IJUE Sheria upate haki yako

IJUE Sheria upate haki yako Lawyer | Legal Consultant | Business & Corporate | Labour & Employment | Contract Advisor | Legal Education Content Creator.
📞& Whtsp 0654819753.

Wanandoa wengi wenye utaifa tofauti wanapofunga ndoa hujikuta wakijiuliza mwongozo wa kisheria utakaotumika iwapo watata...
16/05/2026

Wanandoa wengi wenye utaifa tofauti wanapofunga ndoa hujikuta wakijiuliza mwongozo wa kisheria utakaotumika iwapo watataka kutalikiana, kugawa mali walizochuma pamoja, na kuamua hatma ya ulezi wa watoto wao, hasa pale mali na watoto wanapokuwa katika mataifa tofauti.

Kwa wanandoa ambao mmoja ni Mtanzania na ndoa ilisajiliwa nchini, mahak**a za Tanzania zina mamlaka ya kusikiliza shauri la talaka, ambapo wito wa mahak**a hutolewa na kufikishwa kwa mwenza wa kigeni kupitia balozi wa Tanzania katika nchi anakokaa au kupitia dalali wa mahak**a walioteuliwa na Mahak**a Kuu.

Mali zilizopo Tanzania hugawanywa kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa ya Tanzania kwa kuzingatia mchango wa kila mmoja, huku ushahidi wa mwenza aliye nje ya nchi ukiwasilishwa kwa njia ya affidavit na Ikiwa ni ushahidi wa mdomo, mahak**a inaweza kutumia video conference. Mali zilizopo nje ya Tanzania hugawanywa kwa mujibu wa sheria za nchi husika, kwani mahak**a za Tanzania hazina mamlaka ya kugawa mali nje ya mipaka yake.

Kwa upande wa watoto, iwapo wapo Tanzania, mahak**a hutumia Sheria ya Ndoa kwa kuzingatia kanuni ya ustawi wa mtoto, na ulezi unaweza kutolewa kwa mzazi yeyote kulingana na maslahi ya watoto; lakini iwapo wapo nje ya Tanzania, sheria za nchi wanapoishi ndizo zitatumika kuamua hatma ya ulezi, ingawa jukumu na haki za wazazi hubaki za kudumu.

Vilevile, k**a ndoa ilisajiliwa katika nchi ya kigeni, taratibu za talaka, mgawanyo wa mali na malezi ya watoto hutolewa kwa kutumia sheria za nchi husika, lakini iwapo mali zingine na watoto wapo nchini Tanzania, basi Sheria ya Ndoa ya Tanzania itatumika kugawa mali na kutoa ulezi wa watoto kwa wazazi hao.

Baada ya hukumu ya talaka kutolewa Tanzania, hutumwa kwa balozi wa Tanzania ili kuwasilishwa kwa mahak**a ya nchi ya mwenza wa kigeni kwa uthibitisho na utambuzi wa uhalali wa talaka hiyo, na vivyo hivyo hukumu ya talaka iliyotolewa nje hutumwa Tanzania kupitia balozi na Wizara ya Mambo ya Nje ili mahak**a za Tanzania ziiidhinishe na kuitambua rasmi.

NUKUU
Sheria inalinda haki zako

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein

Waajiriwa na wafanyabiashara wengi wadogo mara nyingi huvunja mikataba kwa kukiuka baadhi ya vifungu vya msingi. Licha y...
06/05/2026

Waajiriwa na wafanyabiashara wengi wadogo mara nyingi huvunja mikataba kwa kukiuka baadhi ya vifungu vya msingi. Licha ya kufahamu kuwa tayari wamekiuka masharti hayo, baaadhi ya wahusika huomba mazungumzo na waajiri au washirika walioingia nao mikataba ili waendelee na mikataba husika ambayo kisheria tayari washaivunja. Kwa dhumuni waweze kutekeleza kile walichoshindwa kukamilisha katika makubaliano waliyoingia.

