Darubini la ushairi-mkuki wa Almasi-malenga Ambrose

Darubini la ushairi-mkuki wa Almasi-malenga Ambrose shughuli-Malenga,mhariri,mwandishi. Uandishi wa vitabu,nakala,habari chipuka, burdani,siasa, michezo

31/01/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Jack Andole, Collo Ogalo, Acquintivillah Yrmah, Laban Muhanji, Sharon Uhuru

Ambia huyu boda maneno matatu.
29/01/2024

Ambia huyu boda maneno matatu.

Anakupea namba Monday, Wednesday gas inaisha, pesa ya nywele inaitishwa.
29/01/2024

Anakupea namba Monday, Wednesday gas inaisha, pesa ya nywele inaitishwa.

Nimetafuta mswaki kumbe Iko Kwa ndevu.. nkt!! Enwei mlisema hii inaitwaje Kwa lugha yenu? BencuteMswaki msafiSHAFFIE ZEL...
14/10/2023

Nimetafuta mswaki kumbe Iko Kwa ndevu.. nkt!! Enwei mlisema hii inaitwaje Kwa lugha yenu? BencuteMswaki msafiSHAFFIE ZELEJoyce Chebet

Happy birthday to me me.🥂 special day ever. Less talk more celebrations.
10/10/2023

Happy birthday to me me.🥂 special day ever. Less talk more celebrations.

30/08/2023

Cole palmer to Chelsea,, deal done

01/08/2023

Pastor anasema , do something that can surprise God. Mimi ni nani!! Nikazima generator. Nimetoka wakisema amen, amen.

POCHI LA BIASHARANasimama kikorongo, mbali Leo nimeonaHili linanikula bongo, pia nyele kunikunaLinaitisha nauli., Kufika...
16/07/2023

POCHI LA BIASHARA
Nasimama kikorongo, mbali Leo nimeona
Hili linanikula bongo, pia nyele kunikuna
Linaitisha nauli., Kufika hapo Kwa duka
'li pochi la BIASHARA, linameza mishara

Pochi hili ndilo kitu, fungua macho uone
Linameza kila kitu, kileleni muachane
Pochi halijui utu, murife usikazane
'li pochi la BIASHARA, linameza mishahara.

Hili pochi lapendeza, ila hatarii kumeza
Lajua kubembeleza, hata pia kupumbaza
Mfuko ukilegeza, mkono linapenyeza
'li pochi la BIASHARA, linameza mishahara

Mafuta yake ni ghali, wewe ndiye mnunuzi
Matembezi mbalimbali, hata kupiga na mbizi
Mshahara wafadhili, baba huezi maizi
'li pochi la BIASHARA , linameza mishahara

Nguo mpya za fesheni, hili pochi linapenda,
Mkitinga madukani, eti bebi nakupenda
Ila ndani akilini, ni mishara lapenda
'li pochi la BIASHARA, linameza mishahara

Zile simu kalikali, pochi hili linataka
Mkiwa kwenye shughuli, kila kitu linadaka
Linaitisha nauli kufika hapo kwa duka
'li pochi la BIASHARA, linameza mishahara

Ni kupe halibanduki, linalo mengi majina
Laitwa saidi chili, Hilo ndilo moja jina
Halizui hata chuki, Kwa mkeo wala Wana
'li POCHI LA BIASHARA , linameza mishahara
Nafunga wangu waraka wasije kunivamia,
Naenda zangu dandora, kwangu nakimbilia
Mapochi Leo tofika, moto mewaashia
'li pochi la BIASHARA, linameza mishahara.

Mwandishi
Malenga Ambrose

Mhariri
Ambrose

NIPE HATA DADAKOHujambo uko uliko, barua nakuandikiaKusema huku niliko, vibaya naumiaNilidhani Mimi wako, nimeishi fikir...
16/07/2023

NIPE HATA DADAKO
Hujambo uko uliko, barua nakuandikia
Kusema huku niliko, vibaya naumia
Nilidhani Mimi wako, nimeishi fikiria
Kumbe nawe una wako, vyetu vyako twatumia?

K**a singekuwa wako, laiti ningalijua
Ningetafuta mamako, yote haya kumwambia
Nitafte na babako, nimnyweshe mbili bia
Nimwambie huyo wako, mahari hatochukuwa

K**a singekuwa wako, hivi nisingeumia
Ona ninavuta Kiko, nawaza nakuwazuwa
Moyo una babaiko, ndani Kwa ndani nalia
Najifanya Mimi wako, na wako unamjua

Nishajua kwako siko, mwengine natafutia
Hata k**a ni DADAKO, hakika namchukuwa
Zaidi wa sura yako, Alo umbo Kako pia
Niache masikitiko, moyo upate tulia.

Mwandishi
Malenga ambrose

Mhariri
Ambrose.

Ipo siku. Langu jicho
24/02/2023

Ipo siku. Langu jicho

Jua uendako,,Jua uendako.
24/02/2023

Jua uendako,,Jua uendako.

MAISHA KWISHAKiserema nakitia,begani kuchumiaMkwasi kaniitia,kibarua kulimiaShati langu lovalia,sijachoka kutumiaNdilo l...
23/06/2022

MAISHA KWISHA
Kiserema nakitia,begani kuchumia
Mkwasi kaniitia,kibarua kulimia
Shati langu lovalia,sijachoka kutumia
Ndilo la kwangu pazia,hata k**a ni la mia
Mola wangu shikilia,nisije kuangamia

*Afajiri naingia,mkundani kulimia
Nani kunihurumia,kiporo kunigawia
Sina kulifanyia,moyo mie najitia
Alasiri tawadia,kunilipa mbili mia
Mola wangu shikilia,nisije
kuangamia

Maishangu shikilia,mana mola
nalilia
Kwani unga mepandia,kilo
mbili,mbili mia
Siasa moto pambia,mie hapa
angamia
Mali mengi tafutia,Kwa mafuta
pandishia
Mola wangu shikilia,nisije
kuangamia

Milangoni fungulia,mwanga wako
mulikia
Walo nacho saidia,lala hoi tunafia
Kura zetu mwatumia,serikali kuingia
Ya kwangu kuwapigia,sidhubutu
natupilia
Mola wangu shikilia,nisije
kuangamia

Virago napachikia, ukutani natulia
Mana njaha najutia,tonge sina
kulitia
Kinywani nakaukia,mola kwako
nakujia
Hapa hapana tulia,huku mie najutia

Malenga,

Ambrose.

Address

Shinyalu
Kakamega
NONE

Telephone

+254794232801

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Darubini la ushairi-mkuki wa Almasi-malenga Ambrose posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Darubini la ushairi-mkuki wa Almasi-malenga Ambrose:

Share

Category