Zechariah Wakili Msomi

Zechariah Wakili Msomi Public Legal Practitioner and Consultant

If the law is against a lawyer, the lawyer will argue the facts. If the facts are against a lawyer, the lawyer will argu...
18/02/2026

If the law is against a lawyer, the lawyer will argue the facts. If the facts are against a lawyer, the lawyer will argue the law. If both the facts and the law are against a lawyer, the lawyer will argue procedure

People ask how do I become a billionaire? 🤷‍♂️"Change the life of a billion people and by definition you'll become a bil...
17/08/2024

People ask how do I become a billionaire? 🤷‍♂️

"Change the life of a billion people and by definition you'll become a billionaire."

Look at Zuckerberg, Bill gate, Steve Jobs? They didn't finish school but yet... the rest is history.

Jinsi ya kusajili kampuni, nyaraka zinazotakiwa, gharama za usajili, vigezo na mambo ya kuzingatia kabla na baada ya kus...
11/08/2024

Jinsi ya kusajili kampuni, nyaraka zinazotakiwa, gharama za usajili, vigezo na mambo ya kuzingatia kabla na baada ya kusajili kampuni nchini Tanzania

(Procedures for the registration of companies, costs for registration and things to take into account before and after registration of a company in Tanzania).

Mwandishi: Zechariah Wakili Msomi
(Advocate/Wakili)
[email protected]
(0612275246 au 0754575246 WhatsApp).

1: Tuanze na MAMBO YA KUZINGATIA MWANZONI KABLA YA KUANZA KUSAJILI KAMPUNI

Kabla ya kuanza kusajili kampuni unatakiwa uandae au uwe na vitu vifuatayo karibu:

{i}: Hakikisha unafahamu sheria na kanuni zinazohusu usajili na uendeshaji wa Makampuni katika nchi au eneo lako. K**a huelewi tafuta wataalamu waliosomea hayo mambo. Mfano Mwanasheria n.k.

{ii) Hakikisha unafahamu gharama za kusajili na kuendesha kampuni, ikiwa ni pamoja na gharama ada za kisheria, kodi n.k.

(iii) Tafuta jina la Kampuni (company Name). Chagua jina la kampuni ambalo halijatumika au halifanani na jina la kampuni nyingine yoyote. Unaweza kufanya upekuzi (search) kwenye mfumo wa BRELA kwa kufanya name clearance ili kujihakikishia k**a jina unalotaka kutumia halifanani au k**a limeshasajiliwa na kampuni nyingine au bado. Na k**a una jila la kampuni ila haujawa tayari kusajili au unahofia litatumika na mtu mwingine unaweza kuomba kulinda jina la kampuni BRELA.

{iv}: Aina ya kampuni (Company Type):
Chagua aina ya kampuni unayotaka kusajili, mfano kampuni ya umma (public company) au kampuni binafsi (private company), kampuni ya kigeni (foreign company).

{v}: Idadi na majina kamili ya wanachama (members) wa kampuni.

{vi}: Kitambulisho cha taifa kwa kila mwanachama (National Identification Number/NIDA) au pasi ya kusafiria (passport kwa raia wa kigeni).

{vii} Anwani ya makazi (address), barua pepe (email) na namba za simu (mobile phone numbers) za kila mwanachama wa kampuni. Kwa eneo ambalo limepimwa (surveyed), unatakiwa ujue namba ya kiwanja (plot number), block number, mtaa, kata, wilaya, mkoa, namba ya nyumba n.k.

{viii} Malengo ya Kampuni (Objectives of the company)..Tafakari juu ya aina ya biashara au kazi unazohitaji kampuni yako kufanya.

{ix} Chagua Mahali au Makao Makuu ya Kampuni (Registered office of the Company). Fahamu ni wapi kampuni yako itafanyia kazi au eneo itakapokua ofisi ya kampuni. Eneo la ofisi linaweza kuathiri kodi na upatikanaji wa soko.

{x} Anwani (address), namba ya simu na barua pepe (email) ya kampuni).

{xi} Majina ya wakurugenzi wa Kampuni (Directors of the company.

{xii} Namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mkurugenzi (director) wa kampuni.

{xiii} Jina la katibu wa kampuni (Company secretary).

{xiv} Mtaji wa kampuni k**a kampuni ina mtaji (share capital)

{xv} Kuandaa Katiba ya Kampuni. Ukishandaa hivyo vitu vyote sasa inafata hatua nyingine ya kuandaa nyaraka. Andaa Katiba ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association au kwa kifupi tunaita MEMARTs) ambayo itaelezea malengo ya kampuni, haki na wajibu wa wanahisa (shareholders) na jinsi kampuni itakavyoendeshwa. Memart sharti isainiwe na kugongwa muhuri wa Mwanasheria/Wakili.

2: HATUA YA KUSAJILI KAMPUNI:

K**a kila kitu kiko tayari Pamoja na Katiba ya kampuni ingia kwenye mfumo wa BRELA uanze kujaza hizo taarifa tulizotaja hapo juu kwa ajili ya kuendelea na Usajili wa kampuni.

Kwa Tanzania, usajili wa Makampuni unafanyika mtandaoni kupitia MFUMO WA USAJILI KWA NJIA YA MTANDAO (Online Registration System/ORS) kwenye tovuti (website) ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Zifuatazo ni hatua za kusajili kampuni nchini Tanzania (procedures for the registration of companies in Tanzania):

{i} Tengeneza kwanza akaunti kwenye mfumo wa Usajili wa makampuni kwa njia ya mtandao (Online Registration System/ORS) kwa kutembelea tovuti (website) ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

K**a ikiwa una akaunti tayari, ingia kwenye mfumo kwa kutumia jina lako la mtumiaji (username) na neno la siri (password).

