NURU YA Matumaini

NURU YA Matumaini MWANGA UNAOMULIKIA MAISHA YAJAYO

15/11/2025

🍞 MKATE WA LEO KUTOKA KWA WACHUNGAJI: || ..............................
Yoshua 20:1-9.
Miji ya Kimbilio na Kimbilio la Neema.

❓ Je, unajua kwamba Mungu amekutayarishia mahali pa kukimbilia kwa ajili ya usalama wako pale unapotenda makosa?

πŸͺ” UTANGULIZI NA MUKTADHA:

Mungu alikuwa amemwagiza Musa aweke miji mitatu upande wa mashariki na mitatu upande wa magharibi wa Mto wa Yordani kuwa ni miji ya makimbilio. Yoshua 20 inaonyesha utekelezaji wa maagizo haya. Miji ya makimbilio ambayo ilikuwa inakaliwa na Walawi, ilikuwa ni mahali palipowekwa kwa ajili ya wale waliokuwa na tuhuma za mauaji (Kutoka 21:12-13, Hesabu 35:9-34, Kumbukumbu 4:41-43, 19:1-13). Ndugu wa karibu wa marehemu alikuwa ana wajibu wa kulipiza kisasi kwa kumuua mkosaji. Mungu anamwagiza Yoshua kuchagua miji ya kimbilio ambamo mtu aliyemuua mwenzake bila kukusudia anaweza kukimbilia ili apate usalama mpaka mahak**a iamue. Na lango la mji lilikuwa linahusisha mahali ambapo palikuwa panaamua nani aruhusiwe kuingia na kutoka na kuweka ulinzi wa mji. Na pia Ζ™ulikuwa na jengo lenye vyumba kadhaa ambapo wazee wa mji walipatumia k**a mahak**a na hata walipatumia kwa ajili ya biashara (Ruthu 4:1). Miji mitatu iko magharibi ya Yordani (Kedeshi, Shekemu na Hebroni) na mitatu iko mashariki (Bezeri, Ramothi na Golani). Mtu aliyesababisha kifo bila nia au bila kukusudia, alipaswa akimbilie mji huo, asimame kwenye lango na kueleza kesi yake. Atapokelewa na kuishi humo hadi kuhani mkuu afe; ndipo anaweza kurudi nyumbani bila kuadhibiwa. Miji hii inapatikana kwa wote, ikiwa ni pamoja na wageni. Hii inaonyesha haki na rehema katika utawala wa Mungu kwa watu wa mataifa yote.

πŸ“– Soma Kwanza: Yoshua 20
Soma maagizo kuhusu miji ya makimbilio na jina la kila mji. Tafakari jinsi sheria hii inavyoonyesha haki, ulinzi na rehema na kupunguza umwagikaji wa damu au vifo vya kiholela na kuonyesha heshima kwa maisha ya mtu.

πŸ“š MUUNDO WA MADA NA UCHAMBUZI WAKE:

πŸͺ’1. Agizo la Kuchagua Miji – Mst. 1–3 – Mungu anamwelekeza Yoshua ateue miji; watu wanaokimbilia huko wanapewa usalama mpaka kesi yao isikilizwe.

πŸͺ’2. Maagizo ya Utaratibu – Mst. 4–6 – Mwuaji wa bahati mbaya anatakiwa kuelezea kesi yake kwanza kwa wazee na baadaye kwa mkutano; anapewa ulinzi kwa kuhifadhiwa katika mahali palipoandaliwa hadi hukumu itakapotolewa. Ikithibitika aliua kwa makusudi anakabidhiwa kwa mlipiza kisasi ili apewe adhabu ya kifo kupitia ndugu wa karibu wa marehemu (Kumbukumbu 19:12). Na kwa yule ambaye aliua kwa bahati mbaya alitakiwa kubaki katika mji huu wa makimbilio hadi Kuhani Mkuu atakapokufa. Kifo cha kuhani mkuu kilikuwa kinaleta upatanisho, kwa sababu alipewa jukumu la kubeba hatia ya dhambi za watu (Kutoka 28:38 na Mambo ya Walawi 10:17). Hili jukumu la kifo cha makuhani wa agano la kale kubeba hatia za wenye dhambi liikuwa linaashiria jukumu la kafara ya Kuhani wa agano jipya Yesu Kristo kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu (1Petro 2:24 na Waebrania 9:11-15).

πŸͺ’3. Orodha ya Miji – Mst. 7–9 – Miji mitatu magharibi (Kedeshi, Shekemu, Kiriath‑Arba/Hebron) na miji mitatu mashariki (Bezeri, Ramothi na Golani) inatajwa; sheria hii inatumika kwa waisraeli na wageni. Miji hii ya makimbilio pia ilikuwa miji ya Makuhani (Yoshua 21;13-38).

πŸͺ” MUHTASARI WA MADA:

🌴1. Miji ya makimbilio ni ishara ya rehema ya Mungu: inatoa nafasi ya usalama na haki kwa wauaji wasio na nia mbaya.

🌴2. Hii inaonyesha kwamba Mungu anatofautisha kati ya kosa la kukusudia na la bahati mbaya.

🌴3. Pia inaonyesha jinsi Yesu alivyokuwa kimbilio letu – tunapomkimbilia tunapata msamaha na ulinzi dhidi ya adui.

🌴4. Sheria hii pia inatukumbusha kuanzisha mifumo ya haki katika jamii zetu na kuwatazama kwa huruma wale waliokosea bila kukusudia.

πŸ‘₯ *MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 20:1-9*

βœ…1. Nia ya Mungu kuweka miji ya makimbilio ni kuepusha umwagaji damu usio na hatia na kutaka mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya kubaini makosa badala ya kila mmoja kujiamulia aonavyo. Unaona hali ya kuheshimu vyombo vya kutoa haki k**a mahak**a kwenye jamii unayoishi au kila mtu anajichukulia sheria mkononi? Je ni halali kumwadhibu mtu kwa kumdhania kuwa alikuwa anakusudia kutenda kosa?

βœ…2. Miji ya makimbilio ilimwakilisha Yesu aliye kimbilio la wenye dhambi. Je mtu aliyetenda dhambi ya kukusudia anaweza kusamehewa na Yesu? (Isaya 1:18). Miji ya makimbilio leo ni kituo cha polisi. Je unajisikia salama zaidi ukiwa mikononi mwa polisi? Baraza la Kanisa lina mamlaka ya kumsamehe mkosaji wakigundua alifanya kosa pasipo kukusudia?

