TPDC Tanzania

TPDC Tanzania natural gas,tpdc,Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania,wizara ya nishati na madini,gas,oil,mafuta,gesi,Tanzania Petroleum Development

Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) is the National Oil Company of Tanzania through which the Ministry of Energy and Minerals implements its petroleum exploration and development policies. TPDC has a manpower strength of about 400 and is organized into seven directorates and three Units, namely: Directorate of Upstream, Directorate of Downstream, Directorate of Finance, Directorate o

f Legal Services, Directorate of Cooperate Strategy and Planning, Directorate of Corporate Management, Directorate of Internal Audit, Communication Unit, Procurement Unit and Risk Management Unit. TPDC was established through the Government NoticeNo.140 of 30th May 1969 under the Public Corporations Act No.17 of 1969. The Corporation began operations in 1973. TPDC is a wholly owned Government parastatal, with all its shares held by the Treasurer Registrar.

TPDC 2026 || MakabidhianoShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi rasmi karakana ya kisasa ya kuongez...
05/06/2026

TPDC 2026 || Makabidhiano
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi rasmi karakana ya kisasa ya kuongeza mfumo wa gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) kwenye magari kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Juni 5, 2026, yakilenga kuimarisha matumizi ya nishati safi na kukuza ujuzi nchini. Gharama na Makubaliano ya Mradi Ujenzi wa karakana hiyo umegharimu shilingi bilioni 1.52 za Kitanzania na umejengwa ndani ya eneo la Kituo Mama cha kujaza gesi asilia (CNG Mother Station) kilichopo UDSM.
Mradi huu ni utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na mkataba wa upangishwaji ardhi uliosainiwa kati ya taasisi hizo mbili tangu mwaka 2022. Ujuzi na Mafunzo ya Vitendo kwa Wanafunzi Mbali na kutoa huduma za ufungaji na matengenezo ya mifumo ya CNG kwenye magari, karakana hiyo itatumika k**a kituo cha mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi wa uhandisi wa UDSM.
Hatua hii itasaidia kujenga wataalamu wazalendo na kuandaa wanafunzi wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira katika sekta ya nishati. Manufaa ya Kiuchumi na Kimkakati. Karakana hiyo ina vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kupunguza gharama za usafiri kwa wananchi wanaotumia magari, huku ikichochea utafiti na ubunifu wa nishati. Huu ni sehemu ya mkakati wa Serikali unaotekelezwa na TPDC katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi, nafuu na salama nchini.

TPDC 2026 || DodomaShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani ...
05/06/2026

TPDC 2026 || Dodoma
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, likitoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya gesi asilia, miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika pamoja na mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa.
Akitembelea banda la TPDC, Mhe. Naibu Waziri wa Maji (Mb), Mhandisi Kundo Mathew, amepongeza juhudi za TPDC katika kusambaza na kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, akieleza kuwa hatua hiyo inasaidia kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa ambao ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya uharibifu wa mazingira na ukataji miti.
Katika maonesho hayo, TPDC inaendelea kutoa elimu kuhusu miradi ya utafutaji, uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na matumizi ya gesi asilia, pamoja na nafasi ya sekta ya mafuta na gesi katika kuongeza mapato ya Serikali, kuvutia uwekezaji, kuimarisha usalama wa nishati na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Wananchi wanaotembelea banda la TPDC wanapata fursa ya kujifunza kuhusu mchango wa gesi asilia katika uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwandani, usafiri na matumizi ya majumbani, sambamba na nafasi yake katika kuhifadhi mazingira kupitia matumizi ya nishati safi.

TPDC 2026 || Eid Al adha
27/05/2026

TPDC 2026 || Eid Al adha

TPDC 2026 || Jeshi la PolisViongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wamefanya ziara ya kutembelea miundombinu mbali...
26/05/2026

TPDC 2026 || Jeshi la Polis
Viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wamefanya ziara ya kutembelea miundombinu mbalimbali ya gesi asilia inayosimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuendelea kuwajengea uwezo kuhusu usimamizi na ulinzi wa miundombinu ya kimkakati ya taifa.
Ziara hiyo inahusisha viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi wakiwemo Mak**anda Wakuu wa Wilaya (OCD) pamoja na mak**anda kutoka mikoa yote yenye miundombinu ya gesi asilia. Mnamo tarehe 25.05.2026, viongozi hao walitembelea miundombinu ya kupokelea gesi asilia katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam, ambapo walipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika eneo hilo pamoja na umuhimu wa miundombinu hiyo katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati nchini.
Aidha, viongozi hao walipata pia fursa ya kutembelea Kituo Mama cha Kujaza Gesi Asilia kwenye Magari (CNG Mother Station) kinachomilikiwa na TPDC kilichopo eneo la Mawasiliano jijini Dar es Salaam, ambapo walijionea namna teknolojia ya matumizi ya gesi asilia kwenye magari inavyotekelezwa pamoja na mchango wake katika matumizi ya nishati safi, salama na yenye gharama nafuu.
Ziara hiyo itaendelea kwa kutembelea miundombinu mingine muhimu ikiwemo bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba mkoani Mtwara pamoja na visima vya kuzalisha gesi asilia vilivyopo Kata ya Msimbati mkoani humo.
Ziara hiyo inalenga kuongeza uelewa wa viongozi hao kuhusu shughuli za uzalishaji, uchakataji, usafirishaji na matumizi ya gesi asilia pamoja na kuimarisha ushirikiano katika kulinda miundombinu hiyo ya kimkakati ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa taifa.

