Faculty of Law-Mzumbe University

Faculty of Law-Mzumbe University Law is general

Maisha ya Vyuoni huwa yanakupatia sio tu elimu ya darasani bali vile vile yanakukutanisha na elimu flani ya maisha. Ukia...
12/01/2023

Maisha ya Vyuoni huwa yanakupatia sio tu elimu ya darasani bali vile vile yanakukutanisha na elimu flani ya maisha. Ukiacha hatua k**a hiyo aliyochukua huyo kijana kwa mujibu wa Mwananchi, kuna wanachuo hufeli masomo yao kutokana na kuachwa/kuachika katika mahusiano ya kimapenzi. Mtu anampenda mwenzake kuliko anavyojipenda mwenyewe (anaenda beyond "Neighbourhood Principle"). Ukijipenda mwenyewe, hautakubali nafsi yako ipoteze malengo ya kile ulichokifuata Chuo kwa sababu ya mtu mwingine. Bahati mbaya unakuta mwingine anakuja kujifunzia mapenzi chuoni anakutana na mtu ambaye ameshagraduate kwenye masuala hayo akiwa secondari. Ukik**atwa kwenye mahusiano ya aina hiyo ndo ukiachwa unaona k**a dunia nzima aliyekuwepo ni huyo tu aliyekuacha. Na hapo sasa ndo inafikia mtu hataki kusoma, anatumia ada aliyopewa na wazazi wake kumuhudumia mtoto wa mtu, anawekw off campus k**a mpishi wa mwenzake anayeingia darasani, matokeo yake ukiachwa ni Discontinuation, kupata wendawazimu na hata kujinyonga. Maisha ya Chuoni ni lazima uyaendee kwa umakini ili kuweza kutimiza malengo yako, kuishi na wakubwa wenzio sio kazi ndogo. Ukitoka Chuoni, hutoki na degree tu, unatoka na experience nyingine za maisha. Katika jambo hili, TUPENDE KWA UMAKINI NA KIASI NA NAFSI YAKO NI BORA ZAIDI KULIKO MAPENZI.

Pale unapokutana na classmate wako wa enzi za primary😁😁😁😁😁
10/01/2023

Pale unapokutana na classmate wako wa enzi za primary😁😁😁😁😁

Utasikia Sir, kazi anayo Koku ndo yuko mikese anatokea Dar kwa masuala mbalimbali ya kiutumishi. Sir; "hata angekuwepo h...
10/01/2023

Utasikia Sir, kazi anayo Koku ndo yuko mikese anatokea Dar kwa masuala mbalimbali ya kiutumishi. Sir; "hata angekuwepo hapa, hakuna mtu angesoma, mtapresent kwa maswali ya papo kwa hapo kulingana na requirement ya swali, sogea mbele twende kazini, unatakiwa uwe tayari maana hujui siku wala saa mwana wa adamu atakuja"😁😁😁😁😁😁😁

Kuna vijana wengi tuliowahi kukutana darasani wameitwa kuanza kazi katika vituo mbalimbali vya utumishi wa umma. Wengine...
10/01/2023

Kuna vijana wengi tuliowahi kukutana darasani wameitwa kuanza kazi katika vituo mbalimbali vya utumishi wa umma. Wengine baada ya subira ya muda mrefu sana. All the best wote mlioitwa katika utumishi wa umma. Vijana wengi wameingia katika ajira za serikali katika mwaka huu wa fedha. Kwa wale wanaofanya application, ni vyema mtu ukiwa unaendelea kufuatilia bila kuchoka taarifa za ajira uliyoiomba iwe katika sekta ya umma au binafsi. Usisubiri kupigiwa simu katika ulimwengu huu ambao ushindani wa ajira ni mkubwa sana.

Simu yako ikijaa, save kwenye ubongo. Katika safari ya maisha, sometimes anayekuja kukusaidia mlimani, ni mtu ambaye ush...
06/01/2023

Simu yako ikijaa, save kwenye ubongo. Katika safari ya maisha, sometimes anayekuja kukusaidia mlimani, ni mtu ambaye ushamsahau katika maisha yako.

