Jukwaa La Sheria

Jukwaa La Sheria NAWE UTAIFAHAMU SHERIA NA SHERIA ITAKULINDA !!!

ZIJUE AINA ZA MIKATABA YA KAZIUle msemo usemao kazi nzuri ukiwa hujaipata na huwa mbaya ukiwa nayo unaweza ukaonyesha uh...
26/01/2018

ZIJUE AINA ZA MIKATABA YA KAZI

Ule msemo usemao kazi nzuri ukiwa hujaipata na huwa mbaya ukiwa nayo unaweza ukaonyesha uhalisia wakati unapaswa kufahamu ni aina ipi ya mkataba wa ajira uliosainiwa kati ya mwajiri na mwajiriwa.

Kwa mujibu wa sheria ya mikataba mkataba ni makubaliano kati ya pande mbili yenye nguvu ya kisheria kwa lugha nyingine makubaliano ambayo pande zote mbili zinawajibika kisheria. Mkataba ni moja ya mambo muhimu sana kati ya haki za mfanyakazi wakati mwingine kuliko hata kiasi cha fedha na marupurupu anayopaswa kulipwa.

Mkataba wa kazi hutoa mwelekeo wa ajira ya mfanyakazi, huonyesha usalama wa ajira, haki na wajibu wa mfanyakazi pamoja na haki na wajibu wa mwajiri, kueleza majukumu ya msingi ya mfanyakazi, muda na mahali pa kazi na maswala mengine muhimu kwa mujibu wa sheria.

Kukosekana kwa mkataba wa kazi huhatarisha usalama wa ajira yenyewe. Hivyo ni wajibu wa kila mwajiri na mwajiriwa kuhakikisha anapata mkataba wa ajira ikiwezekana hata kabla hajaanza kufanya kazi yenyewe na kulipwa mshahara wake wa kwanza.

Pamoja na uwepo wa kipindi cha matazamio (probation period) lakini hilo haliondoi wajibu wa kuwepo kwa mkataba wa kazi. Baadhi ya waajiri wasio waaminifu wamekuwa wakitumia kipindi cha matazamio k**a kigezo cha kutompa mfanyakazi mkataba wa kazi bila kutambua kwamba inawezekana kabisa mtu akasaini mkataba wa kazi na mkataba ukaeleza kuwa kipindi cha matazamio kitakuwa ni cha muda gani japo kisheria hakipaswi kuzidi miezi sita. Pia ndani ya kipindi cha matazamio mwajiri anayo haki ya kusitisha mkataba wa kazi endapo hataridhishwa na utendaji wa mfanyakazi au kwa sababu nyingine zozote zinazokubalika na ambazo ni halali kisheria.

Aina ya mkataba wa kazi huonyesha mustakabali wa kazi yenyewe, humpa mfanyakazi na mwajiri fursa ya kufahamu haki na wajibu wa kila upande na hivyo kujenga mazingira mazuri ya utekelezwaji wake kwa kulinda maslahi ya kila upande.

Mkataba wowote ule unaoingiwa kati ya pande mbili ni lazima uwe na vigezo vikuu vya mkataba ikiwemo makubaliano ya pande mbili, malipo halali, lengo halali, uwezo wa kuingia mkataba na hiari. Bila kujali ni aina ipi ya mkataba wa kazi mliosaini, k**a kimojawapo kati vigezo vikuu vya uhalali wa mkataba kitakosekana kinaweza kuufanya mkataba wenyewe kuwa batili tangu mwanzo.

Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 mikataba ya ajira iko ya aina tatu ambayo ni; Mkataba usiokuwa na muda maalum, mkataba wa muda maalum kwa wataalam na kada ya uongozi pamoja na mkataba wa kazi maalum.

Mkataba usiokuwa na muda maalum ni mkataba ambao unasainiwa kati ya mwajiri na mwajiriwa ambao unaweza kuonyesha tarehe uliyosainiwa lakini hauonyeshi au hauelezi kuwa utaisha lini. Mikataba ya namna hii mara nyingi huwa katika taasisi za umma na baadhi ya taasisi binafsi.

Aina ya pili ya mkataba wa kazi ni mkataba wa muda maalum kwa kada ya uongozi. Aina hii ya mkataba huusisha zaidi kada ya uongozi au mwajiriwa mwenye fani ya aina fulani ambaye huajiriwa kushika wadhifa fulani wa juu katika utekelezaji wa majukumu yake.

