Ijue Sheria Na Haki Zako

Ijue Sheria Na Haki Zako Msaada Wa Kisheria

JE ZUIO  LA  MAHAKAMA  NI NINI NA KATIKA   MATUKIO   GANI  UNAWEZA  KUOMBA  ZUIO?1.ZUIO  LA  MAHAKAMA  NI NINI.Ni  amri ...
10/03/2025

JE ZUIO LA MAHAKAMA NI NINI NA KATIKA MATUKIO GANI UNAWEZA KUOMBA ZUIO?

1.ZUIO LA MAHAKAMA NI NINI.
Ni amri inayotolewa na mahak**a kumzuia mtu kutofanya jambo fulani kwa muda. . Aidha yeyote ana haki ya kuomba amri hii ikiwa anaona kuna jambo fulani linafanyika na ikiwa litaendelea kufanyika basi litaharibu au kupoteza kabisa kitu fulani.
Kwahiyo zuio ni amri inayobeba maagizo maalum kwa mtu au watu maalum kuwaamrisha kutoendelea na kitu fulani k**a tulivyoona hapo juu.Sheria ya Mwenendo wa Madai, Sura ya 33 na Sheria nyingine mtambuka zimeongelea kuhusu zuio.

2. KATIKA MATUKIO GANI UNAWEZA KUOMBA ZUIO.
( a ) Kwa mfano, umeshindwa kulipa mkopo na tayari una taarifa kuwa benki au taasisi yoyote ya fedha inataka kwenda kuuza na unahisi kuna pahala hapaendi sawa katika mikataba yenu.
Basi unaomba zuio ili hiyo mali yako uliyoweka rehani isiuzwe mpaka hapo hilo eneo ambalo mmeshindwa kuelewana litakapopatiwa majibu.

( b ) Kwa mfano, umemuuzia mtu gari, pikipiki, au mashine yoyote. Mtu huyo hajalipa kiasi cha pesa iliyobaki k**a mlivyokubaliana. Lakini anaendelea kutumia kifaa hicho. Unaweza kuomba kumzuia kuendelea kutumia mpaka atakapolipa kiasi kilichobaki ili asiendelee kuharibu au kuzeesha kifaa hicho.

( c ) Kwa mfano, we ni mpangaji katika nyumba ya kuishi au biashara. Mwenye nyumba,eneo anataka kukutoa kwenye pango hilo bila kufuata utaratibu au kwa kukiuka baadhi ya makubaliano kwenye mkataba wenu. Unaweza kuomba zuio asiendelee kukutoa.

Pia mazingira mengine yoyote ambayo unahisi kuna kitu, jambo linataka kuharibiwa au kuingiliwa, kuuzwa, kupotezwa,kufichwa kinyume na utaratibu unaweza kuomba zuio hilo.

3. SHARTI KUU .

Ili uweze kuomba zuio ni lazima pia kuwepo na shauri la msingi. Kwa maana utafungua shauri la msingi kulalamikia jambo fulani halafu utaomba zuio ndani ya shauri hilo. Kwa mfano unafungua shauri kulalamikia mwenye nyumba kusitisha mkataba wa pango bila kufuata utaratibu.

Hilo ni shauri kuu. Halafu ndani mwake unafungua shauri dogo la kuomba zuio ili asikuondoe katika nyumba mpaka kwanza shauri kuu la kukiuka utaratibu litatuliwe.

Kwahiyo ni sharti kuwapo shauri kuu ukilalamikia jambo fulani halafu ndani mwake ndio uombe zuio.

4. UMUHIMU WA ZUIO.

( a ) Linasaidia mali yako kutouzwa au kutoondolewa kwenye nyumba k**a mgogoro unahusu nyumba.

( b ) Linalinda mali yako isiharibiwe ,isifichwe, isihamishwe,isiingiliwe kwa namna yoyote ile k**a ipo katika mazingira hayo.

( c ) Linakupa nafasi ya kutafakari na kujipanga ikiwa upo katika presha ya kukimbizana na jambo ama mgogoro.