βœ…3. Je amani huzalisha haki au haki ndiyo inayozalisha amani? Mahak**a zipo kwa ajili ya kudumisha amani au zipo kwa ajili ya kuwagombanisha watu? Je mtu aliyenyimwa haki anaweza kuwa na amani? Je kuna uwezekano mdhulumaji akamuona anayedai haki k**a anachochea vurugu na ukosefu wa amani?

βœ…4. Je, jamii yako ina mifumo gani ya haki na rehema kwa watu wanaokosea bila nia mbaya? Je wewe binafsi una utaratibu wenye huruma wa kuwatendea wale wanaokukosea kwa bahati mbaya?

βœ…5. Unajifunza nini kuhusu kumkimbilia Yesu k**a kimbilio lako wakati unapokosea? Je kuna uwezekano wa kufanya dhambi ambayo hukukusudia? Dhambi ambayo mtu anatenda wakati hajakusudiwa inahesabiwa kuwa ni dhambi? (Warumi 7:20).

πŸ” MASWALI YA TAFAKARI:

🍞1. Je unahitaji kujua kwamba unaweza kukimbilia wapi unapofanya makosa?

🍞2. Je, sheria hii inakutia changamoto kuanzisha mahali pa usalama na msamaha katika familia au jumuiya yako?

🧱 MATUMIZI MAISHANI:

Waza njia za kuonyesha rehema kwa mtu aliyekukosea bila kukusudia. Toa kimbilio la maneno na matendo, ukikumbuka kwamba nawe unapokosea unahitaji rehema kutoka kwa Mungu kila siku. Msamehe mwenzi wa maisha, mtoto wako au mtu mwingine. Uwe tayari kumsamehe deni mtu anayeonekana kushindwa kulipa.

_Andiko la Kutia Moyo_

Naye atakaa katika mji huo, hadi hapo atakaposimama mbele ya mkutano kuhukumiwa, hadi kifo chake kuhani Mkuu mwenye kuwapo katika siku hizo; ndipo yule mwuaji atarudi , na kuuendea mji wake mwenyewe, hadi mji huo alioutoka hapo alipokimbia (Yoshua 20:6).
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. (Zaburi 46:1).

_Neno la Baraka - Benediction_

Bwana akufungulie madirisha ya mbinguni na akumwagie baraka tele hata isiwepo nafasi ya kutosha na kikombe chako kijae kisukwe sukwe hata kumwagika. Bwana akuponye magonjwa yako, akupatie nguvu na afya njema na akuongezee siku za kuishi kwa furaha hapa duniani. Bwana aondoe dhoruba na akupatia upendo wa kweli katika ndoa yako na akujalie kuishi na amani na watu wote. Bwana abariki mashamba yako, biashara yako na kazi yoyote ya halali unayoifanya kwa bidii, ubunifu na bila kukata tamaa. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nawe sasa na hata milele.

_Tamko la Imani_

Hizi baraka ambazo zinatoka katika Neno la Mungu, ninazipokea kwa Imani na ninatanguliza shukrani kwa wema wa Bwana katika maisha yangu. Ninaamini hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele (Zaburi 23:6).

πŸ”‘ SALA YA MWISHO:

Mungu mwenye rehema nyingi, hakika wema wako na fadhili zako ni kuu sana na unastahili kuabudiwa. Nisaidie kujua kuwa usalama wangu unapatikana kwa kukimbilia kwa Jina la Yesu ambalo ni ngome imara na kila anayelikimbilia anakuwa salama. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu niwezeshe kutambua kuwa wokovu wangu unapatikana kupitia kwa kifo cha msalabani cha Kuhani Mkuu Yesu Kristo na niwezeshe kumchagua Yeye kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Kwa sababu nimeutafuta ufalme wa mbinguni kwanza na haki yake, ninaomba unizidishie na mahitaji yangu mengine ya kimwili sawasawa na ahadi zako na wingi wa utajiri wako. Ninaomba kwa Imani kupitia kwa jina la Yesu, Amina.

πŸ‘€πŸ‘€πŸ‘€ Watayarishaji wa Mwongozo huu wa Biblia: Pr. Stephen Letta, Pr. Lusekelo Mwakalindile, na Pr. Enos Mwakalindile, Dar es Salaam, Tanzania.

➑️ Jiandae kwa Somo la Kesho: Sura ya 21 – Miji ya Walawi na Hakuna Ahadi iliyoanguka.

12/11/2025

🍞 MKATE WA LEO KUTOKA KWA WACHUNGAJI: || ............................
Yoshua 19:1-51.
Urithi wa Makabila Yaliyobaki na Zawadi kwa Yoshua.

❓ Je, unaona thamani ya kugawana baraka zako na kuwapa wengine nafasi ya kwanza kabla ya kujitunza mwenyewe?

πŸͺ” UTANGULIZI NA MUKTADHA:

Sura hii inaendelea na ugawaji wa ardhi kwa makabila yaliyobaki: Simeoni, Isakari, Asheri, Naftali na Dani. Kila kabaila linapewa sehemu ya ardhi kulingana na kura. Simeoni anapata sehemu ndani ya Yuda kwa sababu urithi wa Yuda ulikuwa mkubwa; Dani anapigania eneo lake kutokana na shinikizo la Wafilisti na baadaye anachukua mji kwa Jina la Leshemu (baadaye unaitwa Dani, Jina la babu yao). Mwishoni mwa sura, watu wa Israeli wanampa Yoshua mji wa Timnath‑Serahu katika nchi ya Efraimu k**a zawadi yake kwa huduma aliyoitoa. Yoshua anaujenga mji huo na kuishi humo.

πŸ“– Soma Kwanza: Yoshua 19

Soma habari ya ugawaji wa ardhi kwa makabila yaliyosalia na zawadi kwa Yoshua. Tafakari umuhimu wa kushiriki baraka na mtu kuthamini huduma yake kwa jamii.

πŸ“š MUUNDO WA MADA NA UCHAMBUZI WAKE:

πŸͺ’1. Urithi wa Simeoni – Mst. 1–9 – Simeoni anapokea ardhi ndani ya Yuda kwa kuwa urithi wa Yuda ulikuwa mkubwa sana; hii inaonyesha kushirikiana katika baraka.

πŸͺ’2. Urithi wa Isakari, Asheri, Naftali na Dani – Mst. 10–48 – Maelezo ya mipaka na miji ya kila kabila. Dani anashindwa kuwathibiti wenyeji wa eneo la kusini magharibi mwa Benjamini (fungu la 41-46) na baada ya kunyang'anywa sehemu ya urithi wake na Waamori ( Waamuzi 1:34-35;18:1) au Wafilisti (Waamuzi 13-16) na wanaamua wao wenyewe kujiongezea eneo kwa kuenda kaskazini katika eneo linaloitwa Leshemu na hapa wanafanikiwa kuwapiga wakazi wake na kulimiliki (Waamuzi 18:27).