Hata hivyo aina nyingine za waajiriwa wanaweza pia kuwa na mkataba wa muda maalum bila kujali kada anayotoka kulingana na mahitaji maalum ya mwajiri.

Aina ya tatu ya mkataba wa kazi ni mkataba kwa kazi maalum. Mkataba huu unaweza kupewa kipindi maalum cha kuisha au mara nyingi kuisha kwake hutegemea kuisha kwa kazi husika ambazo mwajiri na mwajiriwa watakuwa wamekubaliana kutekeleza.

Hii yaweza kuhusu utekelezaji wa mradi Fulani au shughuli maalum ambayo kuisha kwake ndiyo huashiria kufikia mwisho kwa mkataba wa ajira.

Jambo la muhimu na la kuzingatia ni kwamba kifungu cha 15 cha sheria ya ajira na mahusiano kazini, 2004 kinamtaka kila mwajiri na mwajiriwa kuhakikisha kuwa kabla ya kuanza kazi, kuna mkataba wa maandishi uliosainiwa kati ya pande hizo mbili.

Pamoja na uwezekano wa kuwepo na makubaliano kati ya mwajiri na mfanyakazi ya kuwa na mkataba ulio chini ya mwaka mmoja lakini makubaliano hayo yanapaswa yafanyike kwa sababu za msingi na si kwa lengo la kujaribu kumnyima mfanyakazi baadhi ya haki zake zilizopo kisheria. Baadhi ya waajiri huingia kwenye makubaliano mapya ya mkataba na mfanyakazi kila baada ya miezi mitatu au sita ili kukwepa baadhi ya gharama zikiwemo kodi na malipo watakayowajibika kumlipa mfanyakazi kwa mujibu wa sheria jambo ambalo halikubaliki kisheria.

Mkataba ndio utakaoeleza aina ya shuguli utakazofanya, mipaka, unawajibika kwa nani, malipo yako, haki zako za msingi, namna ya kuvunja mkataba na maswala mengine muhimu ambayo hamuwezi kukubaliana tu kwa maneno. Kukosekana kwa mkataba wa maandishi kunahatarisha ulinzi na usalama wa haki na wajibu wa mwajiri na mwajiriwa. Usikubali kuanza kazi bila mkataba.

Usikubali kusaini mkataba bila kuusoma na kuuelewa na pia ni muhimu kujua umeingia mkataba wa aina gani kati hizo aina tatu nilizoeleza hapo juu, ili ujue haki na wajibu wako kisheria na namna gani maslahi yako k**a mwajiri au mwajiriwa yanaweza yakalindwa pasipo vikwazo vya aina yoyote.

ADVOCATE JUSTINE KALEB
CEO/LEGAL CONSULTANT
MORIAH LAW CHAMBERS,
MAVUNO HOUSE - POSTA MPYA,
(OPPOSITE TO TOTAL PETROL STATION),
1ST FLOOR - OFFICE NO. 102,
P.O. BOX 70849,
DAR ES SALAAM - TANZANIA - EAST AFRICA.
MOB: +255 755 545 545 600 / +255 713 636 264
TEL: +255 222 110 684
EMAIL: [email protected]
FACEBOOK: Moriah Law Chambers

MAMBO SABA YA KUJIULIZA KABLA YA KUKOPESHA (JUSTINE KALEB - 0755545600/0713636264)Kukopesha ni kitendo cha kumpa mtu, ki...
05/01/2018

MAMBO SABA YA KUJIULIZA KABLA YA KUKOPESHA
(JUSTINE KALEB - 0755545600/0713636264)

Kukopesha ni kitendo cha kumpa mtu, kikundi cha watu au taasisi kiasi fulani cha fedha au mali kwa makubaliano ya kurejesha fedha hizo baada ya muda zikiwa pamoja na riba au k**a jinsi zilivyo. Pia kukopesha ni kuazimisha mali au fedha kwa mtu ambaza atawajibika kurejesha ndani ya muda mliokubaliana kwa masharti mliyokubaliana.

Kukopesha huleta ladha nzuri ya mafanikio kifedha wakati wale wanaokopeshwa wanapokuwa waaminifu kurejesha fedha hizo kwa wakati. Kukopesha hukuza mtaji kwa haraka, hulinda thamani ya pesa yako na huongeza mzunguko wa pesa na kukuza uchumi. Huwafanya watu kutimiza malengo yao na huwa chanzo cha mitaji kwa watu wengine na kuvutia faida kubwa ndani ya muda mfupi.