Ukishafungua akaunti utaenda sehemu inayohusika na kusajili makampuni, mfumo utakuruhusu kuanza kufanya maombi ya usajili wa kampuni.

{ii} Jaza taarifa za kampuni yako k**a vile jina la kampuni, aina ya kampuni, ofisi ya kampuni, wakurugenzi wa Kampuni, katibu wa kampuni, mtaji wa kampuni, idadi ya hisa na thamani ya kila hisa, malengo au shughuli ambazo kampuni inakusudia kufanya n.k.

Zingatia: Malengo ya kampuni (objectives) unayochagua kwenye mfumo wa BRELA lazima yafanane na yale uliyojaza kwenye Katiba ya Kampuni (Memorandum and articles of association).

Ukimaliza kujaza taarifa za kampuni yako kwenye mfumo, mfumo utakuletea nyaraka/fomu mbali mbali za kuambatanisha. Kuna fomu ya majumuisho (consolidated form) yenye maelezo (information) zote ulizojaza kwenye mfumo na fomu ya uadilifu (integrity form). (Fomu nyingine ni fomu namba 14(b).

{iii} Pakua (download) na kusaini hizo nyaraka.
Kuna nyaraka au fomu zinatakiwa kusainiwa na wakurugenzi (directors) na secretary (katibu) wa kampuni pamoja Mwanasheria/Wakili.

{iv} Scan na Kupakia nyaraka zote kwenye mfumo. Ukishasaini nyaraka zako zote, unatakiwa uzi-scan kila nyaraka peke yake ziweke katika mfumo wa PDF alafu zipakie kwenye mfumo kila moja sehemu yake.*

Nyaraka za kuambatanisha:

Katiba ya Kampuni (MEMARTs)
Fomu ya majumuisho (Consolidated Form).
Fomu ya uadilifu (integrity form)
Form namba 14(b). (Zingatia: Katiba ya Kampuni na fomu namba 14(b) lazima visainiwe na kugongwa muhuri wa Mwanasheria/Wakili).

{v} Lipia gharama ya maombi ya kusajili kampuni. Baada ya kupakia nyaraka zako kwenye mfumo na kuendelea mbele, mfumo utakupeleka kwenye ukurasa wa kufanya malipo. Utapewa control number (namba ya kulipia) kwa ajili ya kufanya malipo. Utachagua aina au njia unayotaka kutumia kufanya malipo. Unaweza kulipia kupitia Bank au unaweza kulipa kwa simu.

{vi} Maombi kuwasilishwa na kufanyiwa kazi BRELA. Baada ya kufanya malipo, maombi yako yatatumwa na mfumo kwa ajili ya kufanyiwa kazi BRELA kisha utasubiri kusajiliwa na kupewa cheti cha usajili (certificate of incorporation) au kurudishiwa maombi kwa ajili ya marekebisho k**a kuna kitu hakiko sawa.

{vii} Kufatilia maendeleo ya maombi yako kwenye mfumo. Baada maombi yako kutumwa na mfumo kwa ajili ya kufanyiwa kazi BRELA, endelea kuingia kwenye mfumo mara kwa mara kuangalia maendeleo ya maombi yako yalipofikia. Au kucheki k**a kuna marekebisho yoyote umeambiwa ufanye.

{viii} Kupakua cheti cha kusajiliwa kwa kampuni (download and print certificate of incorporation). K**a kila kitu Kiko sawa maombi yako yatashughulikiwa. Utatumiwa cheti chako kwenye akaunti yako uliyofungua kwenye mfumo wa BRELA. Kisha hatua ya mwisho utaingia kwenye mfumo na kupakua cheti cha usajili wa kampuni yako. Cheti hiki kinathibitisha kuwa kampuni yako imesajiliwa rasmi nchini Tanzania.

3: GHARAMA ZA KUSAJILI KAMPUNI:

Kuna gharama za Serikali (BRELA) na gharama za Wakili (mwanasheria) atakayekusaidia kufanya maombi ya kusajili kampuni k**a utakuwa umetumia Wakili (mwanasheria) n.k. Tuanze na gharama za Serikali. Ada hutofautiana kulingana na aina ya kampuni unayotaka kusajili na thamani ya hisa za kampuni:

Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni zaidi ya Tsh. 20,000/= lakini si zaidi ya Tsh. 1,000,000/= Tsh. 95,000 /=

Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni zaidi ya Tsh. 1,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh. 5,000,000/= Tsh. 175,000 /=

Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni zaidi ya Tsh. 5,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh. 20,000,000/= Tsh. 260,000 /=

Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni zaidi ya Tsh. 20,000,000/= lakini si zaidi ya Tsh. 50,000,000/= Tsh. 290,000 /=

Kampuni ambayo thamani ya hisa zake halisi ni zaidi ya Tsh. 50,000,000/= Tsh. 440,000 /=

Kampuni ambayo haina mtaji wa hisa = Tsh. 300,000 /=

Ada ya kufungua jalada kwa ajili ya maombi, Tsh.. 22,000/= kwa kila waraka, yaani Malengo na Katiba ya Kampuni. Tsh. 66,000/=

Gharama ya kila Ushuru wa stempu (stamp duty) katika kila nakala ya Malengo na Katiba ya Kampuni = Tsh. 10,000/=

Gharama za ushuru wa stempu katika Fomu namba 14b = Tsh. 1,200/=

Kulinda jina la kampuni ni Tsh. 50,000 /=

Kubadilisha jina la kampuni Tsh. 22,000 /=

Gharama ya kupata nakala ya Cheti cha Usajili Tsh. 4,000 /=

GHARAMA ZA MWANASHERIA AU WAKILI:

Gharama za mwanasheria au Wakili itategemea umempa kazi ya ukubwa gani mfano kukuandalia nyaraka (MEMARTs) na kuzigonga muhuri tu, au pamoja na kuendelea na zoezi zima la kufanya maombi ya usajili kwenye mfumo au kuendelea kufatilia vibali/leseni na matakwa mengine ya kisheria baada ya kusajili kampuni lako n.k.