πŸͺ’3. Zawadi kwa Yoshua – Mst. 49–51 – Yoshua anakuwa wa mwisho kupokea sehemu ya urithi wake baada ya makabila yote anayoyaongoza kupata. Huu ni mfano mzuri wa kiongozi mwenye roho ya utumishi, unyenyekevu na kuwatanguliza wengine kwanza. Na Bwana alimuahidi kwamba atapewa eneo atakalolichagua. Lakini bado hachagui eneo kubwa na maarufu badala yake anachagua eneo dogo pembezoni mwa mji katika milima ya Efraimu. Eneo alilopewa lilikuwa linaitwa Timnath-Serah ambalo lina maana ya 'sehemu ambayo imebaki.'

πŸͺ” MUHTASARI WA MADA:

🌴1. Sura hii inaonyesha upendo na ukarimu katika makundi mbalimbali ya jamii, kwa jinsi ambavyo Yuda alikuwa tayari kushiriki ardhi yake na Simeoni. Hata hivyo inaonekana Waisreali hawakuwa na juhudi kubwa kupigana na kumiliki ardhi yote ambayo Mungu aliwaahidia na hivyo kusababisha kugawana ile ndogo iliyokuwepo. Hii inatufundisha kwamba Mungu ametuahidi baraka nyingi ila tutapokea kulingana na imani na juhudi zetu. (Mwanzo 15:18 na Kumbukumbu 11:24).

🌴2. Kila kabila linagawiwa miji na vijiji. Bwana ameahidi kuwabariki Wana wa Israeli mijini na vijijini au mashambani. Hata Bwana wetu Yesu aliwahubiria watu walioko mijini na vijijini (Yoshua 19:7-8, Kumbukumbu 28:3, Mathayo 9:35).

🌴4. Maandiko Matakatifu yanaonyesha eneo la kila kabila na mipaka yake. Hapa tunajifunza umuhimu wa kila mtu binafsi na ama kikundi cha watu k**a vile Kanisa kujua mipaka ya eneo ambalo wamepewa kulimiliki na kulifanyia utume.

🌴3. Mwisho wa sura, tunamwona Yoshua akipokea urithi wake baada ya kuwahudumia wengine kwanza. Hii inatufundisha kwamba viongozi wa kweli wanatanguliza mahitaji ya wengine kabla ya mahitaji yao na wanapokea baada ya kuwahudumia wengine. Hapa tunaona Roho ya ushindi dhidi ya roho ya ubinafsi.

🌴4. Hapo nyuma tumekuwa tukiona kundi la watu katika kabila ndio wanaopewa ardhi. Lakini hapa tunaona mtu binafsi akigawiwa urithi wake. Hii inatufundisha kwa kiwango fulani kiongozi anaweza kupewa nyongeza fulani ya baraka tofauti na watu anaowaongoza kwa sababu majukumu yake pia ni makubwa zaidi ya watu wa kawaida. Paulo anasema, " Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kutoa unabii na kufundisha. (1 Timotheo 5:17).

🌴5. Ugawaji wa ardhi unatukumbusha pia kwamba Mungu ana sehemu maalum na mahsusi kwa kila mmoja wetu.

🌴6. Baada ya kushindwa kumiliki sehemu waliyopewa kutokana na nguvu za wenyeji, kabila la Dani linaamua kutafuta mji mwingine na kuuangamiza na kuumiliki. Kitabu cha Mithali kinasema kwamba mwenye haki anaweza kuanguka mara saba na akainuka tena. Hii ikitokea tumeshindwa kufanya jambo fulani tusikate tamaa, badala yake tufanye jambo lingine tofauti. Kwa mfano unaposhindwa katika biashara ya bidhaa fulani kwa muda fulani unaweza kubadilisha bidhaa nyingine.

πŸ‘₯ *MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 19:1-51*

βœ…1. Kwa nini Yuda hawakuhitaji eneo kubwa la urithi hata ikabidi sehemu ya urithi wao wapewe Simeoni? Inakufundisha nini kutoka na ukweli kwamba Joshua alijiweka wa mwisho kupokea urithi na umiliki wa nchi.

βœ…2. Unadhani viongozi wa nchi za Afrika wanamudu kufanya hivyo. Viongozi wachache waliomudu kujisahau na kutanguliza raia wao walifanikiwaje na wengine wameshindwaje?

βœ…3. Je, unaona urithi wako k**a nafasi ya kuwatumikia wengine kwanza? Unajifunza nini kutoka kwa mfano wa Yoshua? Ni wapi katika maisha yako unaweza kusaidia wengine β€œmakabila madogo” kupata nafasi yao ya kustawi?

πŸ” MASWALI YA TAFAKARI:

🍞1. Je, umejifunza kushukuru na kuridhika na urithi wako uliojaliwa bila kuangalia wengine wamepewaje?

🍞2. Je unatumiaje baraka yako kuwainua wengine k**a walivyofanya kabila la Yuda kwa Simeoni?

🍞3. Je unajifunza nini kupitia kitendo cha watu kumpa Yoshua zawadi baada ya huduma yake ndefu?

🧱 MATUMIZI MAISHANI:

Chukua hatua ya kushirikisha wengine baraka zako – iwe ni muda, mali au ujuzi. Weka kando kile unachomiliki ili kuwainua wale wanaohitaji. Jua kwamba Bwana ana sehemu maalum kwa kila mmoja wetu, na kuwatumikia wengine hakupunguzi gawio lako.

_Andiko la Kutiamoyo_

Watu wa kabila la Dani walipopoteza nchi yao, walikwenda na kushambulia mji wa Leshemu. Waliushinda na kuuteka, na baada ya kuwaua wakazi wake wote, waliumiliki halafu wakaubadili Jina kuuita Dani; Jina ambalo lilikuwa la babu yao.(Yoshua 19:47 Kiswahili cha Kisasa).

_Neno la Baraka_ Benediction

Hata baada ya kushindwa katika jambo fulani, uwe na moyo wa ushujaa wa kujaribu kufanya jambo lingine, na katika jambo hili lingine, Bwana akupe mafanikio. Hata baada ya kupitia uzoefu mchungu wa kushindwa katika jambo fulani, Bwana akupe nguvu ya kuendelea kupambana na kufanya jambo lingine hadi ushindi utakapopatikana. Bwana abariki juhudi zako za kupambania kupata mwenzi wa maisha, kuleta amani katika ndoa yako, kuboresha afya yako, hali yako ya kiuchumi na zaidi ya yote Imani yako. (Hesabu 6:24-26).

