23/09/2025
Taarifa zinazohitajika kukusaidia kuanda tamko lako la wosia.
1.majina yako kamili k**a yanavyosomeka katika NIDA.
2.umri,dini yako
3.hali yako ya afya ya akili.
Hapa upo na afya ya akili au
unachangamoto ya afya akili.
Je unatatizo lolote la kisaikolojia ,vyema kuwa muwazi.
4.unaandika kwa hiari yako ama unalazimishwa kufanya hivyo.elezea
5.je unaishi mwenyewe au umeolewa.
6.je warithi wako ni watoto au watu wazima, Wataje kwa majina na umri wao.
7.je una miliki mali yeyote? zitaje kwa makundi haya.
A.zinazoamishika, taja
B.zisizo amishika,taja.
8.je mali hizo unazimiliki peke yako au
mnamiliki na mwenza wako.
Taja mali unazo miliki binafsi na
zile ambazo mnamiliki na mwenza au jamaa au rafiki au ndugu.
9.je una mali ambazo umezipata ndani ya ndoa? Taja
je una mali ambazo ulikuwa nazo kabla ya kuolewa, taja
10. Je mali husika zipo nchini au nje ya nchi ,taja
11. Ainisha mali na sehemu zilipo .
12. Je mali husika unazo nyaraka za umiliki wa mali hizo, mfano mikataba,hati .
13. Bainisha watu ambao unataka kuwarithisha kwa
majina ,
uhusiano wako kwake,
umri, na
Kwa asilimia unazotaka wapate katika mgawanyo huo.
14. Bainisha msimamizi wa wosia kipindi ukiwa haupo ,
taja jina lake,
umri ,
uhusiano wake kwako,
na sababu za kumchagua mf ni mwadilifu,mnapendana ,ni damu moja ,ni mtumishi wa kanisa ni mtu mwenye maadili.
15. Bainisha mashaidi utakao taka washuhudie wosia wako na kusaini ambao watashuhudia maelekezo yako kipindi haupo au umekata kauli.taja majina yao sharti wawe watu wazima.
(hapa wanatakiwa awe ndugu mmoja ,rafiki mmoja na mtu baki mmoja ,mashaidi wanatakiwa watoke katika makundi tofauti ili kuleta usawa katika taarifa).
16. Baada ya kugawa mali zako ,ni vyema ukatoa sababu ya kwa nini umegawa kulingana na ulivyotaka hii ni nzuri inaonesha wazi haukubagua ,haukulazimishwa na ulitenda hayo kwa kadri ya mapenzi yako na utashi wako.
17. Unaweza mshirikisha mwenza wako au la pia utoe sababu kwa nini haujapenda kumshirikisha kuandaa wosia .
sababu utakayo itoa itasaidia kujua dhamila yako na vile ambavyo ulimpima mwenza wako kwa kadri ya tabia ,maamuzi ,na namna ya kulinda mali tajwa...hivyo itapunguza kuwa na hoja za kupinga wosia kwa hoja za upungufu wa akili au chuki binafsi ,kwa kuwa umeweka sababu bayana inaonesha ulikuwa reasonable and sound mind wakati unaanda wosia.
18. Bainisha wosia wako ungependa uhifadhiwe wapi ? Mf rita,kanisani,mahak**ani ,bank au kwa mtu binafsi mf msimamizi wa wosia au mwanasheria nk
19. Hakikisha nyaraka zote za mali ni sahihi na hazina dosari kabla ya kugawa na unazimiliki kialali kwa mujibu wa sheria.
20. Epuka kugawa mali za kurithi ambazo ni za jumuiya pasipo kubainisha kwa maelezo ya kina namna ambavyo una uhalali nazo.
21. Kumbuka kusema warithi wakabidhiwe mali husika katika wosia wakifikisha umri gani.k**a wanao rithi ni watoto wadogo .
22. Kumbuka kubainisha mapato yote yatakayotokana mali zako ambazo umewarisisha watoto zitumikeje na kwa utaratibu upi mpaka ambapo watoto watakapofikia uwezo wa kukabidhiwa interm of age and ability to control the property.maelezo k**a ifunguliwe akaunti ya watoto au mtoto juu ya mahitaji yake ni muhimu.
23. Custodian of child ni muhimu kubainisha ukiwa haupo watoto au mtoto wako akae na nani na kwa nini na ikitokea kuna shida nani aseme maamuzi ya mwisho juu ya hatima ya mali na uangalizi wa watoto wakati umri wa watoto ukisubiria kufika waweze kukabidhiwa mali ulizo warisisha.
24. MTANGULIZE MUNGU KATIKA HATUA HII, ILI AKUONGOZE UANDAE WOSIA WAKO KWA HEKIMA NA HAKI .
Wako katika sheria kwa niaba ya BRILLIANT PARTNER ESQ.
CLEMENCE NGOWI
0714751918
Call now to connect with business.