Safari ya kuumaliza mwaka 2022 inamalizika leo. Kuna mengi yametokea katika mwaka huu na bila shaka kuna jema ambalo wew...
31/12/2022

Safari ya kuumaliza mwaka 2022 inamalizika leo. Kuna mengi yametokea katika mwaka huu na bila shaka kuna jema ambalo wewe mpenzi msomaji unaweza kumshukuru Mungu kwa safari hii ndefu ya miezi 12 na kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kutuvusha sote salama kuelekea 2023. Inawezekana mafanikio yakawa madogo katika assessment yako binafsi, lakini mshukuru Mungu japo kwa pumzi ya Uhai. HERI YA MWAKA MPYA KWENU Nyote na Mungu aendelee kutupatia nguvu ya kuendelea kutumikia Taifa na jamii inayotuzunguka katika mwaka 2023. KAZI IENDELEEπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

Tarehe 16 December, 2022, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maend...
22/12/2022

Tarehe 16 December, 2022, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe alifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe. Alitembelea Kituo cha Upanga na Tegeta na kuongea na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam.

Thank you my good people, Faculty of Law, may God bless you all. It was wonderful to work with you for all these 16 yrs ...
19/12/2022

Thank you my good people, Faculty of Law, may God bless you all. It was wonderful to work with you for all these 16 yrs as comrades. Nitawamiss ingawa tutakuwa pamoja katika Utumishi wa watu. KAZI IENDELEEπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

Kila siku unapokuwa umekamilisha jukumu flani ulilopangiwa au ulilojipangia kwa siku hiyo, ni vyema ukamshukuru Mungu kw...
15/12/2022

Kila siku unapokuwa umekamilisha jukumu flani ulilopangiwa au ulilojipangia kwa siku hiyo, ni vyema ukamshukuru Mungu kwa yote ambayo amekujalia na kumshukuru pia kwa fursa ya watu mbalimbali anaokukutanisha nao. Asikwambie mtu, watu unaokutana nao, unaoishi nao, unaosoma nao, unaofanya nao kazi, watu wale wanaokufahamu mienendo yako, wanaojua ubinadamu wako katika uimara na upungufu wako, wanayo nafasi kubwa sana ya kukusemea jema na wakati mwingine kukunenea hata baya ambalo linaweza kukuinua au kukushusha katika maisha. Kikubwa ishi na watu vizuri ila kumbuka pia, katika ubinadamu wako, hutaweza kumfurahisha kila mmoja kwani hiyo ndo mojawapo ya mambo yanayodefine ubinadamu wetu. KAZI IENDELEEπŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

Alifungua njia Dr. Modesta Opiyo (our former Dean, Faculty of Law), akafuata Dr. Ubena John (also our former Dean, Facul...
06/08/2022

Alifungua njia Dr. Modesta Opiyo (our former Dean, Faculty of Law), akafuata Dr. Ubena John (also our former Dean, Faculty of Law) na sasa, na 18 kwenye orodha ya wateule, Dr. Mwajuma Kadilu (our current Lecturer and Head of Department, Civil and Criminal Law, Faculty of Law). Hongera sana kwa uteuzi wake Dr. Kadilu. Kwa wale tuliofanya kazi naye, naamini na hata wanafunzi wake aliowahi kufundisha, they can appreciate uteuzi huu na kwamba she deserve to be at that level in legal profession. We wish her all the best katika utendaji mzuri wa majukumu yake haya mapya. Kiukweli tutammiss Madam Kadilu, she was a very hardworking Lecturer and Colleague in the Faculty of Law, Mzumbe University. Mwenyezi Mungu amemuinua akawasaidie watanzania wengi zaidi kwenye utoaji hakiπŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘

Chuo Kikuu Mzumbe, kupitia kwa Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, leo kimekuwa mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Umma...
19/06/2022

Chuo Kikuu Mzumbe, kupitia kwa Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, leo kimekuwa mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Umma vilivyosaini Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ambao umelenga kuleta mageuzi makubwa katika miundombinu ya Vyuo ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Pongezi kubwa kwa Serikali ya JMT kwa kuwezesha kupatikana kwa mkopo huu utakaoleta mapinduzi makubwa katika miundombinu ya Chuo Chetu. Pichani, Vc wa Chuo akisaini mkataba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dr. Francis Michael, wakishuhudiwa na Mwanasheria wa Wizara na Kaimu Mshauri wa Sheria wa Chuo Kikuu Mzumbe, Wakili Innocent Mgeta. KAZI IENDELEE🀝🀝🀝🀝🀝🀝

Wastue wenzako. Wale wanaohitaji kutransfer pia karibuni Sana Chuo Kikuu Mzumbe
01/11/2021

Wastue wenzako. Wale wanaohitaji kutransfer pia karibuni Sana Chuo Kikuu Mzumbe

Address

P. O. BOX 9
Mzumbe

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Faculty of Law-Mzumbe University posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Faculty of Law-Mzumbe University:

Share