_Tamko la Imani_

Kwa Neema ya Mungu ninaazimia kuwa kushindwa kwangu kwa jana hakutamaanisha mimi ni mtu wa kushindwa na leo na kesho. Ili mradi nina pumzi ya uhai, kamwe sitakata tamaa ninajua siku moja ndoto zangu zitatimia kwa sababu Mtetezi wangu yu hai. Nitaendelea kupambania mambo yangu ya kijamii, afya ya kimwili, katika shughuli zangu za kujipatia mkate wa kila siku na katika mapambano ya kiroho kwa matumaini ya ushindi kwa msaada wa Bwana, Ee Mwenyenzi Mungu, nisaidie! (Unaweza kuimba wimbo unaosema, Nionapo amani k**a shwari au nionapo shida, kwa hali zote umenijulisha ni salama rohoni mwangu)

πŸ”‘ SALA YA MWISHO:

Mungu anayegawa urithi, tunakuomba utufundishe kushirikisha baraka zetu kwa watu wengine. Tuweke tayari kuwapa wengine nafasi kabla ya kudai iliyo yetu. Asante kwa kutupatia viongozi wanaohudumu k**a Yoshua; tuwezeshe kuwathamini na kuwapatia ushirikiano. 7Tunakuomba utuwezeshe kuyafanya haya kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Tunaomba kwa jina la Yesu, Amina.

πŸ‘€πŸ‘€πŸ‘€Watayarishaji wa Mwongozo huu wa Biblia: Pr. Stephen Letta, Pr. Lusekelo Mwakalindile, na Pr. Enos Mwakalindile, Dar es Salaam, Tanzania.

➑️ Jiandae kwa Somo la Kesho: Sura ya 20 – Miji ya Kimbilio na Kimbilio la Neema.

10/11/2025

🍞 MKATE WA LEO KUTOKA KWA WACHUNGAJI: || ............................
Yoshua 16:1-10.
Urithi wa Efraimu na Mapungufu ya Utii.

❓ Je, unaendelea kutii hata baada ya kupokea baraka zako?

πŸͺ” UTANGULIZI NA MUKTADHA:

Sura hii inatoa urithi wa kabila la Efraimu, mmoja wa wana wa Yosefu. Inafafanua mipaka yake na miji yake. Licha ya kupokea sehemu nzuri, wana wa Efraimu hawakuondoa Wakanaani wote kutoka kwenye nchi yao; badala yake waliwaweka kwa kazi za kulazimishwa. Kutotii huku kunakuwa chanzo cha matatizo ya baadaye. Kuishi na Wakaanani kuliwafanya baadhi ya Waisraeli kuoana nao na kuiga ibada zao za sanamu (Waamuzi 2:1-3; 3:1-6, 10:6). Sura hii inaonyesha kwamba urithi bila utii kamili unaweza kuleta mizizi ya dhambi na ushawishi mbaya.

πŸ“– Soma Kwanza: Yoshua 16

Soma maelezo ya mipaka ya Efraimu na matokeo ya kuwabakiza Wakanaani. Tafakari kuhusiana na kuitikia vizuri baraka na urithi wako.

πŸ“š MUUNDO WA MADA NA UCHAMBUZI WAKE:

πŸͺ’1. Mipaka ya Efraimu – Mst. 1–9 – Maelezo ya mipaka ya urithi wa Efraimu; inajumuisha baadhi ya miji iliyowahi kuwa ya Manase.

πŸͺ’2. Wakanaani Wanaobaki – Mst. 10 – Efraimu hawawafukuzi Wakanaani, badala yake wanawaweka kulipa ushuru; hii inaonyesha kutokamilisha utii wao kwa Mungu.

_Anachosema Ellen G. White_

"Hata hivyo, haikumpasa Yoshua kuendeleza vita. Kulikuwako na kazi nyingine mbele yake ya kutekeleza kabla hajaacha utawala wa Israeli. Nchi yote, sehemu zilizotekwa pamoja na zile ambazo zilikuwa bado hazijashindwa, ilibidi zigawiwe miongoni mwa makabila haya. Na ilikuwa wajibu wa kila kabila kutiisha urithi wake mwenyewe. Iwapo watu wangekuwa waaminifu kwa Mungu, angewafukuza maadui zao kwenda mbali na wao; na aliahidi kuwapa urithi mkubwa zaidi iwapo wangebaki kuwa waaminifu kwa agano lake." (Wazee na Manabii Sehemu ya Pili uk 153).

πŸͺ” MUHTASARI WA MADA:

Baraka zinaweza kupungua ikiwa hatutii kikamilifu. Efraimu alipewa urithi mzuri lakini akashindwa kuondoa wapinzani; badala ya kufuata agizo la Mungu, walichagua faida ya muda mfupi ya ushuru. Tabia hii inatukumbusha kwamba kusitawisha dhambi ndogo kunaweza kuwa chanzo cha taabu baadaye. Uaminifu kamili unahitajika ili kuimarisha baraka.

πŸ‘₯ MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 16:1-10

βœ…1. Waefraimu waliingizwa katika makabila 12 kwa upendeeo badala ya baba yao Yusufu aliyekuwa mstari wa mbele kuwatetea katika nchi ya utumwa. Unadhani ni kwa nini hawakuwaondoa kabisa maadui zao k**a walivyofanya ndugu zao? Je waliwaonea huruma Wakanaani au walitaka kuwatumia k**a kitega uchumi?

βœ…2. Baadaye Efraimu walikuja kumwasi Mungu. Unadhani kitendo cha kuwaacha hai maadui zao kilichangia hali hiyo? (Hosea 4:17). Je unapoongoka na kumgeukia Yesu unapaswa kuachana na marafiki wa zamani ulioshiriki nao uovu?

βœ…3. Je, umepokea baraka fulani lakini hukutimiza maagizo yote ya Mungu kuhusu eneo hilo? Madhara yake yameonekana vipi? Kwa nini ni rahisi kuvumilia dhambi ndogo kwa sababu ya faida ya muda? Je unawezaje kukomesha β€œWakanaani” waliobaki kwenye maisha yako?

