Institute of Judicial Administration

Institute of Judicial Administration The Institute of Judicial Administration (IJA) was founded by Cap.05 RE 2002, following the Presiden Thanks for being part of our IJA Facebook community.

Institute of Judicial Administration page is maintained by Public Relations Office providing news and information about people, programs and events at the Institution. We ask visitors to be respectful to one another and to the site hosts. Personal attacks, profanity, commercial solicitations, spam or other inappropriate contributions will be removed. We ask that you stay on point when con

tributing to an arising matter shared to be discussed and refrain from duplicate posts. The page administrators reserve the right to delete inappropriate or abusive visitor comments, and to permanently ban users from the Institute's page. You are all welcome...!!

Tabasamu ndani ya IJA
02/06/2026

Tabasamu ndani ya IJA

Mashindano!!
31/05/2026

Mashindano!!

UDAHILI UMEFUNGULIWA
30/05/2026

UDAHILI UMEFUNGULIWA

WANACHUO IJA WAPEWA MBINU ZA MAFANIKIO NA SOKO LA AJIRAWanachuo wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha Uongozi wa Mahak**a Lusho...
29/05/2026

WANACHUO IJA WAPEWA MBINU ZA MAFANIKIO NA SOKO LA AJIRA

Wanachuo wa mwaka wa mwisho wa Chuo cha Uongozi wa Mahak**a Lushoto (IJA) wamepatiwa elimu maalumu na ushauri wa kitaaluma (Career Guidance and Counseling) kwa lengo la kuwaandaa kitaaluma na kuwajengea uwezo wa kukabiliana na mazingira ya ajira na maisha baada ya kuhitimu masomo yao.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Mei 29, 2026 Chuoni Lushoto, yakihusisha mada mbalimbali zilizowasilishwa na baadhi ya watumishi wa Chuo pamoja na viongozi kutoka Jumuiya ya Wanasheria Vijana Tanzania (Association of Young Lawyers – AYL).

Katika mafunzo hayo, wanachuo wamehimizwa kuzingatia nidhamu, maadili na mwenendo mwema (attitude) k**a msingi muhimu wa mafanikio katika maisha yao ya kitaaluma na mara baada ya kumaliza masomo yao.

Aidha, washiriki wamefundishwa mbinu na namna bora ya kuandaa wasifu binafsi (Curriculum Vitae – CV), wakisisitizwa kuhakikisha taarifa zilizopo kwenye CV zinaendana na nyaraka nyingine muhimu ikiwemo cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Taifa (NIDA) na vyeti vya kitaaluma.

Sambamba na hilo, wanachuo wameaswa kujenga mtandao mpana wa mahusiano ya kitaaluma (networking), wakielezwa kuwa mahusiano mema ni nyenzo muhimu inayoweza kufungua fursa mbalimbali za maendeleo na ajira.

Vilevile, wamehimizwa kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali yanayoendelea duniani pamoja na uwezo wa kuchanganua mambo kwa kina.

Kwa upande wa matumizi ya teknolojia, wanachuo wamesisitizwa kutumia mitandao ya kijamii kwa tija, kwa kuwa mitandao hiyo ni sehemu ya kujinadi (visibility), ufadhili wa masomo na fursa nyingine za maendeleo.
Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahak**a ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, aliwataka wanachuo kuzingatia nidhamu, maadili na mwenendo mwema katika maisha yao ya kazi.

“Katika ulimwengu wa kazi za kitaaluma (corporate world), kinachoangaliwa zaidi ni mwenendo mzuri (right attitude) yako kuliko hata ujuzi ulionao. Hivyo hakikisheni mnakuwa na mwenendo mzuri,” amesema Mhe. Dkt. Kihwelo.

Aidha, aliwasisitiza wanachuo kujitofautisha kwa kufanya mambo kwa ubora na upekee badala ya kuwa wa kawaida, akiwataka kuzingatia kauli ya “Be Extraordinary and Not Ordinary.”

IJA NA AYL WAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAJENGA WANACHUO KITAALUMA Chuo cha Uongozi wa Mahak**a Lushoto (IJA) kimeingia maku...
28/05/2026

IJA NA AYL WAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAJENGA WANACHUO KITAALUMA

Chuo cha Uongozi wa Mahak**a Lushoto (IJA) kimeingia makubaliano ya ushirikiano (MOU) na Umoja wa Wanasheria Vijana (Association of Young Lawyers – AYL) wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) yenye lengo la kuwajenga wanachuo kitaaluma, stadi za maisha pamoja na kuwaandaa vyema kwa ushindani katika taaluma ya sheria na ajira.

Makubaliano hayo yamelenga maeneo mbalimbali muhimu ikiwemo utoaji wa ushauri wa kitaaluma na maisha (Mentorship), mafunzo ya vitendo kupitia Moot Court, mafunzo ya sheria, semina, pamoja na programu nyingine zitakazowawezesha wanachuo kuongeza uwezo wao wa kitaaluma na kiutendaji.

Hafla ya kusainiwa kwa Hati hiyo imefanyika leo Mei 28, 2026 Chuoni IJA na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka IJA pamoja na AYL ambayo ni sehemu ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Akizungumza wakati wa utiaji saini huo, Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahak**a ya Rufani, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, amepongeza hatua hiyo akieleza kuwa ushirikiano huo utafungua fursa kubwa kwa wanachuo kupata maarifa, uzoefu wa vitendo na mtandao mpana wa kitaaluma kutoka kwa wanasheria waliopo kazini.

“Makubaliano haya ni hatua muhimu katika kuwaandaa wanachuo wetu kuwa wataalamu wenye ushindani, maadili na uwezo wa kukabiliana na changamoto za taaluma ya sheria,” amesema Mhe. Dkt. Kihwelo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa AYL, Wakili Emmanuel Ukashu, ameishukuru IJA kwa kuonesha imani kwa chama hicho na kuahidi kuwa AYL itatekeleza kwa vitendo maeneo yote yaliyokubaliwa katika hati hiyo kwa manufaa ya wanachuo na maendeleo ya taaluma ya sheria nchini.

Wajumbe wengine wa AYL walioambatana katika ziara hiyo ya siku mbili ni Makamu Mwenyekiti, Wakili Joseph Mkami pamoja na Katibu wa Chama hicho, Esther Peter.

Katika ziara hiyo, viongozi wa AYL walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Chuo ikiwemo studio ya kisasa ya kuzalishia maudhui ya mtandaoni, maktaba pamoja na mabweni ya wanachuo.

Aidha, viongozi hao walifanya kikao na viongozi wa Serikali ya Wanachuo (IJASO) pamoja na viongozi wa vilabu mbalimbali vya wanachuo ambapo waliwahimiza kuwa na maono makubwa, kuzingatia uadilifu.

IJA, LEVO na GIZ WAENDELEA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KUTOA ELIMU YA SHERIA LUSHOTOKatika kuendelea kuimarisha uele...
28/05/2026

IJA, LEVO na GIZ WAENDELEA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KUTOA ELIMU YA SHERIA LUSHOTO

Katika kuendelea kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu maana, vyanzo na athari za ukatili wa kijinsia pamoja na masuala mbalimbali ya sheria, Chuo cha Uongozi wa Mahak**a Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na Asasi ya Kiraia ya Kisheria ya Legal Vision Organization (LEVO), kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani (GIZ), wametoa elimu ya kisheria na msaada wa sheria kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Zoezi hilo, ambalo litachukua siku sita, tayari limefanyika katika makanisa ya EAGT, TAG na Katoliki, Soko la Lukozi, Shule ya Sekondari Lukozi, Shule ya Msingi Lukozi, Kiwanja na Mng'alo pamoja na kwa makundi ya akina mama na waendesha bodaboda wa maeneo ya Mnazi na Mng’alo.

Elimu hiyo ilianza kutolewa Mei 24, 2026 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendelea kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kujenga mazingira salama yenye usawa, haki na heshima kwa wote.

Kupitia kampeni hiyo, wananchi wameendelea kuelimishwa kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia, umuhimu wa kulinda haki na utu wa kila mwanajamii pamoja na wajibu wa jamii kushiriki kikamilifu katika kutokomeza vitendo hivyo.

Zoezi hilo linaendeshwa na wahadhiri na maafisa sheria kutoka IJA, wasaidizi wa kisheria kutoka LEVO pamoja na maafisa kutoka GIZ.

Kutoka IJA yupo Mhadhiri Msaidizi Bw. Roggers Cletus, Maafisa Sheria Bi. Jackline Kulwa na Bw. George Banoba. Kutoka LEVO wapo Bw. Miraji Abdalah Malinda, Bi. Doris Maiko Kiungulia, Bi. Diana Godfrey pamoja na Bw. Gadson Wilfred Honkonyo.

