T

he need to train nationals for the commercial sector therefore gave birth to a business training institute in the country. In 1965 the establishing Act of the College, Act of Parliament No. 31 of 1965 was enforced. The said Act gave the College its legal status as an autonomous institution with its Governing Body. The duties of the Governing Body were to govern and administer the College activities under the Ministry responsible for Trade. Nyerere, the first President of the United Republic of Tanzania officially opened the new College in January 1965. The College was officially named the “College of Business Education” (CBE).

WANAFUNZI WA K**E CBE WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA UHIFADHI TAULO ZA K**EChuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kupi...
14/05/2026

WANAFUNZI WA K**E CBE WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI SAHIHI NA UHIFADHI TAULO ZA K**E

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kupitia Kurugenzi ya Huduma za Wanafunzi kimeendelea kuwawezesha wanafunzi wa k**e kwa kutoa mafunzo kuhusu matumizi sahihi na uhifadhi sahihi wa taulo za k**e zilizotumika.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na Bi. Sapiencia Masaga, Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu wa CBE, pamoja na Bi. Irene Felix Masawe kutoka ORA Sanitary Pads.

Katika mafunzo hayo, wanafunzi walipata elimu kuhusu:

✅ Matumizi sahihi ya taulo za k**e
✅ Aina mbalimbali za taulo za k**e
✅ Umuhimu wa usafi binafsi wakati wa hedhi
✅ Namna salama ya kuhifadhi taulo zilizotumika
✅ Madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na ukosefu wa usafi wakati wa hedhi
✅ Utunzaji wa afya na mazingira wakati wa hedhi
✅ Mafunzo ya vitendo kuhusu matumizi sahihi ya taulo za k**e

Aidha, washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali, kushirikiana uzoefu wao, pamoja na kupatiwa taulo za k**e kutoka ORA Sanitary Pads.

CBE inaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunzia kwa kuzingatia afya, ustawi, na maendeleo ya wanafunzi.

🎓 CAREER FAIR 2026 – CBEChuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinakukaribisha kwenye Career Fair 2026!🗣️ Kauli Mbiu:“Ubunifu ...
14/05/2026

🎓 CAREER FAIR 2026 – CBE

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinakukaribisha kwenye Career Fair 2026!

🗣️ Kauli Mbiu:
“Ubunifu na Ujuzi kwa Vijana: Msingi wa Ukuaji wa Biashara na Viwanda Tanzania”

🎤 Mgeni Rasmi:
Mhe. Dennis L. Londo (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

📅 Tarehe: 29 Mei, 2026
⏰ Muda: 03:00 Asubuhi – 06:00 Mchana
📍 Mahali: Viwanja vya Basketball, CBE – Dar es Salaam

🌟 Jiunge nasi kwa fursa za kipekee za kujifunza, kuunganishwa na wadau wa sekta mbalimbali, na kuchunguza njia za mafanikio katika taaluma na biashara.

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA NA TAASISI ZAKEMkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. E...
14/05/2026

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA NA TAASISI ZAKE

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Edda Tandi Lwoga, Mei 13, 2026 ameshiriki katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Wizara kupitia baadhi ya Taasisi zake, ambapo ameungana na Viongozi wengine wa Wizara ya Viwanda na Biashara akiwepo Naibu Waziri Mhe. Dennis Londo pamoja Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge  ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb.), ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na taasisi zake kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake, huku akizitaka kuongeza kasi ya utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayolenga kukuza uchumi wa taifa.

🚀 Boresha Usimamizi wa Mikopo kwa Ufanisi Zaidi!Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinakualika kwenye mafunzo maalum ya:📊 ...
09/05/2026

🚀 Boresha Usimamizi wa Mikopo kwa Ufanisi Zaidi!

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kinakualika kwenye mafunzo maalum ya:
📊 Mbinu za Kisasa za Usimamizi wa Mikopo ya Wajasiriamali

🎯 Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo watumishi wa Halmashauri ili kusimamia kwa ufanisi mikopo inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

🔍 Utajifunza jinsi ya:
✔️ Kuboresha tathmini na utoaji wa mikopo
✔️ Kuimarisha ufuatiliaji wa matumizi ya mikopo
✔️ Kupunguza mikopo chechefu
✔️ Kuelewa taratibu na sheria za serikali
✔️ Kuongeza ufanisi wa ukusanyaji na urejeshwaji
✔️ Kubadilishana uzoefu na wataalamu wengine

👥 Walengwa:
Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Biashara, Wahasibu na wadau wa mikopo ya 10%

📍 Ratiba ya Mafunzo:
📌 Mbeya: 25 – 28 Mei
📌 Dodoma: 22 – 25 Juni

💰 Gharama: Tsh 540,000
(Inajumuisha mafunzo, chakula, chai na ukumbi)

📞 Wasiliana nasi:
Dkt. Nasibu Mramba
📱 0755 488 381
📧 [email protected]
[email protected]

📌 Nafasi ni chache — jiandikishe mapema!