πŸ” MASWALI YA TAFAKARI:

🍞1. Kuna eneo gani katika maisha yako ambalo umeamua kulibakiza ili β€œkujipatia ushuru” badala ya kulimaliza kabisa? Utatumia njia gani kuhakikisha unafanya uamuzi wa utii kamili?

🍞2. Je, unathamini zaidi kupata baraka au kumtii Mtoa Baraka? (Tafakari kuhusu tofauti hiyo).

🍞3. Je uko tayari kupambana Ili kurithi maeneo yote ambayo Mungu amekuahidi? Je una uthubutu wa kumuomba Mungu akupanulie mipaka yako na kukupa maeneo mengine ya ziada ili kupanua ufalme wake hapa duniani? (Kutoka 34:24).

🧱 MATUMIZI MAISHANI:

Andika maeneo katika maisha yako ambayo unahitaji kukamilisha utii – tabia ambazo bado hazijatubiwa kikamilifu. Chukua hatua za kuziondoa kabisa. Omba msaada wa Mungu na ushirika wa marafiki wa kiroho ili kukomesha dhambi zilizobaki.

_Andiko la Kutia Moyo_

Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe Mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa kutoka kwa mkono wa Sauli; nami nikakupa nyumba ya Bwana zako, na wake wa Bwana zako kifuani mwako; nikakupa nyumba ya Israeli na ya Yuda; na k**a hayo yalikuwa machache, ningalikuongezea mambo mengine mengi. (2 Samweli 12:7-8). Bwana alikuwa tayari kuwaongezea makabila ya Israeli eneo la urithi.

_Tamko la Imani_

Ƙulikuwa na mtu mmoja Jina lake Yabezi, aliyeheshimiwa kuliko ndugu zake wote. Mama yake alimpa Jina la Yabezi kwa sababu alimzaa kwa maumivu. Lakini Yabezi alimwomba Mungu wa Israeli akisema, "Ee Mungu, nakusihi unibariki na kuipanua mipaka yangu. Mkono wako uwe pamoja nami na unilinde na kutokana na jambo lolote ovu, lisiniumize." Naye Mungu akamjalia yale aliyoomba.

_Neno la Baraka_
(Hesabu 6:24-26)

Bwana amekupatia maeneo ambayo unayamiliki kwa sasa, lakini hujakamilisha kumiliki maeneo yote ambayo amekuahidi na yuko tayari kukuongezea mengine k**a ukimwomba. Usiridhike na baraka ulizonazo wakati huu. Pambana kupata baraka zaidi kwa utukufu wake. Bwana akuongezee baraka kwa kuwafanikisha zaidi watoto wako na akufanye kuwa baraka kwa watu ambao wako karibu na wewe, Bwana aondoe magonjwa mwilini mwako na kukujalia afya njema na maisha marefu, Bwana abariki mashamba yako, shughuli zako za ujasiriamali, biashara zako na kazi yoyote ya kukupatia kipato kwa ajili ya utukufu wa Jina lake kuu.

πŸ”‘ SALA YA MWISHO:

Ee Bwana wangu, Wewe uliye mwaminifu kutimiza agano lako, hakika unastahili kuabudiwa na uhimidiwe milele na milele. Ninakushukuru kwa baraka ambazo umenipatia katika maisha yangu. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, naomba unisaidie kutii agizo lako la kutoiga desturi mbaya za Wakaanani au watu waovu wa dunia hii. Ee Bwana Yesu ninakuhitaji uwe Mkombozi wangu kutoka dhambini kwa sababu ninahitaji kuokolewa na damu yako iliyomwagika pale msalabani. Ninaomba unipe ushindi dhidi ya majaribu na uniandae kwa ajili ya kuirithi Kaanani katika mbingu mpya na nchi mpya. Naomba unisikie kwa sababu ninaomba kwa Jina la Yesu, Amina.

πŸ‘€πŸ‘€πŸ‘€ Watayarishaji wa Mwongozo huu wa Biblia: Pr. Stephen Letta, Pr. Lusekelo Mwakalindile, na Pr. Enos Mwakalindile, Dar es Salaam, Tanzania.

➑️ Jiandae kwa Somo la Kesho: Sura ya 17 – Urithi wa Manase na Mabinti wa Zelofehadi.

09/11/2025

🍞 MKATE WA LEO KUTOKA KWA WACHUNGAJI: ||............................
Yoshua 14:1-15.
Urithi wa Kalebu na Moyo Usiochoka.

❓ Je, unaendelea kuishikilia ahadi ya Mungu hata k**a imechukua miaka mingi?

πŸͺ” UTANGULIZI NA MUKTADHA:

Sehemu ya urithi wa makabila inaendelea kutolewa. Kisha Kalebu, mwana wa Yefune, kutoka kabila la Yuda, anamkumbusha Yoshua kuhusu ahadi ya Musa miaka 45 iliyopita. Kalebu alikuwa mmoja wa wale wapelelezi wawili waliotoka kupeleleza nchi na kuleta taarifa yenye imani, hivyo Musa aliahidi eneo ambalo alitembea litakuwa urithi wake. Sasa akiwa na umri wa miaka 85, Kalebu bado anasema ana nguvu k**a zamani na anataka mlima wa Hebroni unaokaliwa na majitu (Anakimu). Yoshua anambariki na kumpa Hebroni, na Kalebu anawafukuza wana wa Anaki. Hebroni inakuwa urithi wake wa kudumu.

πŸ“– Soma Kwanza: Yoshua 14

Soma mazungumzo ya Kalebu na Yoshua kuhusu ahadi ya zamani, jinsi anavyodai milima aliyoahidiwa, na jinsi anavyoshinda majitu. Tafakari uaminifu unaotaka kuvumilia hadi mwisho.

πŸ“š MUUNDO WA MADA NA UCHAMBUZI WAKE:

πŸͺ’1. Kugawa Nchi na Kumbukumbu ya Ahadi – Mst. 1–5 – Yoshua, Eleazari kuhani na viongozi wanagawa nchi kwa makabila yaliyosalia kwa kupiga kura; na wanakumbusha makabila ya Lawi hawana urithi wa ardhi bali wanapewa miji.

πŸͺ’2. Kalebu Adai Ahadi Yake – Mst. 6–15 – Kalebu anasimama mbele ya Yoshua na kukumbusha ahadi ya Musa; anaonyesha imani na nguvu zake; anaomba mlima wa Hebroni na anakubali kumshinda Anakimu; Yoshua anambariki na kumpa Hebroni, ambayo inakuwa milki ya Kalebu.

