12/07/2013
TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAKABIDHI TAARIFA ZAKE MBILI KWA WAZIRI WA SHERIA NA MAMBO YA KATIBA TAREHE 03 APRILI, 2013 DODOMA
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imekabidhi Taarifa mbili za Mapitio ya Mfumo wa Sheria unaosimamia Haki za Madai na Taarifa juu ya Sheria za Mila kwa Makabila yanayofuata mkondo wa mama kwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Mh. Mathias Chikawe.
Makabidhiano ya taarifa hizo yamefanyika mkoani Dodoma baina ya Mwenyekiti wa Tume Mh. Jaji Aloysius Mujulizi na Waziri wa Sjeria na Mambo ya Katiba Mh. Mathias Chikawe na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba Mh. Angela Kairuki, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde pamoja na Makamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
1. TAARIFA JUU YA MAPITIO YA SHERIA ZINAZOSIMAMIA HAKI ZA MADAI
Mapitio ya mfumo wa haki za madai ni moja kati ya juhudi mbalimbali za kuleta mabadiliko zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Programu ya Maboresho ya Mazingira ya Biashara Tanzania (BEST).
Katika kufanya utafiti wake Tume iliwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mahak**a na Mabaraza, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu,Taasisi zisizo za serikali, Jumuiya za Wafanyabiashara, Madalali, Mawakili na Taasisi na Idara za Serikali.
Katika kufanya utafiti, Tume ilijikita katika kufikia misingi ya utoaji haki k**a ilivyoainishwa na Ibara 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Misingi hii ni:-
• usawa – Yaani kutenda haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi.
• uharaka – Yaani kutochelewesha haki bila sababu ya msingi.
• haki – Yaani kutoa fidia ipasayo kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine, na kwa mujibu wa sheria mahususi iliyotungwa na Bunge.
• usuluhishi – Yaani kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika migogoro; na
• utayari – Yaani kutenda haki bila kuweka msisitizo kwenye kanuni zinazoweza kukwamisha haki kutendeka.
Mradi huu unahusisha Mapitio ya Sheria tisa (9) na kanuni nane (8) zifuatazo:-
• Sheria ya Mamlaka ya Rufani, 1979 [Sura 141 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Usuluhishi, 1931 [Sura 15 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai, 1966 [Sura 33 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Ushahidi, 1967 [Sura 6 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Mashauri Dhidi ya Serikali, 1967 [Sura 16 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Mahak**a za Ardhi, 2002
• Sheria ya Ukomo wa Mashauri, 1971 [Sura 89 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Mahak**a za Mahakimu, 1984 [Sura 11 Mapitio ya 2002]
• Sheria ya Mabaraza ya Kata, 1985 [Sura 206 Mapitio ya 2002]Kanuni
• Muonekano wa Maafisa wa Serikali (Tangazo Na. 306 la Mwaka 1964)
• Mwenendo wa Mashauri ya Madai kwenye Rufaa zinazo tokea Mahak**a ya Mwanzo) Kanuni (Tangazo Na. 312 la Mwaka 1964)
• Tozo za Ada kwenye Mahak**a Kuu (Kitengo cha Biashara), 1999 (Tangazo Na. 275 lilofanyiwa marekebisho na Tangazo Na. 428 la mwaka 2005)
• Madalali wa Mahakamu Juu ya Uteuzi Wao, Malipo, na Udhibiti wa Nidhamu (Tangazo Na. 315 la Mwaka 1997);
• Tozo za Ada za Mahak**a (Tangazo Na. 308 la Mwaka 1964)
• Likizo za Mahak**a (Tangazo Na. 307 la Mwaka1964)
• Masijala za Mahak**a Kuu (Tangazo Na. 164 la Mwaka 1971)
• Lugha ya Mahak**a (Tangazo Na. 115 la Mwaka 1981)
Tume imefanya utafiti kwenye sheria zinazosimamia Haki za Madai kwa kubainisha mapungufu yaliyopo na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mapungufu husika. Tume inawasilisha taarifa ya Utafiti kwa Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria kwa hatua zaidi chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria.
2. TAARIFA JUU YA SHERIA ZA MILA KWA MAKABILA YANAYOFUATA MKONDO WA UKOO WA MAMA
Tume ya Kurekebisha Sheria iliamua yenyewe kupitia sheria za mila kwa makabila yanayofuata mkondo wa ukoo wa mama. Itakumbukwa kuwa katika matamko ya serikali ya mwaka 20013, sheria za mila zilizoandikwa na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuwa ni sheria za mila chini ya sheria za Tanzania zilikuwa ni sheria za mila kwa makabila yanayofuata ukoo wa Baba (Patrineal Societies). Hivyo Tume iliona umuhumu wa kuzitambua sheria za mila kwa makabiula yanayofuata ukoo wa mama na hatimaye kuziandika ili zijulikane kirahisi na kutumika kwenye maeneo ya makabila husika.
Tume ilifanya utafiti kwenye Wilaya za Kilombero, Kilosa, Ulanga Mvomero, Namtumbo, Tunduru, Ruangwa, Nachingwea, Masasi na Nanyumbu kwa nia ya kutambua sheria za mila zinzotumika kwenye wilaya hizo na hatimaye kuziandika. Wilaya hizi zilichaguliwa baada ya kubainika kuwa wakazi wake wanafuata mkondo wa ukoo wa mama. Tume imekamisha utafiti huu na inawasilisha taarifa ya utafiti kwa Waziri wa Katiba na Mambo ya Sheria kwa hatua zaidi chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria