Pwani Trends

Pwani Trends Your Coast, Your News, Your Vibes! WhatsApp: 0758160696, Call: 0783868397 or email: [email protected]
(2)

Get the latest trends, juicy gossip, crime updates, breaking news, and side-splitting MEMEs from the Coast region of Kenya, all in one spot!

“ENOUGH IS ENOUGH!” 💧🔥«"Wiki mbili sasa bila maji huku kampuni za usambazaji maji zikiwa kimya. Cha kushangaza ni kuona ...
06/09/2026

“ENOUGH IS ENOUGH!” 💧🔥

«"Wiki mbili sasa bila maji huku kampuni za usambazaji maji zikiwa kimya. Cha kushangaza ni kuona biashara ya water buzzer ikiendelea kunoga. Hizi buzzer zinatoa wapi maji?"»

— Concerned Citizens

🚨 “HIZI WATER BUZZER ZINATOA WAPI MAJI?” WANANCHI WAIBUA MASWALI MAZITO KUHUSU MGOGORO WA MAJI 💧👀

Hasira za wananchi zinaendelea kuongezeka baada ya wiki mbili za ukosefu wa maji huku kampuni za usambazaji zikilaumiwa kwa ukimya wao. Kilichozua maswali zaidi ni kuonekana kwa malori ya kusambaza maji yakiendelea kufanya biashara k**a kawaida, jambo ambalo limewafanya baadhi ya wakazi kuhoji chanzo cha maji hayo wakati huduma rasmi zikidaiwa kusitishwa.

Mjadala sasa umehama kutoka kwenye ukosefu wa maji kwenda kwenye maswali ya nani anafaidika zaidi wakati wananchi wanahangaika kutafuta huduma hiyo muhimu. Je, ni bahati mbaya tu kwamba biashara ya water buzzer inanoga wakati mabomba yamekauka, au kuna kitu ambacho wananchi hawajaambiwa? 🤔💧

Bujra wa Kwale aripotiwa kupata ajali
06/09/2026

Bujra wa Kwale aripotiwa kupata ajali

“BUJRA AMEPATA AJALI MBAYA YA BARABARANI” — MAGWAYA NDANI

Muunda maudhui Magwaya Ndani ameripoti kuwa muunda maudhui mwenzake wa Kwale, Bujra wa Jimbo Media, amepata ajali mbaya ya barabarani na kwa sasa anapelekwa hospitalini.

Jamii ya Pwani, tuungane kumuombea Bujra katika kipindi hiki kigumu? 🙏🏽

🚨 NAJMA MANGI AZIDISHA MASHAMBULIZI, HASIRA ZA WANANCHI KUHUSU MAJI ZAMIMINIKA KWENYE COMMENTS 💧👀Kadri mgogoro wa maji u...
06/09/2026

🚨 NAJMA MANGI AZIDISHA MASHAMBULIZI, HASIRA ZA WANANCHI KUHUSU MAJI ZAMIMINIKA KWENYE COMMENTS 💧👀

Kadri mgogoro wa maji unavyoendelea kuwauma wakazi wa Kilifi, Hon Najma Mangi ameongeza presha kwa viongozi wa sekta ya maji kwa kudai uwazi zaidi kuhusu ukusanyaji wa mapato, malipo ya bili na usimamizi wa huduma. Kauli yake iligusa hisia za wananchi wengi ambao walijitokeza kwa wingi kwenye comments kueleza machungu yao kuhusu mabomba makavu licha ya kuendelea kulipa bili kila mwezi.

💥 Babae Brown Thomas:
"Huezi imba tu tamu ya Mung'aro na Kilifi haina maji."

💥 Alfan Mwinyi:
"Hawa watu wametuzoea sana, wanafanya vile wanataka."

💥 Kenneth Shungu:
"Hatujawahi kumbana na kitu k**a hii."

💥 Duncan Bongo:
"MD ni Catherine Baya..."

💥 Margaret Mwangangi:
"Twalipa bill na taps ziko dry."

Mjadala sasa unaonekana kuhamia kutoka kwa ukosefu wa maji kwenda kwa maswali ya uwajibikaji, huku wananchi wakitaka majibu kuhusu fedha wanazolipa na kwanini huduma imeendelea kuwa ya kusuasua. Je, suluhisho la mgogoro huu ni kuongeza uzalishaji wa maji, au wananchi wanachotaka kwanza ni uwazi na uwajibikaji kutoka kwa wanaosimamia huduma hiyo? 🤔💧

“TOKA JANA SIJAAMINI PENDO WETU, WEWE ULIPIGIA SIMU MARA YA MWISHO IKIWA JANA…” 😭😭 “God knows you better, lala mahali pe...
06/09/2026

“TOKA JANA SIJAAMINI PENDO WETU, WEWE ULIPIGIA SIMU MARA YA MWISHO IKIWA JANA…” 😭😭

“God knows you better, lala mahali pema peponi na unisalimie nduguyo DJ Mashua. Rest in peace Mama Gen Z.” — BEATRICE DAMA KAHINDI

“TOKA JANA SIJAAMINI PENDO WETU…” 😭😭

Mtangazaji wa Kaya FM, Beatrice Dama Kahindi, ameomboleza kwa huzuni na machungu marehemu Mama Pendo, maarufu k**a Mama Gen Z, akimkumbuka k**a mpendwa na rafiki yake aliyekuwa akiwasiliana naye hadi siku chache kabla ya kifo chake.

Je, ni kumbukumbu gani ya Mama Gen Z utakayoendelea kuikumbuka? 🕊️💔

KALOLENI YAGUBIKWA NA MAJONZI 💔🕊️Mama Pendo “Mama Gen Z” Mashua afariki dunia.
06/09/2026

KALOLENI YAGUBIKWA NA MAJONZI 💔🕊️

Mama Pendo “Mama Gen Z” Mashua afariki dunia.

R.I.P MAMA PENDO “MAMA GEN Z” 🕊️💔

Mama Pendo Mashua wa Kaloleni, maarufu k**a Mama Gen Z, amefariki dunia. Alikuwa ndugu wa marehemu DJ Mashua.

Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito. Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu. 🕊️💔

Nyote mnakaribishwa.
06/09/2026

Nyote mnakaribishwa.

“MIMI PIA NAITAKA HIYO SUPPORT!” 🎭🔥«"Nyinyi wasanii wa kwetu Bamba hebu niacheni nipumue mana hiyo support mnayotaka mim...
06/09/2026

“MIMI PIA NAITAKA HIYO SUPPORT!” 🎭🔥
«"Nyinyi wasanii wa kwetu Bamba hebu niacheni nipumue mana hiyo support mnayotaka mimi pia naitaka hivyo hivyo. Nimetoa series, kuna hata mmoja ameenda kuangalia kwanza?"»
— Ruby Kache

🚨 “MIMI PIA NAITAKA HIYO SUPPORT!” RUBY KACHE AWAGEUKIA WASANII WA BAMBA 🔥👀

Muigizaji na muunda maudhui Ruby kache ameonekana kuchoshwa na kile anachodai ni tabia ya baadhi ya wasanii wa Bamba kutaka kuungwa mkono kila wakati bila wao kurudisha mkono kwa wenzao. Kupitia ujumbe wake, Ruby amehoji kwa nini anatarajiwa kusapoti kazi za wengine ilhali kazi zake mwenyewe hazipati ushirikiano sawa kutoka kwa wasanii anaowasaidia.

Kauli hiyo imegusa mjadala mpana unaowakumba wasanii wengi wa maeneo mbalimbali, ambapo kila mmoja anatamani kuungwa mkono lakini wachache ndio wanaoonekana kuwa tayari kusapoti wenzao. Je, tatizo la wasanii wengi ni ukosefu wa support au ni kila mmoja kutaka kusaidiwa zaidi kuliko kusaidia wengine? 🤔🔥

🚨 FATUMA RAMADHAN ATAKA MJADALA WA HESHIMA, VIJANA WAMJIBU KWA MAKOMBORA YA KISIASA 🔥👀Kilichoanza k**a wito wa mjadala w...
06/09/2026

🚨 FATUMA RAMADHAN ATAKA MJADALA WA HESHIMA, VIJANA WAMJIBU KWA MAKOMBORA YA KISIASA 🔥👀

Kilichoanza k**a wito wa mjadala wa staha na heshima kati ya vijana kiligeuka haraka kuwa kikao cha kuwajibishana kisiasa, baada ya Hon. Fatuma Ramadhan kuuliza ikiwa vijana wanaweza kujadili mustakabali wa nchi bila matusi. Badala ya kujadili hoja pekee, baadhi ya wachangiaji walielekeza moto wao kwa misimamo yake ya kisiasa na viongozi anaohusishwa nao.

💥 Daniel Kanyalla:
"Ruto must go... wachana na wakora na cartels wanaouza Wapwani mchana kwa ajili ya matumbo yao."

💥 Kadedw Junior:
"Ubaya hautafuti kiti, unataka kupangwa. Ungebaki huko broadbased wakati ukijua huwezi pewa tikiti?"

💥 Viser Mike:
"Ulidisapoint watu kuingia hii siasa ya vyama..."

💥 Godfrey Mbugua:
"You really started well but you diverged too early... Is there a chance to restructure yourself before elections? Yes you can."

Kadri mjadala ulivyoendelea, ilionekana wazi kuwa baadhi ya vijana hawakuwa wakijibu swali la Fatuma pekee, bali walikuwa wakitoa hukumu yao kuhusu safari yake ya kisiasa na maamuzi aliyofanya hadi sasa. Swali la msingi sasa linaonekana kubaki palepale: je, katika siasa za leo, inawezekana kutenganisha hoja na mtu, au kila mjadala huishia kuwa kura ya imani kwa anayezungumza? 🤔🔥

06/09/2026

Good morning fam.
Wewe huenda kanisa gani, taja kanisa yako leo huenda ukapata churchmate.

Mwili wa mwalimu Enock kupumzishwa nyumbani kwao Tezo kwa Chokwe
05/09/2026

Mwili wa mwalimu Enock kupumzishwa nyumbani kwao Tezo kwa Chokwe

MWALIMU ENOCK KUPUMZISHWA KESHO TEZO 🕊️💔

Hatimaye mazishi ya Mwalimu Enock yatafanyika kesho Jumapili nyumbani kwao Tezo, Kwa Chokwe, mwezi mmoja baada ya kuaga dunia. Enock alikuwa mwalimu wa Garashi Senior School, ambapo jamii ya walimu na wanafunzi watamkosa sana.

Address

Mombasa/Malindi Road
Mombasa
80200

Telephone

+254783868397

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Pwani Trends posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share