Kisheria, mara tu mkataba unapovunjika kwa kukiuka masharti ya msingi, mkataba huo unapoteza uhalali wake na hauwezi kuendelezwa tena. Makubaliano yoyote yanayofanywa baada ya kuvunjika kwa mkataba yanachukuliwa k**a makubaliano mapya, hata k**a wahusika ni wale wale na mada husika inafanana na ile ya awali.

Aidha, waajiriwa na wafanyabiashara wadogo wanapaswa kutambua kuwa endapo wataona hawawezi kutekeleza majukumu ya kimkataba kwa wakati uliokubaliwa, na tayari wamesaini mikataba husika, ni wajibu wao wa kisheria kufanya mazungumzo na wahusika wa mikataba hiyo kabla ya kuvunja masharti yoyote ya msingi.

Mazungumzo hayo lengo lake ni kufanya mabadiliko katika mikataba na yanapaswa kufanywa kwa ridhaa ya pande zote na kwa kuzingatia misingi ya nia njema, uwazi na usawa ambapo pande zote watakubaliana kubadilisha au kurekebisha masharti, ili waweke masharti ambayo yanayowapa muda wa kutekeleza majukumu ipasavyo.

Hata hivyo, mabadiliko hayo yanapaswa kuwa kwa maandishi ili kudumisha uhalali wa makubaliano. Makubaliano hayo mapya yanapounganishwa katika mkataba uliopo, yanakuwa na nguvu sawa kisheria na vifungu vya awali.

Zaidi ya hayo, k**a upande mmoja wa mkataba hautokubaliana na upande mwingine kile wanachokihitaji, majukumu ya kimkataba yatatekelezwa kulingana na makubaliana ya awali. Upande utakaovunja mkataba utabeba dhima ya kisheria kwa uvunjifu huo.

NUKUU:
Mkataba sio chombo cha majaribisho, ni nyenzo inayoweza kukubebesha dhima ya kisheria pindi ukikiuka masharti na vifungu vya msingi.

WITO:
Heshimuni makubaliano ya mkataba, badilisheni kwa ridhaa na si kwa uvunjaji.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

Katika sekta ya ajira na kazi, wafanyakazi wa mkataba wa kudumu hubaki na sintofahamu juu ya hatma ya kuongezewa mishaha...
04/05/2026

Katika sekta ya ajira na kazi, wafanyakazi wa mkataba wa kudumu hubaki na sintofahamu juu ya hatma ya kuongezewa mishahara, kwa kuwa mishahara yao haiongezeki licha ya kazi kubwa wanayoifanya pamoja na faida wanayomletea mwajiri na kampuni yake.

Baadhi yao hudiriki kukiuka maadili ya kazi zao ili kujiongezea kipato kwa njia zisizo halali, wengine hutamani kufanya maamuzi ya kuachana na kazi zenyewe, ila kutokana na ukosefu wa elimu ya kazi na mikataba kisheria huogopa kufanya hivyo, wakijiuliza juu ya hatma yao itakuwaje pindi watakapoachana na kazi hizo kiholela.

Kisheria, kila mfanyakazi ana haki ya kuomba kuongezewa mshahara kwa kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa. Hata hivyo, ni muhimu mfanyakazi kutambua kuwa, haki ya ongezeko la mshahara haitathminiwi kwa muda wa utumishi pekee mfanyakazi aliotumikia kampuni au taasisi husika, bali hutathminiwa kwa utendaji na ufanisi wa kazi, nidhamu na mchango wa mfanyakazi husika katika kufanikisha malengo ya kampuni au taasisi.

Aidha, mfanyakazi wa mkataba wa kudumu miongoni mwa taratibu za kisheria ambazo unaweza kuzifuata kuomba ongezeko la mshahara ni pamoja na kuwasilisha maombi rasmi kwa mwajiri kuhusu kuongezewa mshahara ukitaja sababu za kuongezewa mshahara.

Zaidi ya hayo, maombi hayo mfanyakazi unapaswa kuwasilisha kwa maandishi ili kuonyesha uwazi na ushahidi wa maombi yako. Mwajiri atakuwa na wajibu wa kuyajibu maombi hayo kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa. Endapo mwajiri atakataa kujibu maombi hayo bila sababu za msingi,atakuwa amefanya kosa kisheria.