Aidha, kutoka GIZ wapo Mshauri wa Sheria Bi. Neema Ndemno na Mtaalamu wa Mawasiliano, Uhamasishaji na Kampeni Bi. Agnes Mwafifi.

Hii ni awamu nyingine ya kampeni ya utoaji wa elimu na msaada wa sheria inayotekelezwa na GIZ, IJA na LEVO kwa jamii ya Lushoto, ambapo awamu ya awali ilifanyika mwezi Septemba mwaka 2024.

Aidha, GIZ imekuwa mstari wa mbele katika kupinga vitendo vya ukatili wa jinsia ambapo katika kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ili waleta pamoja Mahakimu Wakazi, Mawakili wa Serikali, Polisi dawati la jinsia, viongozi wa dini, wa kimila.

27/05/2026
Eid al Adha Mubarak!!
26/05/2026

Eid al Adha Mubarak!!

PONGEZI ZA UTEUZI
21/05/2026

PONGEZI ZA UTEUZI

MAAFISA WA MAHKAMA ZANZIBAR WAJIFUNZA UZOEFU WA BARA KATIKA USIMAMIZI WA MASHAURI YA KAZI NA BIASHARAMajaji, Naibu Wasaj...
19/05/2026

MAAFISA WA MAHKAMA ZANZIBAR WAJIFUNZA UZOEFU WA BARA KATIKA USIMAMIZI WA MASHAURI YA KAZI NA BIASHARA

Majaji, Naibu Wasajili, Mahakimu na Maafisa Sheria kutoka Divisheni ya Kazi na Divisheni ya Biashara ya Mahk**a Kuu ya Zanzibar wameanza mafunzo maalumu ya kuboresha uendeshaji wa mashauri ya migogoro ya kazi na biashara, wakijifunza kutokana na uzoefu wa Mahak**a ya Tanzania Bara.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanafanyika kuanzia Mei 19 hadi 21, 2026 katika Chuo cha Uongozi wa Mahak**a Lushoto(IJA), ambapo yatahusisha washiriki 12, ambapo sita wanatoka Divisheni ya Kazi na wengine sita kutoka Divisheni ya Biashara.

Akifungua mafunzo hayo, Jaji wa Mahak**a ya Rufani ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, amesema Mahak**a za Tanzania Bara zimejijengea uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa mashauri ya kazi na biashara.

“Kwa miaka mingi, Divisheni za kazi na biashara za Tanzania Bara zimejenga uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa mashauri ya kazi na biashara, kushughulikia kesi ngumu, pamoja na kuimarisha ufanisi wa utoaji wa haki katika Mahak**a maalum.Uzoefu huu ni muhimu kwa maendeleo ya divisheni za Mahk**a ya Zanzibar,” amesema Mhe. Dkt. Kihwelo.

Aliongeza kuwa kutokana na mabadiliko yanayoendelea katika sekta za kazi na biashara, ni muhimu kwa maafisa wa mahak**a kuendelea kujifunza na kubadilishana uzoefu ili kuongeza ufanisi na kuboresha upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Mhe Dkt. Yose Mlyambina akitoa neno la utangulizi, amepongeza mafunzo hayo na kubainisha kuwa yameandaliwa kwa ustadi mkubwa utakaowafanya washiriki kupata uelewa na ujuzi mkubwa katika uendeshaji wa mashauri hayo.

Mafunzo hayo yanahusu Uendeshaji wa mashauri ya kazi katika Mahak**a ya Kazi na mbinu za kushughulikia migogoro ya kibiashara katika Mahak**a ya Biashara yanatarajiwa kuwapa washiriki fursa ya kubadilishana uzoefu wa kitaaluma na kuimarisha uwezo wao katika kushughulikia mashauri kwa ufanisi zaidi.

Hii ni mara ya tatu kwa Chuo kuendesha mafunzo kwa maafisa wa Mahk**a kutoka Zanzibar, baada ya awali kutoa mafunzo Unguja na Pemba kuhusu uendeshaji bora wa mashauri ya uchaguzi.

Address

P. O. Box 20
Lushoto

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Institute of Judicial Administration posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Institute of Judicial Administration:

Share