( d ) Linatoa mwanya wa mazungumzo kati ya mlalamkaji na mlalamikiwa.

5. WAPI UKAOMBE ZUIO.
Zuio linaombwa mahak**ani. Na linaweza kuombwa mahak**a yoyote katika shauri lolote. Linaweza kuombwa kwenye mashauri ya ndoa, mirathi, ardhi, biashara, mikataba, madai ya kawaida ya pesa au mali, makampuni n.k.
Na linaombwa katika mahak**a zote yaani ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi mahak**a kuu na ya rufaa pia. Lakini pia linaombwa kwenye mabaraza ya ardhi ya kata na wilaya.

6. KUKIUKA AMRI YA ZUIO.
Ikiwa utaomba zuio na kupata halafu aliyezuiwa akakiuka na kuendelea na kile alichozuiwa basi kosa linabadilika na kuwa la jinai. Inakuwa jinai ya kuingilia amri na shughuli za mahak**a. Ni kosa ambalo aliyekiuka amri hiyo akithibitika ni kweli kakiuka basi atatakiwa kwenda jela miezi sita ama vinginevyo.
Kinachotakiwa kwako ni kuripoti tu kuwa amri iliyotolewa sasa haitekelezwi na yule aliyeamrishwa kutekeleza. Utaripoti mahak**a hiyo hiyo iliyotoa zuio hilo.

Je? Unazifahamu Athari za Kisheria Kwa Uamuzi wa Kuingia Kwenye Mkataba wa Ajira ya KudumuLeo tunaangalia athari za kish...
30/10/2023

Je? Unazifahamu Athari za Kisheria Kwa Uamuzi wa Kuingia Kwenye Mkataba wa Ajira ya Kudumu

Leo tunaangalia athari za kisheria endapo mwajiri atafanya uamuzi wa kuingia mahusiano ya kiajira na mwajiriwa katika mkataba wa kudumu. Karibu tujifunze.

Aina za Mkataba

Mkataba wa ajira na mwajiriwa utakuwa wa aina zifuatazo;

1. mkataba usio wa muda maalum;
2. mkataba wa muda maalum kwa kada ya wataalam na viongozi
3. mkataba wa kazi maalum

Ufafanuzi

Mkataba usio wa muda maalum – aina hii ya mkataba inajulikana k**a mkataba wa kudumu. Mkataba huu unaanza pale mwajiriwa anaanza kazi na unaisha pale mwajiriwa anapokuwa amefikisha umri wa kustaafu kwa hiyari au lazima kwa mujibu wa sheria. Umri wa kustaafu ni miaka 55 kwa hiyari au 60 kwa lazima.

Athari za kisheria katika mahusiano ya mkataba wa kudumu

Mkataba huu wa ajira unaendelea tangu mwajiriwa alipoanza kazi mpaka atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiyari au kwa lazima.
Endapo mwajiri anakusudia kusitisha mkataba huu kabla ya umri wa kustaafu ni lazima:

1. Awe na sababu halali na za msingi
2. Afuate utaratibu wa haki katika kusitisha mkataba huu

Sababu za msingi na halali zinazoweza kusababisha mkataba wa kudumu kusitishwa ni
Utovu wa nidhamu:

1. Zoezi la kupunguza wafanyakazi (retrenchment)
2. Uwezo mdogo wa utendaji wa mwajiriwa
3. Sababu za kiafya k**a ugonjwa au kuumia kazini

Hivyo Kwa sababu yoyote ile mwajiri anayotaka kuitumia kusitisha mkataba wa kudumu ni lazima afuate utaratibu uliowekwa kisheria kuhusiana na sababu husika. Mfano anataka kusitisha mkataba kutokana na utovu wa nidhamu ni lazima afuate utaratibu husika kabla ya kusitisha ajira hiyo au kusitisha kutokana na uwezo mdogo basi upo utaratibu.

Endapo mwajiri atashindwa kufuata utaratibu, basi mwajiriwa ana haki ya kukata rufaa mbele ya Tume au Mahak**a Kuu kupinga uamuzi wa mwajiri.