NUKUU:
Haki ya mshahara huimarishwa kwa utendaji na ufanisi wa kazi, si muda wa utumishi pekee.

WITO:
Omba ongezeko la mshahara kwa uwazi na ushahidi wa utendaji wako wa kazi.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

Licha ya kuweka mikakati bora ya kufanikisha malengo ya kibiashara, baadhi ya kampuni nchini bado zinapitia changamoto k...
03/05/2026

Licha ya kuweka mikakati bora ya kufanikisha malengo ya kibiashara, baadhi ya kampuni nchini bado zinapitia changamoto kubwa na kushindwa kutekeleza majukumu ipasavyo, hali inayopelekea kujikuta zikijiendesha kwa hasara pamoja na kulimbikiza madeni wasiyoweza kuyalipa kwa wakatii.

Changamoto hizo husababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo kudorora kwa uchumi wa kampuni na migogoro endelevu ndani ya kampuni. Hali hii husababisha biashara kudorora na kupoteza uwezo wa kumudu ushindani wa soko, jambo linalopelekea kampuni kushindwa kufikia malengo yake makuu na kukumbwa na changamoto za kisheria. Hatimaye kampuni huona suluhisho la pekee ni kuiomba mahak**a kuifuta kampuni katika msingi wa haki na usawa.

Kisheria, sababu zinazoweza kupelekea kampuni kufutwa kwa msingi wa haki na usawa ni pamoja na pale ambapo lengo kuu la kampuni limefeli na imekuwa vigumu kwa kampuni kufanikisha lengo hilo; wakati ambapo hakuna tena uaminifu na mshik**ano miongoni mwa wanahisa kutokana na migogoro endelevu pamoja na kushindwa kwa kampuni kutimiza malengo yake ya msingi; na pale ambapo migogoro ya wanahisa imekuwa ya kudumu na imeshindikana kusuluhishwa kwa njia zote za kawaida.

Aidha, mahak**a ikibaini kuwa kampuni imekosa vigezo vya msingi vinavyohalalisha kufutwa kwa msingi wa haki na usawa, haitaruhusu kampuni husika kufutwa. Hii ni kwa sababu hatua ya kufuta kampuni si ya kawaida bali ni suluhusho la mwisho, hivyo mahak**a hulinda maslahi ya wadau wote kwa kuhakikisha kuwa kufutwa kwa kampuni hakufanyiki bila sababu za msingi.

Kwa kufanya hivyo, mahak**a huzuia matumizi mabaya ya mchakato wa kisheria, inalinda wanahisa wachache dhidi ya maamuzi ya kiholela, na kuhakikisha kuwa kampuni inaendelea kutafuta njia mbadala za kutatua migogoro kabla ya kufutwa kabisa.

NUKUU;
Mahak**a hufuta kampuni pale ambapo kuendelea kwake hakutakuwa na manufaa kwa wadau, na si kwa matakwa ya mtu binafsi.

WITO:
Maamuzi ya kufutwa kampuni hayafanywi kwa matakwa binafsi ya mwanahisa mmoja, bali kwa msingi wa haki na usawa unaolinda maslahi ya wote.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753.

Imeandaliwa Hussein Mkuta.

Katika maisha ya ndoa, kumekuwepo na mkanganyiko au uelewa mdogo kati ya mali binafsi na za pamoja, hali ambayo imezalis...
10/04/2026

Katika maisha ya ndoa, kumekuwepo na mkanganyiko au uelewa mdogo kati ya mali binafsi na za pamoja, hali ambayo imezalisha utata wa umiliki na mgongano wa kimaslahi kwa baadhi ya wanandoa. Mkanganyiko huu umetokana au umesababishwa na uchangiaji katika upatikanaji wa mali, jambo linalopelekea kila mwanandoa kujimilikisha mali fulani dhidi ya mwenzake, huku kila mmoja akidai anahusika na umiliki. Hali inayoibua hoja ya msingi: je, ujimilikishaji wa mali za ndoa kiholela kati ya wanandoa unaweza kuifanya ndoa kuepuka migogoro ya umiliki na kimaslahi?

