Legal Consultancy and social advises

Legal Consultancy  and social advises Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Legal Consultancy and social advises, Dar es Salaam.

04/07/2023
Vitabu hivi vinaelezea makosa mengi yanayofanywa na Waajiri mahali pa kazi ambayo ni kinyume na Sheria za kazi, Mambo ya...
04/07/2023

Vitabu hivi vinaelezea makosa mengi yanayofanywa na Waajiri mahali pa kazi ambayo ni kinyume na Sheria za kazi, Mambo ya kuzingatia na kufuata wakati unamuajiri mtu , na njia sahihi ya kuvunja mkataba wa kazi au kumuondoa mtu kazini bila kuvunja sheria, hivyo vina msaada kwako unaependa kuwa na uelewa mkubwa juu ya sheria za kazi. WhatsApp 0682734998 kwa maelezo zaidi.

19/05/2023

APPEAL FROM THE HIGH COURT TO COURT OF APPEAL OF TANZANIA.
● Kwa kawaida mtu anapotaka kukata rufaa kutoka Mahaka Kuu kwenda Mahak**a ya Rufaa basi sheria inamtaka mtu huyo kupeleka maombi ya kukata Rufaa ( Application for leave to Appeal to the Court of Appeal)kule Mahaka kuu ili iweze kutambua k**a sababu zake za kukata rufaa ni za kisheria( point of law) au si za kisheria( matters of fact)na k**a ni za kisheria basi mtu huyo ataruhusiwa kukata Rufaa . Section 5(1)c & s.7 (a) and (b)of The Appellate Jurisdiction Act, [Cap.141 R.E 2019] and Rule 44(1)a & b and Rule 45(a)of The Court of Appeal Rules,2009.

✍📌Lakini leo nakukumbusha kuwa kuna utofauti unapotaka kukata Rufaa kwenye mashauri ya kazi ( labour matters). Kwa Mujibu wa kifungu cha 57 cha Sheria ya Taasisi za kazi ( Labour Institution Act) sura ya 300 marejeo ya mwaka 2019, Rufani kutoka Mahak**a kuu divisheni ya Kazi itapelekwa moja kwa moja Mahak**a ya Rufaa bila kuomba kibali mahaka kuu ( without application for leave to Appeal) tofauti na ilivyo kwnye mashauri mengine, ila ufanano uliopo ni kuwa Rufaa lazima pia iwe ni kwenye sababu za kisheria tu (point of law only)

Mashauri ya Jinai katika Mahak**a ya Mwanzo ( The Primary Court)✍Mamlaka ya Mahak**a ya mwanzo katika kusikiliza mashaur...
04/09/2021

Mashauri ya Jinai katika Mahak**a ya Mwanzo ( The Primary Court)

✍Mamlaka ya Mahak**a ya mwanzo katika kusikiliza mashauri ya jinai.

Mahak**a ya mwanzo ina mamlaka wa kusikiliza na kuamua baadhi ya mashauri ya jinai yanayotokana na makosa yaliyobainishwa kwenye jedwali la kwanza la Sheria za Mahak**a za Mahakimu, Sura Na.11 ya mwaka 2019( The first schedule to The Magistrates' Courts Act, [Cap. 11 R.E 2019]
Hata hivyo Mahak**a ya mwanzo haina mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayotokana na makosa ya kubaka, unyang’anyi wa kutumia nguvu, mauaji, uhujumu uchumi, rushwa , kugushi , uhaini na mengine mengi.

