27/08/2025
UMUHIMU WA TATHMINI.
Miongoni mwa changamoto kubwa ninazoziona kwa vijana wengi siyo kukosa maono, siyo ukosefu wa malengo, wala siyo mtaji au wateja. Tatizo kubwa ni hili: kukosa tathmini — kabla, wakati, na baada ya kila hatua wanayopiga.
Tathmini ni mchakato wa kupima thamani, gharama au matokeo ya jambo. Kwa lugha rahisi, ni upimaji au uchambuzi.
Mara tu unapobaini kusudi lako na ndoto unazotaka kuzitimiza, hatua ya kwanza kabisa ni kujiuliza:
👀Je, maono yangu ni makubwa au madogo kiasi gani?
🤠Naweza kuutimiza vipi kwa usahihi?
⌚Utachukua muda gani?
💰Thamani yangu ya sasa ni ipi, na ninakusudia kufikia thamani gani?
🤔Nipo na watu wa aina gani, na watasaidia au kuharibu maono yangu?
Maswali haya ndiyo husaidia kuhesabu gharama ya maono. Ukishindwa kuyapima kwa makini, unaweza kupoteza ndoto yako kabisa.
Ni bora uchelewe kuanza biashara, uwekezaji, au hata uhusiano wa ndoa, kuliko kuingia bila tathmini ya kina.
✅Usioe au kuolewa bila tathmini ya gharama.
✅Usiachane na kazi ili kujiajiri bila kutathmini matokeo.
✅Usiharakishe kuwekeza fedha kwenye biashara usiyoijaribu bila tathmini.
✅Na usikimbilie kukosoa mifumo, serikali au taasisi bila tathmini ya matokeo yake.
📌📌mwalimu mmoja alisema: “Mbegu moja inaweza kutoa 30%, 60% au hata 100%. Lakini kosa dogo kwa kukosa tathmini linaweza kukugharimu mavuno yote.”
Hata Yesu Kristo alifundisha kanuni hii katika Luka 14:28-30:
> “Kwa maana ni yupi kati yenu, akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba ana vya kutosha kukamilisha?
baada ya kuuweka msingi, naye hawezi kuumaliza, wote wamwonapo waanze kumdhihaki,
wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, naye hakuweza kumaliza.” (Luka 14:28-30)
So,
Matokeo ya kutofanya tathmini ya kina kabla ya hatua fulani ni mabaya na hayatoishia tu kukuathiri binafsi lakini hata jamii na ulimwengu unaokuzunguka utashuhudia na kukucheka kwa dharau ....
Na mimi pia sitasita kujumuika nao ,Tutakucheka tu😂😂