Kisheria, hakuna uhalali kwa wanandoa kujimilikisha mali za ndoa kiholela bila kufuata misingi na taratibu za kisheria k**a sheria ilivyobainisha, kwa kuwa uhalali wa upatikanaji wa mali za ndoa unatambuliwa kwa mchango wa pamoja wa wanandoa wote wawili, unaolindwa kwa misingi ya haki na usawa, na si kwa majina pekee yanayoonekana katika hati miliki.

Hata hivyo, ndoa kuingia kwenye migogoro ya umiliki na kimaslahi ni suala lisiloepukika pale wanandoa wanapojimilikisha mali za ndoa kiholela, wakidhani wanastahili umiliki na maslahi makubwa kuliko wenza wao, bila kutambua mchango wa wenza wao iwe ni mali, pesa, au nguvu vimehusika katika upatikanaji wa mali hizo.

Aidha, kuna baadhi ya wanandoa hutambua mchango mkubwa wa wenza wao katika upatikanaji wa mali, lakini hudai umiliki wao pekee, na kuwatenga wenza wao bila chochote baada ya ndoa zao kuvunjika. Hali hii husababisha migogoro ya umiliki na maslahi kuwa jambo lisiloepukika.

Zaidi ya hayo, mali za ndoa hujumuisha mali za pamoja ambazo zilizopatikana kwa juhudi za pamoja za wanandoa wakati wa ndoa, mali zilizoboreshwa kwa mchango wa wote wawili, pamoja na mali ambazo kisheria zinatambuliwa kuwa sehemu ya maisha ya ndoa.

NUKUU:
Mali za ndoa ni uruthi wa mchango wa pamoja, unaolindwa kwa misingi ya haki na usawa.

WITO:
Heshimu mchango wa mwenzako, mali za ndoa ni usawa, si jina pekee.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

09/04/2026

Je, wadhamini wawilii ndiyo ngao ya kisheria ya kulinda Uadilifu kwenye Mirathi? 📖 🇹🇿

Katika taratibu za mirathi, msingi wa haki na uwazi ni jambo muhimu la kuhakikisha kuwa watu wote wenye maslahi halali n...
05/04/2026

Katika taratibu za mirathi, msingi wa haki na uwazi ni jambo muhimu la kuhakikisha kuwa watu wote wenye maslahi halali na mirathi husika wanashirikishwa kikamilifu. Ushirikishwaji huu unahusisha warithi, wadai, na mtu yeyote aliye na mchango wa moja kwa moja katika mali ya marehemu. Kutoshirikishwa kunaleta dosari kubwa ya kisheria kwa sababu mirathi si mali ya msimamizi, bali ni mali inayohusu familia na watu wenye maslahi nayo.

Kisheria, kutoshirikishwa kunavunja haki ya kikatiba ya kusikilizwa. Mahak**a inatambua kuwa kila mwenye maslahi na mirathi husika ana nafasi ya kutoa hoja zake kabla ya barua za usimamizi wa mirathi kutolewa. Ikiwa taratibu za mirathi zitaendelea bila ushirikishwaji, matokeo yake ni mgawanyo usio halali wa mali na kuibua migogoro ya kifamilia. Hivyo, ushirikishwaji si hiari bali ni wajibu wa kisheria.

Zaidi ya hayo, ushirikishwaji unaleta uwiano kati ya taratibu za kisheria na uhalisia wa kifamilia. Unaposhirikishwa, unazuia dhuluma na unalinda heshima ya marehemu kwa kuhakikisha mali zake zinagawanywa kwa haki. Mahak**a haikubali hoja ya kutoshirikishwa, mara nyingi huamuru uchunguzi wa kina juu ya kutoshirikishwa kwa walalamikaji hasa wale wenye maslahi na mirathi husika, jambo linaloongeza imani ya wananchi katika mfumo wa haki.