Kutorejeshwa kwa fedha hizo za mkopo ndani ya muda mliokubaliana na mkopaji huleta ishara ya aidha kutolipwa kabisa fedha hizo au kulipwa nje ya muda ambapo thamani yake itakuwa imeshuka tofauti na mlivyokubaliana hapo awali. Kutorejeshwa kwa mkopo huleta hasara, huchelewesha kutimia kwa malengo ya mkopeshaji, huvunja mahusiano mazuri ya kibiashara yaliyojengwa kwa muda mrefu kati ya mkopaji na mkopeshaji na mkopeshaji asipokuwa mwangalifu anaweza kufilisika kwa sababu ya kukopesha watu ambao hawalipi.

Kukopa harusi, kulipa matanga ndio msemo unaoweza kukupa taswira nzuri ya mambo gani ujiulize kabla ya kukopesha. Wengine hujifariji kuwa mdaiwa hafungwi, kwa hiyo wanaweza wasikulipe na wasipate madhara yoyote kisheria, lakini wanajidanganya tu maana mdaiwa anaweza kufungwa. Sheria ya mwennendo wa Kesi za Madai, SURA 33 ya 2002 katika Jedwali la Kwanza, Kifungu cha XXI Kanuni ya 35 na 36 kwamba, mdaiwa anaweza kufungwa endapo atashindwa kulipa deni na ikiwa mdai ataiomba mahak**a imfunge mdaiwa na atakuwa tayari kugharamia gharama zake awapo gerezani. Hivyo mahak**a baada ya kujiridhisha inaweza kuamuru mdaiwa ak**atwe afungwe k**a mfungwa wa madai (civil prison).

Usipokuwa makini kabla ya kukopesha unaweza ukajikuta unafirisika, unagombana na watu, ndoa yako inavunjika, undugu unaisha na urafiki uliodumu kwa muda mrefu unavunjika. Hii ni kwa sababu tu umeshindwa kujenga mazingira mazuri ya uwajibikaji kisheria kati yako na yule unayemkopesha. Hii haijalishi unamkopesha nani na kiasi gani unachokopesha.

Mali bila daftari hupotea bila habari. Ukishindwa kuweka kumbukumbu zako vizuri utapoteza pesa nyingi pasipo kujua na hatimaye kufilisika. Fedha haina undugu, ujamaa, kujuana wala urafiki. Ukitaka kufanikiwa kifedha na kudumisha mafanikio yako, lazima ujenge misingi imara ya kisheria itakayolinda fedha zako na kulinda maslahi ya vizazi vijavyo. Hivyo usikopeshe kwa kuangalia leo, bali kopesha kwa kuangalia kesho. Usiwe na maono ya kuku bali kuwa na maono ya tai yenye uwezo wa kuona miaka mingi ijayo na kuchukua tahadhari mapema iwezekanavyo.

Kwanza jiulize; je kuna mkataba wa maandishi kati yako na yule unayemkopesha? Hii ina maana usimkopeshe mtu kwa makubaliano ya mdomo tu. Hii haijalishi unamuamini kiasi gani. Katika maswala ya kifedha usimuamini mtu kupita kiasi, atakuja kukushangaza atakapokugeuka na kukuliza.

Pili jiulize je, mkataba huo umeshuhudiwa na wakili, hakimu au shahidi mwingine yeyote? Ni muhimu kuwa na mtu wa tatu k**a shahidi katika mkataba wenu, atasaidia kuutetea mkataba huo.

Tatu jiulize, je mtu huyo anayeingia mkataba huo ana mamlaka kisheria ya kuingia mkataba huo na je ndiye atakayewajibika katika urejeshwaji wa mkopo huo? Usije ukaingia mkataba na mtu mwingine na ukatarajia ulipwe na mtu mwingine, utakwama.

Nne jiulize, unafahamu anwani sahihi ya huyo unayemkopesha kwa maana ya anapoishi, ofisi yake, mawasiliano yake, mjumbe wake na mengineyo? Usimkopeshe mtu ambaye mmekutana tu barabarani, kanisani au msikitini. Siku akiacha kupita hiyo njia au kuja kwenye ibada umepoteza fedha zako. Fahamu nyumbani kwake, majirani zake na kiongozi wake wa serikali, mwajiri wake na ikiwezekana wafanyakazi wenzake.