Hata hivyo gharama za kumlipa Wakili (Mwanasheria) kwa kazi yoyote ile ikiwemo kazi ya maombi ya kusajili kampuni, zimeanishwa kwenye sheria maalum inaitwa the Advocates Remuneration Order, 2015.

4: MAMBO YA KUZINGATIA BAADA YA KUSAJILI KAMPUNI:

Nafikri hapa sasa ndo mahali pa muhimu sana kuliko hata mwanzo. Wengi wakishamaliza kusajili kampuni wanalala na ku relax. Wanasahau kwamba kuna utitiri wa mambo ya kuzingatia kisheria na yasiyo ya kisheria baada tu ya kumaliza kusajili kampuni. Fahamu kwamba kampuni ni moja kati ya biashara ambayo inadhibitiwa mno na sheria (iko very much regulated).

Baada ya kampuni kusajiliwa na kupata cheti cha usajili (certificate of incorporation), yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia la sivyo utaiona kampuni chungu:

(i) Hakikisha tena unafahamu sheria na kanuni zinazohusu usajili na uendeshaji wa Makampuni. K**a huelewi tafuta wataalamu waliosomea hayo mambo mfano wanasheria, wahasibu n.k.

(ii) Pili, hakikisha unapata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN Certificate) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

JINSI YA KUPATA TIN (NAMBA YA UTAMBULISHO WA MLIPA KODI):

Zamani utaratibu ilikua baada ya kusajili kampuni unapewa certificate of incorporation ambayo ni tofauti na TIN number. Kwa hiyo mtu ulikua ukitoka BRELA unaingia mtandaoni (online) kwenye tovuti ya TRA kuomba TIN ambayo unapewa namba nyingine tofauti.

Lakini kwa sasa wameamua kubadilisha na kuweka ushirikiano kati ya mfumo wa TRA na BRELA ili kwamba ile namba ya usajili (incorporation number) ya kampuni unayopewa BRELA baada ya kusajili kampuni, inakuwa hiyo hiyo ndiyo TIN ya kampuni.

Kwa sasa mifumo ya BRELA na TRA imekua linked, hivyo kampuni ikishasajiliwa BRELA na kupewa namba ya usajili (incorporation number) na TIN ya kampuni inatoka papo hapo. Ile namba ya cheti cha usajili wa kampuni (incorporation number) inakua ndiyo namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ya kampuni yako. (Na kuanzia muda huo kampuni inakuwa na wajibu wa kulipa kodi TRA).

Hivyo unachotakiwa kufanya baada ya kusajili kampuni ni kutembelea ofisi ya TRA na kuwasilisha nyaraka mbalimbali za usajili wa kampuni kwa ajili tu ya kuthibitisha (ku verify) TIN ya kampuni ili upewe cheti cha TIN original hardcopy na TRA.

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOENDA KUOMBA TIN YA KAMPUNI TRA:

Wakati unaenda TRA kuomba (kuthibitisha) TIN ya kampuni unatakiwa kwenda na vitu vifuatavyo:

Kwanza unatakiwa kwenda ofisi ya TRA ndani ya mkoa wa kikodi au ndani ya eneo ofisi ya kampuni lako ilipo.

Unatakiwa kupeleka barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa kuthibitisha kuwa kweli unafanya biashara eneo hilo.

Peleka nakala/kopi za TIN na vitambulisho vya wakurugenzi (directors) wa kampuni k**a NIDA au passport n.k.

Mkataba wa pango wa eneo unapofanyia biashara uliogongwa muhuri wa Mwanasheria/Wakili (ambao utaupeleka TRA wakukadirie kodi ya pango/rental tax na stamp duty).

Nakala/kopi ya katiba ya kampuni (Memorandum and Articles of Association).

Cheti cha Usajili wa Kampuni (Certificate of Incorporation) na kiwe na muhuri wa Mwanasheria/Wakili.

(iii) Kitu kingine baada ya kusajili kampuni unatakiwa kuwasilisha taarifa za wamiliki manufaa (beneficial ownership) BRELA.

(iv) Kuwasilisha marejesho ya kodi (file tax returns) TRA na kulipa kodi zinazotakiwa TRA. Tumeona kampuni ikisajiliwa tu na TIN ya kampuni inatoka papo hapo. Kuanzia muda huo kampuni inakua ina wajibu wa kuanza kulipa kodi zote zinazohusiana na kampuni. Usipofanya hivyo utapigwa adhabu (penalty) za kutosha mpaka utaiona kampuni chungu.

Sasa, kuna marejesho (returns) ya kila mwezi (monthly returns) na marejesho ya kila mwaka (annual returns). Baadhi ya kodi hizo ni k**a ifuatavyo:

Skills and Development Levy (SDL). (Hii inalipwa au ina tozwa kwa kampuni ambayo ina wafanya kazi zaidi ya 10).

Statement and Payment of Tax Withheld for Employees (PAYE). Hii inatozwa au inalipwa na wafanyakazi wa kampuni. Lakini kampuni ndiyo inatakiwa kuwakata wafanyakazi wake na kuhakikisha inawasilisha TRA.

Marejesho ya kila mwaka (annual returns) k**a vile Statement of Estimate of Tax Payable by Instalments on Behalf of Entity (Kodi ya makadirio). Kampuni ikishasajiliwa inapewa miezi mitatu mitatu ya kuwasilisha kodi ya makadirio. Hata k**a kampuni haitegemei kuingiza mapato yoyote huo mwaka bado inatakiwa kuwasilisha marejesho (ku file return).

Withholding Tax

Stamp Duty

Value Added Tax (VAT)

Na kadhalika (e.t.c)

(v) Kuomba leseni ya biashara. Baada ya kumalizana na BRELA na TRA unatakiwa kufatilia leseni au vibali husika. Kuna leseni zinaombwa BRELA na zingine Manispaa. Itategemeana na aina ya shuguli za kampuni yako.

(vi) Kununua mashine ya EFD kwaajili ya kutoa risiti kwa wateja wako.

(vii) Kufungua Bank akaunti namba ya Kampuni.

HATUA ZA KUFUNGUA BENKI AKAUNTI NAMBA YA KAMPUNI:

Lazima kuwe na kikao cha kampuni ipitishe azimio (resolution) ya kuazimia kufungua akaunti ya Benki na kuchagua nani watakuwa watia sahihi (signatories), kwamba muoneshe ili hela zitoke wanatakiwa kusaini watu wangapi? Labda directors wote wawili au director mmoja na secretary.

Chagua tawi la benki mnapotaka kufungua akaunti.

Andika barua ya kuomba kufungua akaunti kwenye bank mtakayokua mmekubaliana, barua hiyo pia inatakiwa kutaja majina ya watu wenye mamlaka ya kusaini ili hela zitoke.

Cheti cha usajili wa kampuni kutoka BRELA.

Nakala za vitambulisho.

TIN

Leseni ya biashara iliyo hai.

(viii) Kusajili Kampuni kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (⁠NSSF), ⁠WCF n.k. Sajili wafanyakazi wako na mifuko ya hifadhi ya jamii k**a vile NSSF n.k.

(ix) Kutafuta mshauri wa kisheria na Mhasibu.
Ni vizuri kuwa na mshauri wa kisheria na mhasibu ili kuhakikisha unafuata sheria na unafanya maamuzi sahihi ya kifedha.

-----MWISHO----

Disclaimer: Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. K**a unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mwanasheria

Makala hii ya jinsi ya kusajili Makampuni nchini Tanzania imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Wakili Msomi
[email protected]
(0612275246 Halotel)
(0754575246 WhatsApp).

Ukifungua kesi ya ardhi ambayo kiwanja kimesajiliwa au kina hati, unatakiwa kumshtaki pia na Msajili wa hati (Registrar ...
15/07/2024

Ukifungua kesi ya ardhi ambayo kiwanja kimesajiliwa au kina hati, unatakiwa kumshtaki pia na Msajili wa hati (Registrar of titles). Kushindwa kumuunganisha au kumshtaki Msajili kwenye kesi ambayo ardhi ina hati ni kumnyima haki ya kusikilizwa. Na hukumu yoyote itakayotolewa kwenye hiyo kesi bila Msajili kuunganishwa itakua ni batili.

Hii ni kwa mujibu wa maamuzi ya Mahak**a ya Rufani kwenye kesi ya NESTORY MSOFFE & 5 OTHERS Vs THE REGISTERED TRUSTEES OF CATHOLIC ARCHDIOCESE OF ARUSHA CIVIL APPEAL NO. 254 OF 2019.

Je, hata k**a sina ugomvi au malalamiko kuhusu usajili au mtu kupewa hati kwenye kiwanja chenye mgogoro bado kuna haja ya kumuunganisha na Msajili? Kesi hii haijajibu hilo swali, lakini kesi zingine zinasema utamuweka Msajili k**a tu malalamiko yako yanahusu kusajiliwa au kupewa hati kwenye eneo lenye mgogoro. ( Zechariah Wakili Msomi )

Sherehe ya 70 ya mahafali ya kuwakubali na kuwapokea mawakili wapya leo hii, Julius Nyerere International Convention Cen...
03/07/2024

Sherehe ya 70 ya mahafali ya kuwakubali na kuwapokea mawakili wapya leo hii, Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam 🎓

Unapoandaa affidavit au kiapo unatakiwa kuapa juu ya mambo ambayo yako kwenye ufahamu wako binafsi tu. Soma Order XIX ru...
23/05/2024

Unapoandaa affidavit au kiapo unatakiwa kuapa juu ya mambo ambayo yako kwenye ufahamu wako binafsi tu. Soma Order XIX rule 3(1) Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (CPC) inasema, " ..." Hata hivyo, unaruhusiwa kuapa taarifa ambazo haziko kwenye ufahamu wako ila hakikisha unataja chanzo chake.

Kwenye sehemu ya uthibitisho wa kiapo chako au hata ukiandaa nyaraka yoyote ambayo ina kifungu cha kuapa/uthibitisho/verification clause mfano plaint, wakati unathibitisha unatakiwa utaje bayana, aya zipi ni taarifa unazozijua wewe binafsi na k**a kuna taarifa za kuambiwa, ainisha aya zipi ni habari za kuambiwa na ni nani aliyekuambia na utamke kabisa kuwa hayo uliyoambiwa unayaamini kuwa ni kweli.

Ukithibitisha tu juu juu eti "yote niliyosema hapo juu ni kweli tupu kadiri ya ufahamu wangu binafsi" ukaishia hapo wakati kuna aya umechanganya na taarifa za kuambiwa, kiapo chako kinakua batili. "The law does not allow a blanket or rather a general verification" Na ukithibitisha kuwa yote niliyosema ni kweli tupu kadiri ya ufahamu wangu binafsi na imani (belief) bila kutaja aya zipi zinatokana na imani (belief) na chanzo chake, kiapo chako kitakua batili.

Hii ni kwa mujibu wa kesi nyingi sana ikiwemo hii ya Mahak**a ya Rufani, kati ya ANATOL PETER RWEBANGIRA na PRINCIPAL SECRETARY, MINISTRY OF DEFENCE AND NATIONAL SERVICE, CIVIL APPLICATION NO. 548/04 OF 2018. (Hakuna nyaraka ngumu kuandaa k**a kiapo. K**a intern humwamini usimpe hii kazi. Haya ni machache tu kati ya masharti ya affidavit (kiapo)). Zechariah Wakili Msomi ([email protected])

Hati ya madai (plaint) ndio msingi wa kesi yako. Unapofungua kesi Mahak**ani hakikisha umeandika malalamiko au hoja zako...
22/05/2024

Hati ya madai (plaint) ndio msingi wa kesi yako. Unapofungua kesi Mahak**ani hakikisha umeandika malalamiko au hoja zako zote kwenye hati yako ya madai (plaint). K**a kuna hoja au nyaraka yoyote ambayo unatarajia kuisema Mahak**ani hakikisha umeiweka au umeitaja kabisa kwenye plaint.

Hoja au nyaraka ambayo hujaizungumzia popote kwenye hati yako ya madai (plaint) ndo basi tena, hautaruhusiwa kuizungumzia tena baadae katikati ya kesi au wakati unatoa ushahidi. Nyaraka zako zitakufunga mikono na zinaifunga na Mahak**a pia (parties are bound by their Pleadings and the Court is bound by the Pleadings of the parties).

Kujaribu kutolea ushahidi jambo au nyaraka ambayo mwanzo haukuiongelea mahali popote kwenye hati yako ya madai (plaint) au kwenye hati ya utetezi wako (WSD) ni kujaribu kubadilisha kesi angani. Hauruhusiwi kabisa kutoka nje ya ulichokiandika tangu mwanzo kwenye hati ya malalamiko (plaint) au utetezi (WSD). (Ikiwa mtu atafanya hivyo basi ni sababu nzuri hata ya kukatia rufaa). Lengo ni kuzuia kuviziana na kushtukizana Mahak**ani.

Hii ni kwa mujibu wa kesi nyingi sana za Mahak**a Kuu na Mahak**a ya Rufani, ikiwemo hii hapa chini ya RICHARD JOSEPH RUSISYE Vs IBRAHIM SALUM SUUD, LAND CASE NO. 167 OF 2020 (HC at DSM)
Zechariah Wakili Msomi ([email protected])

Kwa sasa ukifungua kesi Mahak**a Kuu, tumia au andika SUB REGISTRY (MASJALA NDOGO) na sio DISTRICT REGISTRY k**a tulivyo...
21/05/2024

Kwa sasa ukifungua kesi Mahak**a Kuu, tumia au andika SUB REGISTRY (MASJALA NDOGO) na sio DISTRICT REGISTRY k**a tulivyokua tunaandika zamani.

Hii ni kutokana na marekebisho ya Sheria ya mwaka 2021 na 2024 ambapo kanuni za Masjala za Mahak**a Kuu (the High Court Registries Rules) zimefanyiwa marekebisho kwa kufuta neno "DISTRICT REGISTRY" na kuweka "SUB REGISTRY. Soma the High Court Registries (Amendment) Rules, 2021 na the High Court Registries (Amendment) Rules, 2024.

Marekebisho ya mwaka 2024 sheria inasema, "the principal Rules are amended by deleting the words “DISTRICT REGISTRY” wherever they appear in the principal Rules and substituting for them the word “SUB-REGISTRY ”. Marekebisho haya pia ndiyo yamefuta Masjala Kuu (Main Registry) ya Mahak**a Kuu Dar es Salaam na kuihamishia Dodoma.

Hivyo, kwa Sasa proper Citation ya Mahak**a Kuu ni Sub-Registry na sio District Registry. Unatakiwa kuandika hivi "In the High Court of the United Republic of Tanzania (Dar es Salaam Sub-Registry) at Dar es Salaam.

Tofauti na hapo, ukitumia DISTRICT REGISTRY, kisheria utakua ni k**a umeifungua kesi kwenye Mahak**a ambayo haipo na unaweza kuwekewa pingamizi la kisheria.
Zechariah Wakili Msomi (0754575246)

*JINSI YA KUKAZA AU KUTEKELEZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:*Mwandishi: *Zechariah Wakili Msomi*Zakariamaseke@gmail.comUnap...
19/05/2024

*JINSI YA KUKAZA AU KUTEKELEZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:*

Mwandishi: *Zechariah Wakili Msomi*
[email protected]

Unaposhinda kesi ya madai, mfano umefungua kesi na hukumu imetoka umeshinda kesi, labda Mahak**a imesema ulipwe au urudishiwe nyumba, hauishii hapo tu, ili uweze kulipwa au kupata hiyo nyumba inabidi uombe ex*****on (utekelezaji wa hukumu) wengine wanaita KUKAZIA HUKUMU. Ni k**a unafungua kesi ya pili kumtaka mdaiwa aitekeleze ile hukumu.

Lakini inategemea, *k**a mdaiwa anakubali kulipa bila shuruti hakuna haja ya kurudi Mahak**ani kufungua maombi ya kukazia hukumu. Utarudi Mahak**ani kutafuta msaada wa amri ya Mahak**a k**a tu mdaiwa hataki kulipa kwa amani.*

Sasa kuna tofauti ya jinsi ya kukazia hukumu za Mahak**a ya Mwanzo na hukumu za Mahak**a zingine k**a Mahak**a ya Wilaya, Mahak**a ya Hakimu Mkazi na Mahak**a Kuu. Utofauti upo kwenye procedures (hatua), documents (nyaraka) na sheria (laws applicable).