Endapo Tume au Mahak**a itaona hapakuwa na sababu halali na za msingi pamoja na utaratibu kutofuatwa basi inaweza kuamuru mwajiriwa husika KURUDISHWA KAZINI au kulipwa FIDIA kiasi kisichopungua mishahara ya miezi 12.

Ieleweke Tume au Mahak**a inayo mamlaka ya kutoa mishahara zaidi ya miezi 12 inategemea na namna shauri lilivyo mbele yake na ushahidi uliotolewa.

Kwa upande mwengine, endapo mwajiriwa anakusudia kusitisha ajira yake na mwajiri wake ambapo ana mkataba wa kudumu anaweza kufanya hivyo endapo;
1. Atakuwa ametimiza umri wa kustaafu kwa hiyari yaani miaka 55 au umri wa kustaafu kwa lazima miaka 60
2. Ataamua kujiuzulu kazi kwa kutoa taarifa ya maandishi.

Ndugu msomaji tunaona jinsi Sheria inavyowabana waajiri katika mazingira ya kuingia makubaliano ya kudumu kiasi kinachosababisha kufuata taratibu nyingi na kuwa na sababu za msingi, wakati kwa upande mwengine mwajiriwa habanwi sana na masharti ya ajira katika mkataba huu wa kudumu.

Hitimisho

Endapo mwajiri anaamua kufanya uamuzi wa kuingia makubaliano ya mkataba wa kudumu ni lazima ajue masharti yanayoambatana na mkataba husika.

Wapo waajiri wengi wanawekeza sana kwa wafanyakazi kwa kuwapeleka mafunzo ili kuongeza ufanisi katika kazi, lakini baada ya kupata ujuzi na utaalam ambao umegharamiwa na mwajiri wafanyakazi hao hugeuka na kwenda mahali pengine kutafuta maslahi bora zaidi. Hivyo ni muhimu kuhakikisha ndani ya mikataba hiyo ya ajira vipo vipengele vitakavyolinda maslahi ya mwajiri pia.

JE? NI KWELI CHIZI HAWEZI KUHUKUMIWA KWA KOSA LA JINAI?Leo tunakwenda  kuangalia Utetezi wa Kisheria unaotokana na Ugonj...
28/10/2023

JE? NI KWELI CHIZI HAWEZI KUHUKUMIWA KWA KOSA LA JINAI?

Leo tunakwenda kuangalia Utetezi wa Kisheria unaotokana na Ugonjwa wa Akili.

Dhana ya Utimamu wa Akili kwa watu wote

Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 imebainisha kuwa ipo dhana inayokanushika kwamba wato wote wana akili timamu kwa wakati wote. Dhana hii inabainishwa katika kifungu cha 12 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ikisema

"Kila mtu atachukuliwa kuwa na akili timamu, na atachukuliwa kuwa na akili timamu wakati wote mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo"

Dhana hii ya kisheria ni muhimu sana katika kusaidia watu wengi kujitetea kuwa wakati anatenda kosa hakuwa vizuri kimawazo au alikuwa amechanganyikiwa. Hivyo endapo kosa litafanyika mahali na mtuhumiwa kuk**atwa atachukuliwa kuwa alikuwa na akili timamu wakati ule wa kutenda kosa alilotenda.

Utetezi wa Kisheria kwa Ugonjwa wa Akili

Sheria inatambua mazingira ambayo mtu anaweza kutenda jambo fulani ambalo kisheria ni kosa lakini mazingira ya utendaji wa kosa hilo alikuwa ameathiriwa na ugonjwa ambao unaathiri akili yake katika kufikiri. Hapa ni lazima ithibitike mbele ya mahak**a kuwa mtuhumiwa alikuwa na tatizo la kiakili wakati anatenda kosa husika.

