UDSM Legal Aid Clinic

UDSM Legal Aid Clinic Exists to deliver free legal services to marginalized and vulnerable communities in Tanzania particularly those unable to afford legal representation.

Our services are Legal Education, Legal Advice, Drafting Legal Documents, & Mediation Services.

26/04/2026

Hivi ndivyo tulivyomaliza siku tatu za huduma ya msaada wa kisheria pamoja na elimu kuhusu maswala ya ukatili wa kijinsia iliyofanyika Bunju A, tunashukuru wananchi wote waliokuja kupata msaada wa kisheria na elimu iloyotolewa toka tarehe 23-25 April, asante wadau wetu tulioshirikiana nao pamoja na ofisi ya kata Bunju na ofisi za serikali ya mtaa. Huu ulikua mwanzo mzuri wa ushirikiano katikata kuhakikisha tunakua na jamii salama.

Leo tumekuwa na wakati mzuri na wenye tija tukiwahudumia wakazi wa Bunju A (Bunju Shule). Kupitia kliniki yetu ya msaada...
23/04/2026

Leo tumekuwa na wakati mzuri na wenye tija tukiwahudumia wakazi wa Bunju A (Bunju Shule). Kupitia kliniki yetu ya msaada wa kisheria, tumefanikiwa kutoa suluhisho na ushauri kwenye:
βœ… Migogoro ya kifamilia na ardhi.
βœ… Migogoro ya mahali pa kazi.
βœ… Ushauri wa kisheria na msaada wa kisaikolojia kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia (GBV).

Shukrani za pekee kwa Ofisi ya Kata ya Bunju A, Idara ya Maendeleo ya Jamii, , na kwa ushirikiano huu wenye lengo la kujenga jamii salama.

BADO HATUJAMALIZA! πŸ“’
Tunaendelea kuwahudumia wakazi wote wa Bunju na maeneo ya jirani kesho Tarehe 24 hadi 25 Aprili, 2026.

K**a una changamoto yoyote ya kisheria au unahitaji ushauri wa kisaikolojia, karibu tukusikilize na kukusaidia. Tunajenga jamii isiyo na ukatili!

Katika harakati ya kuhakikisha tunamaliza kabisa ukatili wa kijinsia kwa watu wote, piga namba hii kwa ajili ya kuripoti...
16/04/2026

Katika harakati ya kuhakikisha tunamaliza kabisa ukatili wa kijinsia kwa watu wote, piga namba hii kwa ajili ya kuripoti au kutoa taarifa pale unapokutana, au unapoona ukatili ukifanyika.

Tukiendelea Kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma! Leo, Kliniki ya Msaada wa Kisheria ya UDSM (Legal Aid Clinic) ipo...
11/04/2026

Tukiendelea Kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma!

Leo, Kliniki ya Msaada wa Kisheria ya UDSM (Legal Aid Clinic) ipo Shule ya sheria(Kampasi Mikocheni) kutoa mafunzo kwa kundi la watu wa kuaminika (Fit Persons) kutoka wilaya Temeke Kuanzia kuelewa Kanuni za Sheria ya Mtoto (Fit Persons) za mwaka 2019 hadi kusimamia afya ya mtoto, tunaiandaa jamii yetu kuwa mstari wa mbele dhidi ya ukatili wa kijinsia (GBV) na utelekezaji.

Mafunzo haya yamelenga kukumbushana kuhusu sheria, nafasi na umuhimu wa watu wa kuaminika katika jamii.

Shukrani za dhati kwa wawezeshaji wetu na wanajamii wote waliojitokeza!

Leo, Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-LAC) kimefanikisha kwa mafanikio mafunzo muhimu...
10/04/2026

Leo, Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-LAC) kimefanikisha kwa mafanikio mafunzo muhimu yaliyofanyika katika Shule kuu ya sheria kwa ajili ya Maafisa Ustawi wa Jamii wetu kutoka Temeke.

Ilikuwa siku ya mafunzo mazuri na ushirikiano tukilenga Amri za Matunzo na Ulinzi wa Mtoto, pamoja na jukumu letu la pamoja katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.

Mambo muhimu yaliyojiri katika vikao vya leo ni pamoja na:
βœ… Haki ya Kukaa na Mtoto na Matunzo: Tukichambua masuala ya kisheria yanayohusu familia.

βœ… Mipango ya Matunzo na Ulinzi: Kutoka kwenye amri za mahakama hadi hatua za utekelezaji.

βœ… Usimamizi wa Mahakama za Watoto: Kuelewa mamlaka ya kisheria na mipaka ya kazi.

βœ… Sifa za Kuasili Mtoto: Uchambuzi wa kina wa sheria za kuasili watoto nchini Tanzania.

Shukrani za dhati kwa Dkt. Veronica Buchumi na Dkt. Florencia Kimario kwa kushiriki utaalamu wao na kuwaongoza maafisa wetu katika masuala haya muhimu ya kisheria.