Eneo hili kuna changamoto. Unaweza kuwa unaelewa vizuri jinsi ya kukazia hukumu ya Mahak**a zote ila ya Mahak**a ya Mwanzo ikakuchanganya. Na hii ni kwa sababu Mahak**a ya mwanzo haifundishwi sana vyuoni wala law school. Lakini vivyo hivyo unaweza kuwa unaelewa vizuri jinsi ya kukazia hukumu za Mahak**a ya Mwanzo ila za Mahak**a za juu zikakuchanganya.

*Kwenye makala hii utajifunza mambo yafuatayo:*

1: Jinsi ya kukazia hukumu ya Mahak**a ya Mwanzo
2: Sheria zinazotumika katika utekelezaji au kukazia hukumu za Mahak**a ya Mwanzo.
3: Njia unazoweza kutumia kuitekeleza hukumu Mahak**a ya mwanzo.
4: Nyaraka zinazotumika kutekeleza hukumu Mahak**a ya Mwanzo.

1: *JINSI YA KUKAZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO (HOW EX*****ON IS DONE IN PRIMARY COURTS)?*

*Hapa tunaangalia Procedure na documents (hatua na nyaraka).*

K**a ilivyo kwa Mahak**a zingine, hatua ya kwanza *unatakiwa kuomba kutekeleza (kukazia) hukumu Mahak**ani. Yule aliyeshinda kesi anatakiwa kupeleka maombi ya kukazia hukumu Mahak**ani.

Unaombaje kukazia hukumu (how)? Kwa maana ya unatumia njia gani? Kwa mdomo au kwa maandishi? K**a ni maandishi hiyo nyaraka inaitwaje?

*Kumekua na ubishani sana eneo hili, baadhi wanasema unatumia barua wengine wanasema unajaza fomu maalum ambayo utapewa pale Mahak**ani au ambayo iko kwenye sheria inayotoa fomu maalumu zinazotumika katika mashauri ya Mahak**a za Mwanzo inaitwa “the Magistrates’ Court (Approved Forms for the Primary Court) Rules, 2020”*

(Kwa Mahak**a zingine, maombi ya kukazia hukumu yanaweza kufanyika kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi (written form). Kwa mdomo k**a madai yako yanahusu pesa (monetary decree) na huyo unayemdai mpo naye Mahak**ani wakati amri ya Mahak**a ya kumtaka alipe inatolewa. Uksioma Order XXI rule 10(1), (1A). Na kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum, FOMU NAMBA TANO (5) ambayo format au muundo wake unapatikana kwenye sheria inaitwa, Civil Procedure (Approved Forms) Notice, GN. No. 388 of 2017. (Hapa naongelea hizo Mahak**a zingine).

Swali, je kwa upande wa Mahak**a ya Mwanzo unatumia document (nyaraka) gani? Hilo swali nitalijibu kwenye kipengele cha mwisho.

*2: SHERIA ZINAZOTUMIKA KUKAZIA HUKUMU YA MAHAKAMA YA MWANZO:*

Utaratibu wa kukazia hukumu za Mahak**a ya Mwanzo unapatikana kwenye sheria zifuatazo:

*(i) The Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11.* (Sheria ya Mahak**a za Mahakimu, sura ya 11). Hii ndiyo sheria mama ya Mahak**a za Mwanzo. Kwa upande wa kesi za madai sheria hii imetaja mamlaka ya Mahak**a ya Mwanzo kwenye jedwali la nne (fourth schedule) la sheria hiyo.

*(ii) “The magistrates’ Courts (Civil Procedure in Primary Courts) Rules. Kwa kiswahili naweza kuziita Kanuni za Mwenendo wa Kesi za Madai Mahak**a ya Mwanzo).* Soma part III kuanzia Rule 56 - Rule 85.
Hii ni sheria ndogo (ni kanuni) zilizotungwa chini ya sheria ya Bunge (Act) inayoitwa Sheria ya Mahak**a za Mahakimu (the Magistrates’ Courts Act kwa kifupi tunaiita ‘MCA’).

Kwa hiyo usitumie Civil Procedure Code (CPC) (Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai) Mahak**a ya Mwanzo. CPC haitumiki Mahak**a ya mwanzo isipokua katika mazingira maalum/machache saana (very rare and exceptional circumstances).

*(iii) The Magistrates’ Court (Approved Forms for the Primary Court) Rules, 2020”.* Hii ni sheria inayotoa fomu mbalimbali zinazotumika katika mashauri ya Mahak**a za Mwanzo, zikiwemo fomu maalum kwa ajili ya kukazia hukumu.

*3: NJIA ZA KUTUMIA KUKAZA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:*

Unaweza kukaza hukumu ya Mahak**a ya Mwanzo kwa njia zifuatazo;

*(i) Kuk**ata na kuuza mali ya mdaiwa (attachment and sale).* Soma Rule/Kanuni ya 56 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahak**a ya Mwanzo na Aya ya 3(2) ya jedwali la nne la sheria ya Mahak**a za Mahakimu (Paragraph 3(2) of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).

*Hakikisha mali unayotaka kuk**ata na kuuza inaruhusiwa kuk**atwa kisheria.* Kujua mali ipi haiwezi kuk**atwa na kuuzwa soma Rule/Kanuni ya 63 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahak**a ya Mwanzo na Paragraph 3(2) ya jedwali la nne la sheria ya Mahak**a za Mahakimu (of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).