Kifungu cha 13 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kinaeleza

13.-(1) Mtu hatawajibika kwa kutenda kosa la kijinai kwa kitendo au kuacha kutenda iwapo wakati wa kutenda kitendo hicho au kuacha kutenda alikuwa katika hali ya ugonjwa wowote unaoathiri akili yake ambapo:-

1. hawezi kujua kitu anachokitenda;

2. hawezi kutambua kwamba hapaswi kutenda au kufanya jambo husika; au

3. hana uwezo wa kuzuia kitendo au kuacha kutenda.

Ufafanuzi
Ugonjwa wa akili kwa mtuhumiwa unaweza kutumiwa k**a utetezi wa kisheria dhidi ya mash*taka ya kijinai k**a ilivyobainishwa katika kifungu cha 13 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Ili mtuhumiwa aweze kutumia utetezi huo na kufanikiwa dhidi ya mash*taka husika ni lazima ugonjwa huo uweze kudhibitisha mojawapo wa vigezo vilivyowekwa kisheria;

Kwamba wakati wa kutenda kosa husika mtuhumiwa hakuwa na uwezo katika akili yake kujua kitu anachotenda.
Ni lazima idhibitike mbele ya mahak**a kuwa mtuhumiwa alikuwa ana ugonjwa ambao umeathiri akili yake kiasi cha kushindwa kujua kitendo gani alitenda. Tunaona mifano mingi barabarani ambapo wapo wagonjwa wa akili na wanaweza kutenda vitendo vingi vya uhalifu ikiwepo kupiga watu au kuharibu mali n.k. mtu wa aina hii endapo atak**atwa na kufikishwa mahak**ani kwa makosa yale ikadhibitika katika maneno yake na hasa vipimo vya madaktari juu ya uwezo wa akili yake kuwa hakuwa anajua kile anachofanya basi anaweza kuachiliwa kutokana na utetezi wa ugonjwa wa akili.

Kwamba wakati wa kutenda kosa husika mtuhumiwa hakuwa na uwezo wa kutambua kuwa kile anachotenda ni kosa.
Ugonjwa wa akili pia unaweza kumwathiri mtuhumiwa kwa kiwango cha kupoteza au kutokuwa na uwezo wa kujua kile anachotenda ni kosa kisheria. Mara kadhaa tumesikia juu ya watu wenye ugonjwa wa akili akibaka mtu hadharani, au kufanya kitendo ambacho kwa kawaida si rahisi mtu aliye timamu anaweza kufanya. Hii ni kwa sababu ugonjwa huo unakuwa umeathiri uwezo wake wa kutambua kile anachofanya ni kosa kisheria.

Kwamba wakati wa kutenda kosa husika mtuhumiwa alikosa uwezo katika akili yake kujizuia kutenda kitendo husika.
Ugonjwa wa akili unaweza kuwa sababu ya utetezi wa kisheria ambapo umeathiri uwezo wa mtuhumiwa kushindwa kujizuia kutenda jambo fulani ambalo ni kosa kisheria. Sheria inaweza kuwa imekataza mathalani watu kutembea bila nguo, lakini kutokana na ugonjwa wa akili mtu anaweza kujikuta anatembea pasipo kuvaa nguo, hivyo mtuhumiwa husika anakuwa ameshindwa kujizuia kufanya kitendo ambacho kimekatazwa na sheria.

Hitimisho

Leo tumeangalia juu ya utetezi wa kisheria kutokana na ugonjwa wa akili ambapo mtuhumiwa anaweza kuutumia endapo itadhibitika kuwa wakati anatenda kosa alikuwa katika hali ya ugonjwa huo. Ifahamike kuwa, kabla ya mahak**a kuukubali utetezi huu wa ugonjwa wa akili ni lazima mtuhumiwa akapimwe na wataalam wa magonjwa ya akili nao wapate nafasi ya kutoa maoni yao kuhusiana na uwezo wa mtuhumiwa wakati wa kutenda kosa. Pia ni muhimu kufahamu kuwa wapo watu wana athiriwa na ugonjwa wa akili katika vipindi fulani na wapo wengine ni wagonjwa wa moja kwa moja.

