Je. Yesu kristo ni nani

Je. Yesu kristo ni nani Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Je. Yesu kristo ni nani, Legal, 0752699107, Kibondo.

03/12/2024

*UKRISTO WA JANA WA LEO.*
Naliwaambia yako mambo mengi yalikuwa katika Ukristo wa asili wa mwanzoni na hayapo baadhi ya hayo kwenye Ukristo wa leo.

Na mengi yaliyobuniwa na wanadamu leo hayakuwepo kabisa kwenye Ukristo wa asili wa mwanzoni.

Ukristo wa mwanzoni ulijengwa juu ya mafundisho ya Mitume, na Wakristo wa mwanzoni waliwasikiliza Mitume na kutii yale waliyoyafundisha kwa kuwa walitambua wito wao wa Kiungu.

*Maandiko yanasema hivi;*

Matendo ya Mitume 2:42
[42] _*Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume,* na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali._

Wakawa WAKIDUMU kwa maneno mengine wakishikilia MAFUNDISHO YA MITUME, *kwa kuwa hao Mitume waliambiwa haya na Bwana Yesu;*

Mathayo 28:20
[20] _na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na *tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.*_

Na Bwana akasisitiza kuwa atakuwa pamoja nao siku zote, sio tu mpaka kifo chao lakini mpaka ukamilifu wa dahari, hiyo ni kusema mpaka wangeondoka duniani Bwana angeendelea kuwa mwaminifu kuwa upande wao.

*Na kabla ya kusulubiwa kwake alisema haya katika maombi yake ya KIKUHANI;*

Yohana 17:20
[20] _Wala si hao tu ninaowaombea; *lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.*_

Bwana anasema si hao tu ninaowaombea (MITUME) lakini na wale WATAKAONIAMINI kwasababu ya NENO LAO.

Katika maombi ya Kikuhani alitukumbuka na sisi leo ambao tutamwamini kupitia NENO LA MITUME ambalo wazi SI NENO LAO MITUME ni la Mungu, lakini hapa alisema NENO LAO.

Bwana aliwainua sana Mitume k**a watenda kazi wake.

*Ndiyo maana Yohana anaujasiri kusema;*

1 Yohana 4:6
[6] _*Sisi twatokana na Mungu.* Yeye amjuaye Mungu atusikia; *yeye asiyetokana na Mungu hatusikii.* Katika hili twamjua Roho wa kweli, na roho ya upotevu._

*Anasema kwa uhakika asiyetokana na Mungu hatusikii.*

Na Bwana Yesu alishatangaza hili kwa ajili yao;

Luka 10:16
[16] *Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi,* naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye

12/11/2024

Je yesu kristo ni nani?
Maana alisema

β€œNa uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.”
β€” Yohana 17:3 .

Address

0752699107
Kibondo

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Je. Yesu kristo ni nani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category