Bi. Constansia Akaro, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara, akiongea na wanafunzi ...
08/05/2026

Bi. Constansia Akaro, Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Biashara Wizara ya Viwanda na Biashara, akiongea na wanafunzi wa CBE kuhusu umuhimu wa kusajili mawazo yao ya biashara mara tu wanapoyabuni .

Alisema hayo katika muhadhara wa umma uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam tarehe 4 Mei 2026.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora wa kiwango katika bidhaa na huduma zinazotolewa ili kujenga imani kwa wateja na kuongeza ushindani sokoni. Pia aliwakumbusha wanafunzi kuhakikisha biashara zao zinazingatia sheria ya vipimo inayotakiwa kufuatwa katika shughuli za biashara ili kuepuka changamoto za kisheria.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Edda Tandi Lwoga, akifungua rasmi muhadhara wa umma uliofanyika katika u...
08/05/2026

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Edda Tandi Lwoga, akifungua rasmi muhadhara wa umma uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam tarehe 04 Mei 2026, akieleza kuwa huu ni muhadhara wa 11 tangu ilipoanzishwa miaka miwili iliyopita. Amesema lengo kuu la mihadhara hiyo ni kuunganisha nadharia ya darasani na uhalisia wa mazingira yanayotuzunguka ili kuwajengea wanafunzi uelewa wa vitendo.

Aidha, ameipongeza Kurugenzi ya Utafiti na Machapisho ya Chuo kwa kuandaa muhadhara huo na kuwaletea wazungumzaji wabobezi, huku akiwahimiza wanafunzi kuitumia fursa hiyo adimu kujifunza uhalisia na kuongeza maarifa yatakayowasaidia katika safari yao ya kitaaluma na maisha kwa ujumla.

Muhadhara huo wa umma ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliendeshwa chini ya mada isemayo, “Ni nini kinahitajika ili kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa?”

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Startup Association, ambaye pia ni Mjasiriamali Mhe. Zahoro Muhaji akiongea na wanafunzi...
08/05/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Startup Association, ambaye pia ni Mjasiriamali Mhe. Zahoro Muhaji akiongea na wanafunzi Muhadhara wa Umma uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam tarehe 4 Mei 2026

Ameeleza kuwa mafanikio katika biashara yanahitaji msingi imara wa ujuzi, mtandao (connections) sahihi pamoja na ustahimilivu wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika safari ya kujenga biashara.

Mhe. Zahoro, amewakumbusha wanafunzi kuwa ajira rasmi ni chache ukilinganisha na wingi wa fursa za kazi zilizopo katika jamii, hivyo amewahimiza kuzingatia kwa umakini mafunzo ya ujasiriamali wanayoyapata chuoni na kuyatumia kwa vitendo.

Muhadhara huo wa umma ulioandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) uliendeshwa chini ya mada isemayo, “Ni nini kinahitajika ili kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa?”

Bw. Masti Mgeni Manyabiashara, amebainisha kuwa changamoto hazipaswi kuonekana k**a kikwazo, bali k**a njia ya kumfikish...
08/05/2026

Bw. Masti Mgeni Manyabiashara, amebainisha kuwa changamoto hazipaswi kuonekana k**a kikwazo, bali k**a njia ya kumfikisha mjasiriamali katika mafanikio, na mara nyingi mwanga wa mafanikio hupatikana baada ya kuvuka mazingira magumu, hivyo mjasiriamali anatakiwa kuwa na uvumilivu katika safari yake.

Picha ya pamoja ya Wanafunzi na watoa mada pamoja na uongozi wa CBE wakati wa Muhadhara wa Umma uliofanyika katika Ukumb...
08/05/2026

Picha ya pamoja ya Wanafunzi na watoa mada pamoja na uongozi wa CBE wakati wa Muhadhara wa Umma uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es Salaam tarehe 4 Mei 2026.

🎓✨ KILA LA KHERI KIDATO CHA SITA 2026 ✨🎓Menejimenti na Watumishi wa CBE tunawatakia wanafunzi wote wa Kidato cha Sita ma...
08/05/2026

🎓✨ KILA LA KHERI KIDATO CHA SITA 2026 ✨🎓

Menejimenti na Watumishi wa CBE tunawatakia wanafunzi wote wa Kidato cha Sita mafanikio makubwa katika mitihani yenu ya kuhitimu.

Endeleeni kuwa na nidhamu, kujiamini, na kufanya bidii — mafanikio yenu ni hatua muhimu kuelekea ndoto zenu. 🌟

Tunawaombea heri na ushindi! 💙

🎓 Scholarship OpportunitiesCBE is sharing scholarship opportunities from other institutions to help students and alumni ...
06/05/2026

🎓 Scholarship Opportunities

CBE is sharing scholarship opportunities from other institutions to help students and alumni continue their studies.

Please check the posts and see which opportunities are suitable for you.

📌 Read the requirements carefully
📌 Apply before the deadline

Take this opportunity to support your education and future.

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salam
P.O.BOX1968

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when College of Business Education - CBE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to College of Business Education - CBE:

Share