Tano jiulize, je mtu huyo ana uwezo wa kulipa fedha hizo alizokopa ndani ya muda mliokubaliana? Usimkopeshe mtu kwa kumhurumia ili atatue shida zake tu, kopesha kwa maslahi ya kibiashara. K**a unajua kabisa mtu huyo hana uwezo wa kulipa pesa hizo ni bora usimkopeshe kuliko ukajiingiza kwenye migogoro isyokuwa ya lazima.

Sita jiulize, je mtu huyo ana dhamana yoyote ya mkopo huo au kuna mtu amejitolea kumdhamini ambaye asipolipa yeye ana uwezo wa kulipa deni hilo? Kukosekana kwa dhamana au mdhamini ni kuhatarisha ulinzi na usalama wa fedha zako.

Saba jiulize, endapo mtu huyo akifariki, akipata ulemavu wa kudumu au tatizo na hivyo kushindwa kurejesha mkopo huo utawezaje kurejesha fedha zako? Ukiona hupati majibu, tafakari mara mbili kabla hujakopesha.

Haya ni mambo ya msingi sana ya kujiuliza na kuyapatia majibu kwanza kabla hujatoa fedha zako kumkopesha yeyote yule. Ukiona huna majibu sahihi ya maswali hayo usithubutu kumkopesha mtu fedha. Sio lazima mkopeshe kila mtu, watu wengine ili muendelee kuwa na mahusiano nao mazuri inabidi usiwakopeshe. Hakikisha umeweka ulinzi wa kutosha wa fedha zako kurudi na faida kabla hujakopesha.

Bora lawama kuliko fedheha. Hata k**a utalaumiwa lakini fedha zako zitakuwa salama. Kwa taasisi zinazotoa mikopo ni muhimu kupata vibali vinavyokuruhusu kufanya hivyo na pia kulinda haki za mteja kisheria kwa kutomdharirisha, kumnyanyasa na kumfanyia fujo kwa sababu tu ameshindwa kuleta marejesho. Kumbuka kudaiwa hakumuondolei mtu haki zake za msingi kisheria.

HERI YA MWAKA MPYA - 2018. HUU UKAWE MWAKA WAKO WA KUFANYA ZAIDI KUPITA MIPANGO YANGO, MATARAJIO YAKO NA MATARAJIO YA MA...
01/01/2018

HERI YA MWAKA MPYA - 2018. HUU UKAWE MWAKA WAKO WA KUFANYA ZAIDI KUPITA MIPANGO YANGO, MATARAJIO YAKO NA MATARAJIO YA MAADUI ZAKO. PATA VITABU HIVI VIKUSAIDIE KUFIKA MBALI ZAIDI. PIGA SIMU NO. 0714636264/0756636264. UBARIKIWE !

16/04/2017

SHALOM MORIAH LAW CHAMBERS RESPECTFULLY WISHES ALL ITS CLIENTS & STAKEHOLDERS A HAPPY PASSOVER. MAY THIS PASSOVER SEASON CONFIRM, CONNOTE AND COMMEMORATE THE PASSOVER OF YOUR LIFE FROM A VICTIM TO A VICTOR, TESTS TO TESTIMONIES, SHAME TO FAME, FEAR TO FAVOR, AND FROM POVERTY TO RICHES DEUTERONOMY 8: 7-18

JE UNATAKA KUTOKA KWENYE SHIMO LA UMASKINI? BASI ANZA KUWEKA AKIBA. AKIBA NI MOJAWAPO YA NGAZI ZA KUPANDIA KUTOKA KWENYE...
22/10/2015

JE UNATAKA KUTOKA KWENYE SHIMO LA UMASKINI? BASI ANZA KUWEKA AKIBA. AKIBA NI MOJAWAPO YA NGAZI ZA KUPANDIA KUTOKA KWENYE SHIMO LA UMASKINI. AKIBA HAIOZI. AKIBA NI SILAHA YA VITA DHIDI YA UMASKINI. PAMOJA NA SHIDA, DHIKI, MADENI, KUPUNGUKIWA NA KUTOTOSHA KWA PESA ZAKO LAZIMA UWEKE AKIBA. ONA MBALI, WAZA KESHO NA UWEKE AKIBA. KILA AKIBA UTAKAYOWEKA ITAKUPA NGUVU, HAMASA NA MSUKUMO WA KUTOKA KWENYE UMASKINI.

