03/07/2017
👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿*GEREZA LA KIHISTORIA LA 'WATUKUFU' WA UHALIFU*
Unapozungumzia simulizi za kusisimua kuhusu ulimwengu wa jela na wafungwa basi huwezi kumaliza na hakika utakuwa mtovu wa nidhamu k**a utaacha kuweka kwenye orodha yako gereza tata na maarufu Nchini Marekani la Alcatraz!
Yes, Alcatraz nyumbani kwa watukufu wa uhalifu
Marekani miaka hiyo.
Gereza hili linapatikana katika jimbo la California kwenye ghuba ya San Fransisco katika kisiwa cha Alcatraz. Alcatraz lilifunguliwa rasmi mwaka 1934 baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa sana, na hadi mwaka 1935 tayari lilikuwa na wafungwa 242 kutoka maeneo tofauti tofauti na profile tofauti tofauti za kihalifu kabla ya kufungwa rasmi 21 March 1963!
*Ulinzi na mazingira kuzunguka Alcatraz*
Gereza hili lilikuwa na urefu wa kilomita 2.7, upana wa kilomita 1.5 na urefu wa mita 3.1 kwenda juu, huku likigawanywa katika blocks nne, block A, B, C na D, chumba cha Mkuu was Gereza, chumba ya wageni, Maktaba na Saluni ya kunyolea wafungwa, huku block "D" likiwa ndio block hatari zaidi kwa msoto kiasi kwamba pamoja na uhalifu wao katika uhalifu, watukutu hawa waliligwaya sana block hili!.
Gereza lilizungushiwa fence za umeme, electric detectors, radios na guard towers. Kikubwa zaidi ni kwamba gereza lilijengwa kwenye kisiwa kilichozungukwa na maji ya baridi mno panda zote na mkondo mkali sana!
Mazingira haya ndio yaliyolifanya gereza hili kuwa la kipekee na kuaminika kuwa gumu kuliko yote kwa mfungwa kutoroka! Hivyo kuonekana sahemu salama kabisa kwa watemi hawa kuishi, " Special to hold the worst of the Criminals"!
They didn't give up! It is
Hii ndo the Alcatraz! You either live as a walking dead inside or try to escape and meet a real death!!
Wasaalam!