Wakati huu Kalebu na Yoshua, ndiyo walikuwa na umri mkubwa kuliko wote katika Israeli. Na badala ya kuomba apewe ardhi ambayo imekombolewa anaomba kupewa eneo ambalo halijatekwa ambalo lina majitu na miji yenye ngome imara, ambalo lilikuwa linaogopwa na wapelelezi kumi.

πŸͺ” MUHTASARI WA MADA NA UCHAMBUZI WAKE:

🌴1. Hadithi ya Kalebu inatufundisha uvumilivu na imani isiyoyumba. Alisubiri miaka 45 lakini hajasahau ahadi ya Bwana.

🌴2. Anafanya uamuzi wa kudai mlima mgumu na watu wenye nguvu ili aonyeshe kwamba Bwana bado ana nguvu.

🌴3. Uthabiti wake unaonyesha kwamba hatupaswi kujisalimisha kwa sababu ya umri mkubwa (uzee) au muda mrefu; uaminifu wa Mungu hauzeeki. (Zaburi 103:5) inasema, "Aushibisha mema uzee wako, ujana wako ukarejezwa k**a tai."). Hebroni inakuwa sehemu takatifu baadaye, mahali ambapo ufalme wa Daudi ulianzia.

🌴4. Katika Yoshua 14:6-12, Kalebu anatuonyesha mfano wa kuzungumza maneno chanya juu ya wema na baraka za Mungu maishani mwetu na uwezo ambao Mungu ametupatia wa kufanya mambo makuu.

πŸ‘₯ MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 14:1-15

βœ…1. Wana wa Israeli walirithishwa nchi kadhaa kila kabila likitwaa nchi mojawapo. Unadhani urithi walioahidiwa watakaokombolewa utahusu kurithi mataifa yaliyopo leo ulimwenguni au sayari zilizotapakaa huko angani? Je unapomfuata Mungu kwa ukamilifu huwezi kutoa habari inayotia watu hofu? Kwa nini Kalebu aliendelea kuwa mwenye nguvu hata baada ya kupigana vita ngumu na baada ya kufikisha miaka 85? Je ni kweli kuwa umri unaotumika kikamilifu katika kazi ya Mungu hauchoki wala kuzeeka?

βœ…2. (Kalebu na Joshua) kati ya wapelelezi 12 walikuwa waaminifu na kufanikiwa kuimaliza safari yao kwa ushindi. Nini siri ya mafanikio yao? Je unafanya nini kujihakikishia unakuwa kwenye kundi la washindi? Kuwapa watu hofu kuwa Mungu ameliacha kanisa lake na kuwashawishi waliache au wasisikilize viongozi wao kunaashiria upo kwenye kundi la washindi watakaoimaliza safari yao kwa ushindi?

βœ…3. Je kipi bora kujitwalia urithi mapema hata kwa njia ya hila na uchawa au kusubiri hata mwisho wakati wa uzee au wakati wa kustaafu Mungu awatumie watu kukupatia urithi na mali za kukusaidia maisha ya uzeeni? Je umehusika katika kufanya maisha yawaliomtumikia Mungu kwa uaminifu kuwa yenye baraka wakati wa uzee wao?

βœ…4. Nini faida ya nchi kutulia na vita kukoma? Nini kinachopelekea nchi kutulia na vita kukoma? Ni jitihada gani zinapaswa kuchukuliwa kwa nchi zilizokuwa vitani ili kukomesha vita na kurejesha utulivu katika nchi? Je, una watu ulioshiriki nao kuanzisha safari ya kundi la kiroho ambao unafarijiana nao sasa mnapoangalia mlikotoka na pale Mungu amewafikisha k**a kundi la kiroho lenye mafanikio?

βœ…5. Je, kuna ahadi za Mungu ulizosahau kwa sababu zimechukua muda mrefu? Je, Kalebu anakutia moyo vipi? Ni maeneo gani ya maisha yako yanayoonekana k**a β€œmilima” yenye majitu yanayokusubiri, na unapokeaje changamoto hizo?

πŸ” MASWALI YA TAFAKARI:

🍞1. Je, kuna watu wazee katika jamii yako wanaoonyesha imani k**a ya Kalebu? Je unajifunza nini kutoka kwao?

🍞2. Unahitaji uvumilivu gani ili kuendelea kuamini huku ukingojea utimilifu wa ahadi?

🧱 MATUMIZI MAISHANI:

Andika ahadi za Mungu ambazo zimechukua muda kutimia. Ziweke katika sala tena, ziamini tena, na chukua hatua fulani kwa vitendo kuelekea kuzitimiza, ukijua kwamba Mungu yuko mwaminifu.

_Andiko la Kutia Moyo_

Ndipo Yoshua akambariki Kalebu mwana wa Yefune na kumpa kuwa sehemu yake. Kwa hiyo, mji wa Hebroni ni sehemu yao wazawa wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi mpaka hivi leo, kwa sababu Kalebu alikuwa mwaminifu kwa Mwenyenzi Mungu, Mungu wa Israeli. (Yoshua 14:13-14 Kiswahili cha Kisasa).

_Neno la Baraka_ (Benediction)

Bwana akupatie imani, ujasiri na moyo wa uaminifu wa kufuata maagizo yake. Bwana akubariki kwa kukupatia mema ya nchi kwa utukufu wa Jina lake kuu. Bwana akutimizie ahadi zake katika maisha. Mungu akuwezeshe kufikia malengo yako katika mambo ya familia, afya, na uchumi. Watoto wako wabarikiwe na ibarikiwe kazi za mikono yako.

_Tamko la Imani_

Lakini sasa tazama! Ni muda wa miaka arobaini na mitano tangu Mwenyenzi Mungu alipoongea na Mose, wakati Waisraeli walipokuwa wanapitia jangwani. Tangu wakati huo Mwenyenzi Mungu k**a alivyoahidi, amenihifadhi hai mpaka leo, na sasa mimi nina umri wa miaka themanini na mitano. Lakini bado nina nguvu k**a nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote. Sasa naomba unipe nchi hii ya milima ambayo Mwenyenzi Mungu aliniahidi siku ile. Wewe ukisikia siku ile kwamba Waanaki (Majitu) waliishi humo katika miji yenye ngome; Mwenyenzi Mungu atakuwa pamoja nami, nami nitawafukuza k**a Mwenyenzi Mungu alivyosema. (Yoshua 14:12-14 Kiswahili cha Kisasa).