✍👨‍⚖ ADHABU INAYOWEZA KUTOLEWA NA MAHAKAMA YA MWANZO ( The Primary Court) KATIKA KESI YA JINAI
mahak**a hiyo inao uwezo wa kutoa adhabu zilizoidhinishwa na sheria kwa kiwango kilichoidhinishwa na sheria kwa mujibu wa jedwali la tatu la Sheria za Mahak**a za Mahakimu. KWA MUJIBU WA Jedwali la tatu la Sheria za Mahak**a za mahakimu sura Na.11 ya mwaka 2019 sehemu ya II kipengele cha 2(1)a,b,na c (The third schedule to The Magistrates' Courts Act,[Cap.11 R.E 2019] part II item 2 (1)a,b & c )mahak**a ya Mwanzo inayomamlaka ya kutoa adhabu zifuatazo:_
●kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili12
●faini isiyozidi laki tano 500,000/=
●Adhabu ya Viboko visivyozidi kumi na mbili 12

Je, Wajuwa ya kuwa pale Masharti ya Mkataba( contract)au ya Mgawanyo wa mali(disposition of Property)au kitu chochote ki...
04/09/2021

Je, Wajuwa ya kuwa pale Masharti ya Mkataba( contract)au ya Mgawanyo wa mali(disposition of Property)au kitu chochote kinachotakiwa na sheria kuwa kwenye Maandishi, Ushahidi wowote wa kuthibitisha masharti hayo ni lazima uwe wa maandishi na sio wa mdomo, hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 100(1)& 101 cha Sheria ya Ushahidi, Sura Na.6 ya Mwaka 2019 .

LIMITATION OF TIME FOR SUIT TO RECOVER LAND.Leo ningependa ufahamu ukomo wa muda katika kufungua shauri la kudai umiliki...
03/09/2021

LIMITATION OF TIME FOR SUIT TO RECOVER LAND.
Leo ningependa ufahamu ukomo wa muda katika kufungua shauri la kudai umiliki wa ardhi (Land possession)
✍ Kwa mujibu wa Sehemu ya kwanza ( Part I) ya NYONGEZA ya Sheria ya Kiwango cha Juu, Sura 89 marejeo ya mwaka 2019( Part I of the Schedule to The Law of Limitation Act,[Cap.89 R.E 2019], shauri la kudai umiliki wa ardhi linapaswa kufunguliwa ndani ya miaka 12, na baada ya muda huo mtu aliyejimilikisha ardhi kwa zaidi ya miaka 12 bila kubughuziwa na mtu yeyote ,basi anajipatia umiliki halalali wa ardhi hiyo.(Adverse possession )

👨‍⚖ kwa Mujibu wa kifungu cha 62 cha SHERIA YA NDOA SURA NO.29 Marejeo ya mwaka 2019,mwanaume/mwanamke hawajibiki kwa ma...
12/04/2021

👨‍⚖ kwa Mujibu wa kifungu cha 62 cha SHERIA YA NDOA SURA NO.29 Marejeo ya mwaka 2019,mwanaume/mwanamke hawajibiki kwa madeni ya mwenza wake aliyokuwa nayo kabla ya Ndoa.

12/04/2021

🇹🇿👨‍⚖👨‍⚖ Je, wajua ya kuwa ni kosa Kisheria kwa mwanaume au mwanamke👫 kumpiga mwenzi wake,bila kujali tamaduni za kabila fulani, hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 66 cha SHERIA YA NDOA,SURA No.29 Marejeo ya mwaka 2019.📌

24/05/2020

On this happy occasion of Eid-ul-Fitr, I pray to Allah to fulfil all your dreams. Eid Mubarak!"🌙

22/05/2020

of persons arrested #
je, unafahamu ni mda gani mtuhumiwa anatakiwa kufikishwa mahak**ani baada ya kuk**atwa na polisi????
kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai sura namba 20 k**a ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019 yaani # The Criminal Procedure Act, [Cap.20 R.E 2019] kifungu cha 32 ni jukumu la Afisa wa polisi kumfikisha mtuhumiwa katika mahak**a yenye uwezo wa kusikiliza shauri lake ndani ya saa 24.Kama mtuhumiwa hatapewa haki ya kupelekwa mahakami ndani ya mda tajwa bila sababu ya msingi basi wanayo haki ya kwenda mahakami kuomba kitu hicho ( Habeas Corpus) section 390 of Cap.20

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255682734998

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Legal Consultancy and social advises posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share