TPDC 2026 || MazungumzoShirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikishwaji ...
25/05/2026

TPDC 2026 || Mazungumzo
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi katika kulinda miundombinu ya bomba la gesi asilia, likieleza kuwa usalama wa rasilimali hiyo ni jukumu la kila mwananchi na msingi wa maendeleo endelevu ya taifa.

TPDC imekuwa ikitekeleza programu ya elimu kwa wananchi katika vijiji vilivyopo kwenye maeneo yanayopitiwa na miundombinu ya bomba la gesi asilia mkoani Pwani, hususan wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga, ili kuongeza uelewa na kuwajengea uwezo wananchi wa kutambua na kuripoti mapema vitendo au shughuli zozote zinazoweza kuhatarisha usalama wa miundombinu hiyo.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa TPDC, Bi. Ashura Hoja alisisitiza kuwa ulinzi wa bomba la gesi unahitaji mshik**ano wa jamii yote.

“Bomba la gesi asilia ni rasilimali ya taifa. Kila mwananchi ana wajibu wa kuwa mlinzi. Tunawahimiza wananchi kutoa taarifa mapema wanapoona shughuli zisizo za kawaida karibu na miundombinu hii,” alisema.

TPDC imewapongeza wananchi wa maeneo husika kwa kuonesha mwamko wa kushiriki katika ulinzi huo, lakini pia imewataka kuongeza umakini zaidi, kwani uharibifu wowote unaweza kuathiri huduma muhimu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Bw. Kassimu Iddi mwananchi wa kijiji cha Jaribu Mpakani Wilaya ya Kibiti alisema elimu hiyo imekuwa chachu ya mabadiliko ya mtazamo katika jamii.

“Sasa tunaelewa kuwa kulinda bomba la gesi ni kulinda maisha yetu na maendeleo ya taifa letu. Tumeamua kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu hii,” alisema Kassimu.

TPDC imeendelea kutoa wito kwa jamii zote zilizopo karibu na bomba la gesi kuwa sehemu ya mfumo wa ulinzi wa pamoja, ili kuhakikisha miundombinu hiyo inalindwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

19/05/2026

TPDC 2026 || Ulinzi wa bomba la gesi
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea kuimarisha ushirikiano na jamii kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya bomba la gesi asilia katika vijiji vya Mkwalia Kitumbo na Sunguvuni, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo, Afisa Mwandamizi wa Maendeleo ya Jamii wa TPDC, Bw. Oscar Mwakasege amesema programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa shirika wa kushirikisha jamii katika kulinda miundombinu ya gesi asilia katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi salama ya maeneo yanayopitiwa na bomba la gesi asilia pamoja na kuwajengea uwezo wa kutambua viashiria vinavyoweza kuhatarisha usalama wa miundombinu hiyo muhimu ya taifa.

“Lengo letu ni kuhakikisha wananchi wanaelewa umuhimu wa bomba la gesi asilia, namna ya kulilinda na kutoa taarifa mapema wanapoona viashiria vya uharibifu au shughuli zisizo salama karibu na miundombinu hiyo,” alisema Bw. Mwakasege.

Wananchi walioshiriki katika mikutano hiyo wameipongeza TPDC kwa kuwafikia moja kwa moja vijijini na kutoa elimu inayosaidia kulinda rasilimali za taifa huku ikijenga uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya usalama.

Zoezi la utoaji wa elimu kwa Umma litaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya juhudi za TPDC za kuimarisha usalama wa miundombinu ya gesi asilia na kujenga mahusiano mazuri kati ya shirika hilo na jamii inayozunguka mradi wa gesi asilia.

TPDC 2026 || Ukaguzi wa KitaluTPDC tumekuwa hapa katika Bonde hili la Eyasi Wembere na kuanza shughuli hizi za utafiti  ...
18/05/2026

TPDC 2026 || Ukaguzi wa Kitalu
TPDC tumekuwa hapa katika Bonde hili la Eyasi Wembere na kuanza shughuli hizi za utafiti tangu Mwaka 2015 na hadi sasa kazi tuliyofanya imegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 47,468,496,207.77 ambazo zote zimetoka ndani ya shirika letu la TPDC.
Maamuzi ya kutekeleza mradi huu yametokana na sifa za Kitalu ambacho kinatupa uhakika uwezekano wa kupata rasilimali ya mafuta kwa vile eneo hili kijiolojia linafana sana na eneo la Lake Albati na Turkana ambayo yote yapo kwenye ukanda wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki ambapo tayari wenzetu wameweza kugundua mafuta.
Aidha kitalu hiki kimepitiwa na Mradi wa Bomba la Mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) ambalo litatuwezesha kulitumia kusafirisha mafuta yetu pindi tutakapogundua na hivyo kuleta msukumo zaidi wa utekelezaji wa shughuli za utafiti katika eneo hili.
Pamoja na hayo jambo kubwa ambalo linatupa nguvu ya maamuzi ya kutekeleza mradi huu ni uwezo ambao shirika letu limewajengea wataalamu wake ambapo kwa sasa shirika lina uwezo wa kuendesha na kusimamia shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia nchini tofauti na hapo awali ambapo tulikua tunategemea watalaam kutoka makampuni ya nje kufanya shughuli hizi na hivyo basi mradi huu ni kielezo cha ufanisi na utaalamu ulioko ndani ya shirika.
Balozi Ombeni Sefue, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC.

Address

Azikiwe/Jamhuri Street
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TPDC Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TPDC Tanzania:

Share