*(ii) Kurejesha na kukabidhi mali (Restitution and delivery of property).* Soma Rule/Kanuni ya 58 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahak**a ya Mwanzo

*(iii) Eviction (kutolewa ndani ya eneo husika).* Soma Rule/Kanuni ya 58 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahak**a ya Mwanzo

*(iv) Seizure of the property (kushikilia mali).* Hakikisha mali unayotaka kushika inaruhusiwa na sheria. Soma Rule/Kanuni ya 56 ya Kanuni za hizo hizo.

Ikitokea mdai anataka kushika au ameshika au amek**ata mali ambayo hairuhusiwi kushikwa au sio yako wewe mdaiwa utafungua maombi ya kuweka pingamizi Mahak**ani. Soma Rule/Kanuni ya 69 ya Kanuni za mwenendo wa kesi za madai Mahak**a ya Mwanzo

Na ikitokea mdai anataka kushika au ameshika au amek**ata mali ya mtu mwingine ambaye sio mdaiwa au asiyehusika na kesi utaratibu ni k**a ule ule wa Mahak**a zingine, unafungua kesi ya pingamizi (objection proceedings) kupinga mali yako kuingizwa kwenye kukaza hukumu. Soma Rule/Kanuni ya 70.

Ikitokea mali yako imeuzwa kwenye mnada kimakosa ili kutekeleza hukumu unaweza kuomba kutengua hayo mauzo. Kwa Mahak**a ya Mwanzo utaratibu upo kwenye sheria yao hiyo hiyo niliyotaja mwanzo, “the magistrates’ Courts (Civil Procedure in Primary Courts) Rules.” (Kanuni za Mwenendo wa Kesi za Madai za Mahak**a ya Mwanzo). Utaratibu na Mambo yote yanayohusu kukazia au kutekeleza hukumu za Mahak**a ya Mwanzo yapo part III kuanzia Rule 56 - Rule 85 ya hiyo sheria.

(v) Njia nyingine ni kumk**ata mdaiwa na kumfunga jela k**a mfungwa wa madai (arrest and detention as Civil Prisoner). Soma Aya ya 4 ya jedwali la nne la sheria ya Mahak**a za Mahakimu (Paragraph 4 of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).

K**a ulifikri deni halimfungi mtu basi unajidanganya. Dawa ya deni ni kulipa tu hakuna namna nyingine.

K**a ilivyo kwa Mahak**a zingine zote, vivyo hivyo ukishindwa kulipa deni k**a ilivyoamriwa na Mahak**a ya Mwanzo, mdai akitafuta mali zako akakosa, basi mdai anaweza kuomba mdaiwa uk**atwe na kufungwa gerezani k**a mfungwa wa madai.Hii ndiyo njia inayotumika pale ambapo mdaiwa ni mtata ana uwezo wa kulipa deni ila hataki kulipa makusudi.

*Wengine wanadhani njia hii inatumika mwishoni kabisa pale ambapo mdai amejaribu njia zote kudai kulipwa imeshindikana,* lakini hilo linaweza isiwe kweli. Kwa sababu Majaji wanatofautiana sana katika kutafsiri sheria. Kuna baadhi ya Majaji wanasema huwezi kukimbilia kuanza kuomba kukaza hukumu kwa kumk**ata mdaiwa k**a mfungwa wa madai kabla hujajaribu njia zingine za kawaida. *Lakini Majaji wengine wanasema unaweza kuanza na aina yoyote ile unayotaka kukaza hukumu hata k**a ni kumk**ata mdaiwa. Ili kuondoa huko mkanganyiko kasome kesi za Mahak**a ya Rufaa ambayo maamuzi yake yanawafunga mikono Majaji wote wa Mahak**a Kuu na Mahak**a zote za chini yake.*

Hata hivyo, kuna utofauti kidogo ikiwa utaamua kukaza hukumu kwa njia ya kukumk**ata mdaiwa na kumfunga jela k**a mfungwa wa madai. Ukisoma Aya ya 4 ya jedwali la nne la sheria ya Mahak**a za Mahakimu (Paragraph 4 of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11) inasema (nanukuu);

*“A primary court may, on the application of the party entitled to the benefit of such order in any civil proceedings, request a district court to take steps for the arrest and detention of any person who has failed to comply with an order for the payment of any amount, including compensation or costs, made by such primary court, and, upon receiving any such request, the district court shall have such jurisdiction and powers to order the arrest and detention of such order as if an application were made for the arrest and detention in the civil Prison of a judgment debtor in accordance with the provisions of the Civil Procedure Code.”*

Kwamba, mdai anatakiwa kuiomba Mahak**a ya Mwanzo kumk**ata na kumfunga jela mdaiwa k**a mfungwa wa madai, (hata hivyo mahak**a ya Mwanzo haina mamlaka ya kutoa amri hiyo), badala yake Mahak**a ya Mwanzo itatakiwa tena kuiomba MAHAKAMA YA WILAYA ichukue hatua za kumk**ata na kumfunga jela huyo mdaiwa ambaye ameshindwa au amegoma kulipa deni la watu.

Hapa pia kuna ubishani, baadhi wanasema huna haja ya kuiomba Mahak**a ya Mwanzo kumk**ata mdaiwa na kumfunga jela k**a mfungwa wa madai kwa sababu Mahak**a ya Mwanzo haina mamlaka ya kutoa amri hito, hivyo wanasema unatakiwa kupeleka maombi moja kwa moja kule Mahak**a ya Wilaya ambayo ndo ina mamlaka. Na documents wanasema ni chamber summons na affidavit!