JE UNATAKA KUTIMIZA NDOTO YAKO? K**A KWELI UNATAKA KUTIMIZA NDOTO YAKO USITHUBUTU KUKATA TAMAA. USIZIRE, USIACHE, USIKUB...
17/10/2015

JE UNATAKA KUTIMIZA NDOTO YAKO? K**A KWELI UNATAKA KUTIMIZA NDOTO YAKO USITHUBUTU KUKATA TAMAA. USIZIRE, USIACHE, USIKUBALI KUSHINDWA, USIKIMBIE MAPAMBANO NA WALA USIOGOPE CHANGAMOTO. WASHINDI HUWA HAWAKATI TAMAA NA WANAOKATA TAMAA HAWAWEZI KUSHINDA. NDOTO YAKO ITATIMIA K**A TU UTAENDELEA KUPAMBANA, KUSHINDANA, KUNG'ANG'ANA, KUSIMAMA NA KUTIMIZA DOTO YAKO.

JE UNATAKA KUFANIKIWA ? LAZIMA UKUBALI KULIPA GHARAMA. GHARAMA UTAKAYOLIPA ITAJENGA MSINGI IMARA NA USIOTIKISIKA WA MAFA...
15/10/2015

JE UNATAKA KUFANIKIWA ? LAZIMA UKUBALI KULIPA GHARAMA. GHARAMA UTAKAYOLIPA ITAJENGA MSINGI IMARA NA USIOTIKISIKA WA MAFANIKIO YAKO. HUWEZI KUFANIKIWA HARAKA HARAKA, GHAFLA GHAFLA, KIRAHISI RAHISI, KIUBWETE UBWETE, KIMTEREMKO, KIMAZINGAOMBWE AU KIMIUJIZA. BADILIKA ! ANZA LEO KULIPA GHARAMA, LAZIMA UTAFANIKIWA. 0756636264 / 0714636264.

JE UNAHITAJI MTAJI WA BIASHARA? MTAJI MKUBWA SANA KWENYE BIASHARA SIO FEDHA NI MAARIFA. MAARIFA NI NGUVU, MAARIFA HULETA...
14/10/2015

JE UNAHITAJI MTAJI WA BIASHARA? MTAJI MKUBWA SANA KWENYE BIASHARA SIO FEDHA NI MAARIFA. MAARIFA NI NGUVU, MAARIFA HULETA FEDHA NA MAARIFA NI FEDHA. UKIPATA FEDHA BILA MAARIFA, WENYE MAARIFA WATATUMIA FEDHA ZAKO KUJITAJIRISHA. KABLA HUJAANZA KUTAFUTA FEDHA TAFUTA KWANZA MAARIFA YA KUTOSHA KUHUSU BIASHARA YAKO. BADILIKA ! ( JUKWAA LA SHERIA NA BIASHARA UK. 33) JIPATIE NAKALA YAKO SASA. PIGA; 0756636264 / 0714636264.

JE UNATAKA KUWA HURU KIFEDHA? BADILIKA KUWA MJASIRIAMALI. UJASIRIAMALI HUKUPA UHURU WA KUJIPANGIA KIPATO CHAKO. WEWE NDI...
13/10/2015

JE UNATAKA KUWA HURU KIFEDHA? BADILIKA KUWA MJASIRIAMALI. UJASIRIAMALI HUKUPA UHURU WA KUJIPANGIA KIPATO CHAKO. WEWE NDIYE UNAYEAMUA UPATE KIASI GANI WAKATI GANI. HAKUPANGII MTU NA HUHITAJI KUSUBIRI MWISHO WA MWEZI. KILA SIKU NI SIKU YA MSHAHARA, NI JUHUDI ZAKO TU. (JUKWAA LA SHERIA NA BIASHARA UK. 24) JIPATIE NAKALA YAKO KWA TSH. 10,000/= TU. PIGA 0756636364 / 0714636264.

IGNORACIA JURIS NON EXCUSAT IS A LATIN MAXIM WHICH MEANS IGNORANCE OF LAW IS NOT AN EXCUSE. YOU CANT DEFEND YOURSELF FRO...
12/06/2015

IGNORACIA JURIS NON EXCUSAT IS A LATIN MAXIM WHICH MEANS IGNORANCE OF LAW IS NOT AN EXCUSE. YOU CANT DEFEND YOURSELF FROM BEING LEGALLY RESPONSIBLE AND ACCOUNTABLE JUST BECAUSE OF YOUR IGNORANCE OF LAW.

Address

POSTA MPYA, MAVUNO HOUSE, 1ST FLOOR, OFFICE NO. 102B
Dar Es Salaam
P.O.BOX70849DARESSALAAM

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Jukwaa La Sheria posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Jukwaa La Sheria:

Share