Kwa pamoja, tunaimarisha mstari wa mbele wa ulinzi wa watoto!


Baada ya mafanikio makubwa ya mafunzo yetu ya Januari, tumefungua semesta hii kwa Awamu ya Pili ya Uweshaji Maarifa (Cap...
09/04/2026

Baada ya mafanikio makubwa ya mafunzo yetu ya Januari, tumefungua semesta hii kwa Awamu ya Pili ya Uweshaji Maarifa (Capacity Building) kwa ajili ya wanachama wa Klabu ya Msaada wa Kisheria (Legal Aid Clinic) – Chuo Kikuu cha Dar es Salaam!

Safari hii, tumewaleta wataalamu bingwa, mawakili, na walimu wa sheria ili kuziba pengo kati ya nadharia za darasani na uhalisia wa kazi.

Nini kimejiri?
Wanafunzi wetu wamepata fursa ya kipekee ya kujifunza kwa vitendo:
βœ… Namna ya kupokea na kuhudumia wateja (Client Consultation).
βœ… Mbinu bora za uandaaji wa nyaraka za kisheria.
βœ… Taratibu za kufungua mashauri (Filing cases) na uendeshaji wake.

Kwanini tunafanya hivi?
Tunaamini kuwa kuona na kufanya kwa vitendo ndiyo nyenzo kuu ya kujiamini. Tunawaandaa vijana hawa kuwa watendaji makini na wenye ujasiri wanapopata dhamana ya kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.

Kazi inaendelea! Stay tuned kwa updates zaidi za mafunzo haya ya siku tatu.

Heri ya Pasaka, kwenu nyote ikawe siku ya baraka,furaha na Amani.
05/04/2026

Heri ya Pasaka, kwenu nyote ikawe siku ya baraka,furaha na Amani.

Nyingine tenaaa! πŸ”₯Katika harakati za kusogeza elimu ya sheria kwa vijana wetu kuanzia ngazi ya sekondari, leo tulikuwa n...
26/03/2026

Nyingine tenaaa! πŸ”₯

Katika harakati za kusogeza elimu ya sheria kwa vijana wetu kuanzia ngazi ya sekondari, leo tulikuwa na wasaa mzuri wa kutembelea Shule ya Sekondari Mikocheni. Hii ilikuwa ni klabu yetu ya 7 ya kutoa elimu ya msaada wa kisheria!

Muitikio ulikuwa wa kishindo, na tunajivunia kuona familia ya watoa msaada wa kisheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ikizidi kukua.

Shule gani nyingine ungependa tuifikie? Tuambie kwenye comment hapo chini! πŸ‘‡πŸΎ

Je, unajua kuwa ukatili wa kijinsia (GBV) ni changamoto ya jamii nzima na si ya mtu mmoja pekee? Ukatili huu huathiri af...
24/03/2026

Je, unajua kuwa ukatili wa kijinsia (GBV) ni changamoto ya jamii nzima na si ya mtu mmoja pekee?

Ukatili huu huathiri afya, elimu, na mustakabali wa vijana wetu. Ni jukumu letu sote:
βœ… Kulinda na kuheshimu usiri wa waathirika.
βœ… Kukataa vitendo vyote visivyo sahihi.
βœ… Kuripoti mapema matukio ya ukatili.

Kumbuka: Kuzuia ni bora kuliko kutibu. Tuungane kuifanya jamii yetu kuwa mahali salama kwa kila mmoja. 🀝

Je, unajua kuwa ukatili wa kijinsia (GBV) ni changamoto ya jamii nzima na si ya mtu mmoja pekee?  Ukatili huu huathiri a...
24/03/2026

Je, unajua kuwa ukatili wa kijinsia (GBV) ni changamoto ya jamii nzima na si ya mtu mmoja pekee?

Ukatili huu huathiri afya, elimu, na mustakabali wa vijana wetu. Ni jukumu letu sote:
βœ… Kulinda na kuheshimu usiri wa waathirika.
βœ… Kukataa vitendo vyote visivyo sahihi.
βœ… Kuripoti mapema matukio ya ukatili.

Kumbuka: Kuzuia ni bora kuliko kutibu. Tuungane kuifanya jamii yetu kuwa mahali salama kwa kila mmoja. 🀝

Eid Mubaraka, kwa waislam wote ikawe siku ya baraka na furaha kwenu na familia zenu.
21/03/2026

Eid Mubaraka, kwa waislam wote ikawe siku ya baraka na furaha kwenu na familia zenu.

Address

Dar Es Salaam
14113

Opening Hours

Monday 07:45 - 04:00
Tuesday 07:45 - 04:00
Wednesday 07:45 - 04:00
Thursday 07:45 - 04:00
Friday 07:45 - 04:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UDSM Legal Aid Clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category