πŸ”‘ SALA YA MWISHO:

Mungu wa vizazi vyote, ninakuomba unijalie imani na nguvu k**a Kalebu. Nisaidie nikumbuke ahadi zako na kuziamini hata baada ya kupita kwa muda mrefu. Ninapokutana na β€œmajitu” katika maisha, na miji yenye ngome imara, nisaidie kutambua kwamba Wewe bado ni Yeye yule Jana, Leo na hata milele, na utanipigania na kunipa ushindi. Zaidi ya yote ninahitaji nguvu za kiroho kwa njia ya ujazo wa Roho Mtakatifu moyoni mwangu k**a ulivyofanya katika Pentekoste. Ninahitaji pia nguvu ya damu ya Yesu Kristo, iliyomwagika msalabani katika mlima wa Golgota. Ninaomba kwa Jina la Yesu, Amina.

πŸ‘€ πŸ‘€πŸ‘€Watayarishaji wa Mwongozo huu wa Biblia: Pr. Stephen Letta, Pr. Lusekelo Mwakalindile, na Pr. Enos Mwakalindile, Dar es Salaam, Tanzania.

➑️ Kesho: Sura ya 15 – Mipaka ya Yuda na Mchango wa Aksa

24/10/2025

USOMAJI BIBLIA KWA MPANGO: JOSHUA 4:1-24

1 Ikawa, hapo hilo taifa zima lilipokuwa limekwisha vuka Yordani, ndipo Bwana akanena na Yoshua, akamwambia,

2 Haya, twaeni watu waume kumi na wawili katika hao watu, kila kabila mtu mmoja,

3 kisha uwaamrishe, kusema, Twaeni mawe kumi na mawili, hapo katikati ya Yordani, mahali hapo miguu ya hao makuhani iliposimama imara, mwende nayo mawe hayo, mkayaweke nchi kambini, hapo mtakapolala usiku huu.

4 Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa amewaweka tayari tangu hapo, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja;

5 naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la Bwana, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mtu wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya kabila za wana wa Israeli;

6 ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya?

7 Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yalitindika mbele ya sanduku la agano la Bwana; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalitindika; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.

8 Basi wana wa Israeli walifanya vile vile k**a Yoshua alivyowaamuru, nao wakatwaa mawe kumi na mawili pale katikati ya Yordani, k**a Bwana alivyomwambia Yoshua, sawasawa na hesabu ya kabila za wana wa Israeli; wakayachukua wakavuka nayo hata mahali pale walipolala, nao wakayaweka nchi kuko huko.

9 Kisha Yoshua akapanga mawe kumi na mawili katikati ya Yordani, mahali pale miguu ya hao makuhani waliolichukua hilo sanduku la agano iliposimama; nayo yapo pale pale hata hivi leo.

10 Kwa kuwa makuhani waliolichukua hilo sanduku walisimama katikati ya Yordani, hata mambo yote Bwana aliyomwamuru Yoshua awambie hao watu yakaisha, sawasawa na hayo yote Musa aliyokuwa amemwamuru Yoshua; kisha hao watu wakafanya haraka wakavuka.

11 Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la Bwana likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu.

12 Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wakavuka, hali ya kuvaa silaha mbele ya wana wa Israeli, k**a Musa alivyowaambia;

13 walipata k**a watu arobaini elfu hesabu yao, wenye kuvaa silaha tayari kwa vita, waliovuka mbele ya Bwana, waende vitani, hata nchi tambarare za Yeriko.

14 Siku ile Bwana alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, k**a walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake.

15 Kisha Bwana akanena na Yoshua, akamwambia,

16 Haya, uwaamuru makuhani, hao waliolichukua sanduku la ushuhuda, kwamba wakwee juu kutoka mle katika Yordani.

17 Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani.

18 Ilikuwa, hapo hao makuhani waliolichukua sanduku la agano la Bwana walipokwea juu kutoka mle kati ya Yordani, na nyayo za miguu yao hao makuhani zilipoinuliwa na kutiwa katika nchi kavu, ndipo maji ya Yordani yaliporudi mahali pake, na kujaa na kuipita mipaka yake, k**a yalivyokuwa hapo kwanza.

19 Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko.

20 Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali.

21 Akawaambia wana wa Israeli, akasema, Watoto wenu watakapowauliza baba zao katika siku zijazo, wakisema, Mawe haya maana yake ni nini?

22 Ndipo mtakapowaarifu watoto wenu mkisema, Israeli walivuka mto huu wa Yordani, kwa njia ya nchi kavu.

23 Kwa sababu Bwana, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hata mlipokwisha kuvuka k**a Bwana, Mungu wenu, alivyoitenda Bahari ya Shamu, aliyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka;

24 watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa Bwana, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche Bwana, Mungu wenu, milele.

🍞 MKATE WA LEO KUTOKA KWA WACHUNGAJI: ||
---------------
Yoshua 4:1-24. Mawe ya Ukumbusho na Kumbukumbu ya Muujiza.

❓ Je, unahitaji kukumbuka kazi za Mungu ili imani yako iimarike?

πŸͺ” UTANGULIZI NA MUKTADHA:

Baada ya kuvuka Yordani, Mungu anamwambia Yoshua achague wanaume 12, mmoja kutoka kila kabila, wachukue mawe 12 kutoka katikati ya mto ambapo makuhani walisimama. Mawe haya yanajengwa k**a kumbukumbu katika Gilgali ili vizazi vya baadaye wakumbuke jinsi Mungu alivyokausha mto. Yoshua pia anasimika mawe 12 ndani ya Yordani mahali makuhani waliposimama. Watu wanafika Gilgali na kusheherekea tukio hilo kubwa, na Yoshua anawaambia wawaeleze watoto wao kuhusu nguvu ya Mungu. Kabila za mashariki zikiwa zimevuka, Yoshua anaheshimiwa k**a Musa mbele ya taifa zima.

πŸ“– Soma Kwanza: Yoshua 4

Soma kuhusu ukusanyaji wa mawe na ujenzi wa kumbukumbu. Tafakari umuhimu wa kukumbuka matendo ya Mungu katika familia na jamii.

πŸ“š MUUNDO WA MADA NA UCHAMBUZI WAKE:

πŸͺ’1. Kuchukua Mawe – Mst. 1–8 – Wanaume 12 wanachukua mawe kutoka mtoni kulingana na maagizo ya Mungu na Yoshua. Mawe yanawakilisha makabila yote.

πŸͺ’2. Makuhani na Kufuata Agizo – Mst. 9–18 – Yoshua anasimika mawe katika mto; makuhani wanasubiri hadi agizo la Mungu litimie; maji yanarudi baada ya wao kutoka mtoni.