Wengine wanasema lazima upite kwanza Mahak**a ya Mwanzo, alafu Mahak**a ya Mwanzo yenyewe ndo itaona kuwa haina mamlaka na kuchukua faili na kulipeleka Mahak**a ya Wilaya. Alafu wewe utaenda Mahak**a ya Wilaya kila kitu utakikuta huko.

Wengine wanasema Mahak**a ya Wilaya ikishaona haina mamlaka, itatoa amri ya kukupa go ahead ya kwenda Mahak**a ya Wilaya, alafu wewe utaenda kufungua maombi ya kutekeleza hukumu Mahak**a ya Wilaya kwa kumk**ata mdaiwa na kumfunga jela k**a mfungwa wa madai, documents utatumia chamber summons na affidavit, utaambatanisha na ile amri na mwenendo wa Mahak**a ya Mwanzo.

Na wengine wanasema Mahak**a za Wilaya zimekua zikikataa mafaili kutoka Mahak**a ya Mwanzo, zinayarudisha na kuwaambia Mahak**a ya Mwanzo waendelee na kutekeleza hukumu hata k**a njia inayotakiwa kutumika ni kumk**ata mdaiwa na kumfunga jela k**a mfungwa wa madai.

Sasa kipi ni kipi? Sina haja ya kueleza maana sheria iko wazi nimeshaeleza huko juu na nikanukuu kabisa. *Soma tena paragraph 4 of the fourth schedule to the Magistrates’ Courts Act (MCA) Chapter 11).*

Mwisho wa siku njia za kutekeleza hukumu ya Mahak**a ya Mwanzo ni k**a zile zile za Mahak**a zingine. Tofauti ni sheria na procedures.

4: Kipengele cha mwisho ni NYARAKA ZINAZOTUMIKA KUOMBA KUKAZIA HUKUMU MAHAKAMA YA MWANZO:

Wengine wanasema barua na wengine fomu. Kipi ni kipi? Kwa kweli wote wako sahihi kabisa.

Mchakato wa kukazia au kutekeleza hukumu Mahak**a ya Mwanzo unakua initiated (unaanza) na kundika barua ya kuomba kukazia hukumu. Alafu baada ya hapo maombi yatapelekwa kwa Mheshimiwa Hakimu ambaye anahusika kusikiliza maombi ya kutekeleza hukumu (anaitwa hakimu mfawidhi/in charge).

Baada ya hapo watakufungulia faili la shauri la kukazia hukumu, utapewa summons (wito wa kuitwa shaurini) utampelekea mdaiwa huo wito ili afike Mahak**ani kujibu maombi, baada ya hapo k**a hataki kulipa kwa amani, utaieleza Mahak**a unaomba kutekeleza hukumu kwa njia gani? Utajaza fomu Maalum ya kuomba kukaza hukumua labda kwa kuk**ata mali za mdaiwa au kumfunga jela n.k. kutegemea na wewe umechagua njia gani. Utalipia gharama za Mahak**a alafu mambo mengine yataendelea.

K**a utachagua kumk**ata mdaiwa na kumfunga gerezani, bado utaanza kwa kuandika barua kuiomba Mahak**a ya Mwanzo kutekeleza Hukumu. Ila utakapowaambia unataka utumie hiyo njia ya kumk**ata mdaiwa na kumfunga mdaiwa au njia yoyote ambayo Mahak**a ya Mwanzo haina mamlaka, wakishaona hawana mamlaka watakuambia uende Mahak**a ya Wilaya.

Je, *kuna haja ya kuambanisha decree (tuzo) na hukumu (judgement) kwenye kukazia hukumu ya Mahak**a ya Mwanzo? Kwa Mahak**a zingine hakuna namna unaweza kutekeleza hukumu au hata kukata rufaa bila kuwa na decree (tuzo).*.Lakini kwa Mahak**a ya Mwanzo hawana utaratibu huo kabisa, walau unaweza kuweka hukumu lakini decree haipo. Hata ukikata rufaa k**a kesi imeanzia Mahak**a ya Mwanzo hakuna ulazima wa kuambatanisha nakala ya hukumu au tuzo (decree) na haitakiwi kabisa lakini sasa kuna saa Masjala/Makarani wanaweza kukomaa na wewe wanakwambia lazima uambatanishe hukumu, kwa hiyo huwa tunaweka kukwepa usumbufu.

Kwa ufupi sana hizo ndo procedures na namna za kukazia hukumu kwa upande wa Mahak**a ya Mwanzo.

Lipo andiko lingine k**a hili refu zaidi ambalo nimeongelea jinsi ya kukazia na kutekeleza hukumu za Mahak**a za juu k**a vile Mahak**a ya Wilaya, Hakimu Mkazi na Mahak**a Kuu. Unaweza kulitafuta mtandaoni.

Asante kwa muda wako.

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zechariah Wakili Msomi ([email protected])
(0754575246 WhatsApp).

-----MWISHO----

Ntoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili. Unaruhusiwa tu kusambaza lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.

Disclaimer: *Lengo la hii makala ni kutoa elimu kwa jamii. Huu sio ushauri wa kisheria kwa mtu yeyote. K**a unahitaji ushauri wa kisheria wasiliana na Mawakili. (Ikiwa kuna sehemu hujaelewa omba ufafanuzi au uliza swali, kuuliza ni bure kabisa).

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke
Wakili / Advocate
(0754575246 - WhatsApp).
[email protected].

Address

Oyster Bay
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 08:00 - 15:00
Tuesday 08:00 - 15:00
Wednesday 08:00 - 15:00
Thursday 08:00 - 15:00
Friday 08:00 - 15:00
Sunday 09:00 - 15:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zechariah Wakili Msomi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Zechariah Wakili Msomi:

Share

Category