03/02/2022
CASE ANALYSIS/UCHAMBUZI WA KESI.
Huu ni uchambuzi wa kesi kabla hujaenda mahak**ani unapaswa kubaini Yafuatayo:
(i)NATURE OF CAUSE OF ACTION
Hapa hupata kugundua hii ni kesi aina gani na iende mahak**a gani yenye mamlaka ya kusikiliza Shauri hilo, Je hilo shauli liko nje ya muda ua ndani ya muda, k**a liko nje ya muda nini cha kufanya, je hiyo kesi inapelekwa kwa njia gani je ni petition, application au plaint ikiwa inapelekwa kwa njia ya petition ukaandaa plaint.
(ii)KUFUATA HATUA ZA KISHERIA/PROCEDURE COMPLIANCE.
Katika kila kesi angalia hatua za kisheria k**a zimefuatwa/au tazama jinsi hatua za kisheria zilivyo tajwa na sheria ni muhimu kuzingatia sana hili ili kuondokana na mapingamizi yasiyo ya lazima.
(iii)USHAHIDI ULIOPO/AVAILABLE EVIDENCE.Mambo ya mambo muhimu sana ni kuangalia je kuna ushahidi wa kutosha unaoweza kukusaidia katika kesi yako, kuna nyaraka muhimu za kukulinda na kutetea madai yako, ainisha hizo nyaraka muhimu na zitazame,
(iv)MASHAHIDI WALIOPO/AVAILABLE WITNESS.
Angalia k**a kuna mashahidi wa kutosha kutetea au k**a kuna mashahidi wa kutosha au kuthibitisha kesi yako wale ni watu wenye uelewa na weredi wa jambo wanalotaka kulitolea ushahidi ikiwa ni pamoja na vielelezo, angalia k**a wanauwezo wa kuelezea vyema ushahidi wako.
(v)NAFUU ZA KISHERIA/AVAILABLE REDRESS.
Je unapeleka kesi mahak**ani kwa lengo gani unataka mahak**a ikufanyie nini? je hicho unachokiomba mahak**a ina mamlaka ya kukupa?,
(vi)UTETEZI/POSSIBLE DEFENCES
Kuangalia k**a kuna utetezi wowote kisheria dhidi yako unaweza kukusaidia ni jambo la muhimu zaidi. Hii ni kwa wote anayesh*taki na anayesh*takiwa.Angalia udhaifu wa kesi yako na jua jinsi ya kuutetea, angalia udhaifu wa aliye msh*taki na jua jinsi ya kuutumia kulinda kesi.
(vii)NJIA MBADALA YA KUTATUA MIGOGORO/ALTERNATIVE DISPUTE RESOLUTION.Kabla hujaamua kwenda mahak**a au kabla hujaxhitakiwa fikiria k**a kuna haja ya kutatua kesi nje ya mahak**a, mkatatua nje ya mahak**a kupunguza gharama na kupoteza muda.