πŸͺ’3. Kumbukumbu katika Gilgali – Mst. 19–24 – Mawe yanapangwa Gilgali; Yoshua anaeleza kuwa ni ishara ya ajabu ya Bwana ili mataifa yote wajue nguvu yake na watu wamche Yeye.

πŸͺ” MUHTASARI WA MADA:

🌴1. Utunzaji wa kumbukumbu za matendo ya Mungu ya wakati uliopita ni wa muhimu kwani unasaidia kuimarisha imani zetu na kutufanya kumtegemea Bwana sasa na wakati ujao. Watu wa Mungu walikuwa na desturi ya kutumia mawe na nyakati fulani kujenga minara ili kutunza kumbukumbu za muhimu (Yoshua 7:26; 24:26-27; Mwanzo 28:18-22; 31:45-471 na Samweli 7:12).

🌴2. Tunatakiwa kuwasimulia watoto wetu mambo mema ambayo Bwana ametutendea na kuirithisha imani yetu kwa kizazi kijacho.

🌴3. Watu wa kabila la Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wanavuka wakiwa tayari kupigana vita ili kuwasaidia ndugu zao. Ni vyema kutekeleza ahadi na wajibu katika kuwasaidia wengine kutimiza mahitaji yao mbalimbali. (Yoshua 4:12-13).

🌴4. Mungu anatimiza ahadi yake ya kumtukuza Yoshua. Bwana ni mwaminifu kutimiza Neno lake. (Yoshua 3:7, 4:14).

🌴5. Lengo kuu ya miujiza ni kuwafanya watu wa wamche Mungu. (Yoshua 4:23-24).

πŸ‘₯ MASWALI YA KUJADILI: JOSHUA 4:1-24

βœ…1. Je, kuna umuhimu wa kuweka kumbukumbu ya matendo makuu aliyokutendea Mungu kwenye maisha yako yaliyopita? Je umeacha alama gani maeneo mbalimbali uliyoishi ambacho ni kielelezo cha namna ulivyojitoa kwa ajili yao?

βœ…2. Unadhani kulikuwa na hatari ya wale makuhani kujiinua kwa kuwa maji yalisubiri nyayo zao zitoke majini ili yaanze kutiririka? Mungu alifanya nini kuzuia hali hiyo ya kujiinua? Je unajisikia fahari na sifa muujiza unapofanyikia kipitia matendo au matamshi yako?

βœ…3. Je Mungu anapotenda muujiza lengo ni kumuinua anayetumika kutenda muujiza au lengo ni kujitukuza Yeye mwenyewe Mungu? Je Mungu anaweza kuruhusu muujiza utendeke kupitia mtumishi wake anayejiinua? (Hesabu 20:7-12). Je watumishi wa Mungu wanaweza kufanya miujiza ambayo Mungu hajahusika nayo? (Mathayo 7:21-23).

βœ…4. Mawe yaliyopangwa katikati ya mto Yordani ambayo baadaye maji yalipofunguliwa hayakuonekana yalituma ujumbe gani? Je kuna wakati unaweza kuacha alama isiyoonekana kwa macho juu ya matendo yako mema kwa jamii husika? Unajisikiaje ikiwa mchango wako haujambuliwa?

βœ…5. Je, una alama za kukukumbusha jinsi Mungu amekuokoa na kukubariki? Je, unazishirikishaje kizazi kijacho? Kwa nini ni muhimu kushirikisha visa vyetu vya imani katika familia na jamii?

πŸ” MASWALI YA TAFAKARI:

🍞1. Ni β€œmawe” gani unaweza kuyaweka ili kukumbuka muujiza ambao Mungu amefanya katika maisha yako?

🍞2. Je, kusherehekea na kushukuru kunakuzuia kusahau matendo ya ajabu ya Mungu?

🧱 MATUMIZI MAISHANI:

Tafuta njia ya kuandaa kumbukumbu ya neema ya Mungu; andika shuhuda zako au weka ishara nyumbani zinazokukumbusha fadhili na ulinzi wa Mungu. K**a unaweza muombe mtu fulani aandike kitabu (Biography) kinachohusu mambo ambayo Mungu amekutendea au wewe mwenyewe andika kitabu chako (autobiography)

_Neno la Baraka_

Kwa sababu Bwana, Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mbele yenu, hadi mlipokwisha kuvuka k**a Bwana, Mungu wenu, alivyoitenda bahari ya Shamu, alivyoikausha mbele yetu hata tulipokwisha kuvuka; watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa Bwana, ya kuwa ni mkono wenye uweza, na ili nanyi mpate kumcha Bwana, Mungu wenu milele. (Yoshua 1:23-24).

_Tamko la Baraka_ (Benediction)

Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme akutendee mambo ya pekee, ambayo watu wa duniani wakiyaona na kuyasikia wakiri siyo mkono wa mwanadamu, bali ni mkono wa Mungu wenye uweza mkuu umefanya. Bwana akutendee haya katika imani yako ili kukuimarisha kiroho. Akutendee katika maisha yako ya kijamii, akutendee katika mwili wako kwa kukupatia uponyaji na afya njema, akutendee katika elimu yako au ya watoto wako, na akutendee kwa kubariki biashara yako na kazi ya mikono yako.

_Tamko la Imani_

Kwa Neema ya Bwana, ninapokea Neno na Tamko hili la Baraka za Bwana katika maisha yangu. Ninaazimia kuongeza bidii na uvumilivu katika kila jambo jema ninalolifanya na ninaamini nitauona mkono wa Bwana maishani mwangu. Ee Mwenyenzi Mungu nisaidie!

πŸ”‘ SALA YA MWISHO:

Bwana wa kumbukumbu, ninakushukuru kwa miujiza uliyonitendea. Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, ninaomba unisaidie nisisahau matendo yako na niyaweke akilini na moyoni. Niwezeshe kwa msaada wa Roho Mtakatifu kuwa mwaaminifu katika kuwasimulia watoto na majirani zangu hadithi ya neema yako ili wote wapate tumaini. Bwana Yesu ninakuhitaji uwe Mwokozi wangu sasa na hata milele. Ninaomba kwa jina la Yesu, Amina.

πŸ‘€πŸ‘€πŸ‘€Watayarishaji wa Mwongozo huu wa Biblia: Pr. Stephen Letta, Pr. Lusekelo Mwakalindile, na Pr. Enos Mwakalindile, Dar es Salaam, Tanzania.

➑️ Jiandae kwa Somo la Kesho: Sura ya 5 – Kutahiri Moyo na Kuabudu Upya.

Address

Mlandizi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NURU YA Matumaini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category