NUKUU:
Haki ya kusikilizwa ni msingi wa uadilifu katika mirathi; bila ushirikishwaji, mirathi hugeuka dhuluma badala ya urithi.

WITO:
Watu wenye maslahi katika mirathi hakikisheni mnadai na kuitendea haki; haki yenu ya kushirikishwa, ili kulinda mali na heshima za familia zenu.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

Katika mfumo wa mirathi nchini, suala la wadhamini wawili limekuwa sharti la msingi kwa mirathi isiyo na wosia. Wadhamin...
01/04/2026

Katika mfumo wa mirathi nchini, suala la wadhamini wawili limekuwa sharti la msingi kwa mirathi isiyo na wosia. Wadhamini hao huchukua jukumu la kumdhamini msimamizi wa mirathi ili kuhakikisha mali za marehemu zinasimamiwa kwa uadilifu na kwa mujibu wa sheria. Mahak**a kuhitaji uthibitisho wa dhamana ya wadhamini wawili wenye kuaminika kwenye mirathi isiyo na wosia, imelenga kulinda maslahi ya warithi na wadai dhidi ya udanganyifu na kuzuia matumizi mabaya ya mali na migogoro ya kifamilia.

Kwa upande wa mirathi yenye wosia, sharti la wadhamini wawili linaweza kupunguzwa au kuondolewa kulingana na mazingira. Ikiwa marehemu alimteua msimamizi wa mirathi kupitia wosia wake, mahak**a huona kuwa uteuzi huo ni wa kutosha pale itakapojiridhisha. Hata hivyo, iwapo kuna mashaka kuhusu uadilifu wa msimamizi au mgongano wa maslahi, mahak**a bado inaweza kuhitaji wadhamini wawili kwenye mirathi hiyo ili kulinda haki za warithi na wadai. Hii inaonyesha kuwa sharti la wazamini wawili ni chombo cha kulinda uhalali wa mchakato mzima wa mirathi.

Aidha, sharti hili limeongezwa ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa mirathi. Wadhamini wawili wanakuwa k**a ngao ya kisheria, wakihakikisha kuwa msimamizi hatumii mali vibaya, na iwapo atafanya hivyo, wadhamini wanaweza kuwajibika kisheria kwa kile alichotenda msimamizi. Hii inaleta uwiano kati ya uhuru wa msimamizi na ulinzi wa maslahi ya warithi na wadai. Kwa mantiki hiyo, sharti la wadhamini linaongeza nidhamu na kuondoa mianya ya udanganyifu katika taratibu za mirathi.

NUKUU:
Wadhamini wawili ni ngao ya uadilifu katika mirathi

WITO:
Chagueni wadhamini waaminifu na wenye uadilifu ili kulinda mali na heshima ya familia.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

Kwa hakika, maisha ya mahusiano ni kizungumkuti. Baadhi ya wanawake hulazimishwa kutoa ujauzito na wenza wao ili kukwepa...
28/03/2026

Kwa hakika, maisha ya mahusiano ni kizungumkuti. Baadhi ya wanawake hulazimishwa kutoa ujauzito na wenza wao ili kukwepa jukumu la malezi. Wanawake hao, hupinga maamuzi hayo, huamua kulea ujauzito hadi hujifungua bila msaada wowote wa wenza wao. Changamoto huibuka baada ya kujifungua, pale wenza wao wanapodai watoto waliowakataa awali kwa nguvu na vitisho. Hali inayowaacha wanawake katika sintofahamu, wakijiuliza: je, ni haki kisheria kwa mwanaume kudai mtoto baada ya kutaka mimba itolewe?

Kisheria, ni kosa la jinai mwanaume kumlazimisha au kumtaka mwanamke atoe mimba bila sababu halali za kitabibu. Hata hivyo, mara mtoto anapozaliwa, mwanaume ana haki ya kudai mtoto wake kisheria hata k**a awali alitaka mimba itolewe. Haki hii hutokana na wajibu wa lazima na wa kisheria wa wazazi wote wawili kumlea na kumtunza mtoto bila kujali mazingira ya ujauzito. Pamoja na hayo, baba hapaswi kutumia haki hii vibaya au kwa mabavu, anapaswa kufuata taratibu za kisheria.

Aidha, baba anahitajika kutimiza wajibu wake kisheria kwa heshima na uaminifu. Pia ni wajibu wake kuhakikisha mtoto anaishi chini ya uangalizi wa mama na katika mazingira bora ya kimalezi. Zaidi ya hayo, ili kumuandalia mtoto mustakabari mzuri wa maisha yake ya baadae, wazazi wanapaswa kumlinda dhidi ya migogoro ya kifamilia. Mtoto anapokuwa karibu na migogoro ya wazazi hupata athari hasi zinazoweza kuharibu dira ya maisha yake, kuathiri masomo na kudhoofisha malezi yake kwa ujumla.

NUKUU:
Haki ya mtoto ni kipaumbele, migogoro ya wazazi si urithi wake.

WITO:
Wazazi, timizeni wajibu wenu kwa heshima na uaminifu; mlindeni mtoto dhidi ya migogoro, ili apate mustakabali bora.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

Katika maisha ya ndoa, baadhi ya wanawake huolewa kwa ahadi tu kwamba mahari yao italipwa baada ya ndoa. Changamoto kubw...
26/03/2026

Katika maisha ya ndoa, baadhi ya wanawake huolewa kwa ahadi tu kwamba mahari yao italipwa baada ya ndoa. Changamoto kubwa ni kwamba ahadi hizo hubaki hewani bila utekelezaji. Wanawake hujikuta wakibeba mzigo wa ndoa isiyo na msingi thabiti wa haki, huku wakikosa uthibitisho wa kisheria wa mahari yao. Hatimaye, migogoro inapoibuka, wanawake huibua suala la mahari k**a hoja ya kuvunja ndoa, wakidai kuwa malipo ya mahari yao ndiyo talaka yenyewe.

Kisheria, mahari si talaka. Mwanamke hana mamlaka ya kumtaliki mwanaume, bali katika dini ya Kiislam anaweza kuomba kuachwa kwa kurudisha mahari au mali fulani k**a fidia. Talaka hiyo hutegemea makubaliano ya maridhiano ya pande zote mbili na mara nyingi husababishwa na chuki ya mke kwa mume. Hata hivyo, ili talaka hiyo iwe halali kisheria nchini, ni lazima ithibitishwe kwa amri ya mahak**a.

Aidha, mara nyingi chanzo cha talaka huwa ni migogoro inayoibuka kati ya wanandoa, na si ahadi ya mahari isiyotekelezwa pekee. Wanaume wanaoahidi kulipa mahari baada ya ndoa ni lazima wazitekeleze ahadi hizo kwa uaminifu, kwani ni deni la heshima lisiloepukika kwao. Wanandoa pia wanapaswa kuhakikisha wanasuluhisha migogoro yao kwa hekima na maridhiano, kwa kuwa migogoro hiyo huacha athari hasi kwa watoto.

Watoto hukua katika mazingira yenye ukosefu wa utulivu, jambo linaloweza kuathiri malezi yao, masomo na mustakabari wao wa kimaisha. Kisheria, wajibu wa malezi na matunzo unabaki kwa wazazi wote wawili, hivyo ni muhimu kusimamia haki na majukumu ya kifamilia ili kulinda ustawi wa watoto na kudumisha heshima ya ndoa.

NUKUU:
Ndoa yenye heshima hujengwa kwa uaminifu na majukumu ya pamoja.

WITO:
Simamieni haki zenu, suluhisheni migogoro yenu, na lindeni mustakabali wa maisha ya watoto wenu.

Kutojua sheria si sababu ya kushindwa kutumia haki zako. Kwa maelezo zaidi, wasiliana nami kupitia 0654819753 kwa WhatsApp au simu.

Imeandaliwa na Hussein Mkuta.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255776135249

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when IJUE Sheria upate haki yako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to IJUE Sheria upate haki yako:

Share

Category