Ndio maana ni muhimu kwetu k**a wananchi kufuata utaratibu wa kisheria wakati tunasughulikia masuala ya uhalifu kwani tunaweza kuadhibu mtu kutokana na makosa aliyofanya pasipo kujua kuwa wakati mtu huyo anatenda makosa hayo alikuwa katika hali gani ya kiafya kwenye akili yake. Ni mchakato wa kimahak**a pekee unaoweza kutusaidia kufahamu hasa kiini cha tatizo lililosababishwa na mtuhumiwa endapo lilisabashwa akiwa na akili timamu au la.

UVUNJAJI WA MKATABA NA MATOKEO YAKEKuvunja mkataba ni NiniNi ile hali ya kutotekeleza matendo au majukumu yale mliokubal...
25/10/2023

UVUNJAJI WA MKATABA NA MATOKEO YAKE

Kuvunja mkataba ni Nini

Ni ile hali ya kutotekeleza matendo au majukumu yale mliokubaliana ndani ya
mkataba husika kwa makusudi, haijalishi mkataba huo ni wa makubaliano ya
maandishi au wa makubaliano ya mazungumzo tu, k**a hujatekeleza wajibu wako
na majukumu yaliyooanishwa katika mkataba husika kwa makusudi hapo utakuwa
umevunja mkataba.

Mfano: mkataba wenu ni wa makubaliano ya maandishi, na unahusisha kuuziana
nyumba kwa kiasi cha fulani, ila mlikubaliana mnunuzi akulipe pesa zote ndani ya
miez mitatu, k**a ikitokea mnunuzi kashindwa kukulipa pesa ndani ya miezi mitatu
k**a masharti yanavyosema kwenye mkataba atakuwa amevunja mkataba. Hiyo
ndio maana ya Kuvunja mkataba.

TAMBUA KUWA

Katikaa uvunjaji wa mkataba au mikataba, ikiwa k**a mkataba unaeleza k**a
ukikeuka hata sharti moja tu utakuwa umevunja mkataba basi hapo moja kwa moja
umevunja mkataba husika,au k**a hukivunja vigezo utakuwa umevunja mkataba
basi utakuwa umevunja mkataba.

JINSI YA KUUTEKELEZA MKATABA ULIOVUNJWA.

Siku zote, kwenye mikataba husika yule anaekeuka masharti au Kuvunja mkataba
ndiye anaestahili kumlipa mwenzake ambae kwa namna moja au nyingine kaingia
kwenye hasara kwa mkataba kuvunjikaa.
K**a sheria ya mikataba iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018, inavyoelezea
katika kifungu cha 73 kifungu kidogo cha Kwanza.

Na ikaendelea kusema kwenye kifungu cha 73 kifungu kidogo cha pili cha sheria
hiyo hiyo ya mikataba kuwa, hasara ambayo mtu kaipata kutokana na kuvunjikaa
kwa mkataba atalipwa iwapo hasara hiyo aliyoipata sio ya siri.

Na kifungu cha 75 cha sheria ya mikataba iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018,
imeelezea kuwa kimfano mtu ameubatilisha mkataba wa halali kwa makusudi kwa
kutotekeleza majukumu ya kimkataba anatakiwa kulipa fidia kwa madhara
aliyomsababishia mwenzake.

Na k**a mkataba unaelezea k**a mmoja wao atavunja mkataba atatakiwa kulipa
kiasi kadhaa au kitu chochote k**a mkataba unavyoelekeza, basi atatakiwa kulipa
kiasi hicho, k**a kifungu cha 74 kifungu kidogo cha nne cha sheria ya mikataba
inavyoelezea.

MUDA WA KUFUNGUA KESI YA UVUNJAJI WA MKATABA

Muda wa kufungua kesi ya mtu aliyevunja mkataba unaanza palepale mkataba
ulipovunjika, na sheria inaelezea uvunjaji wa mkataba mwisho wa kufungua kesi
yake ni miaka 6, ikipita hapo mtu hana mamlaka au uwezo wa kufungua kesi ya
uvunjaji wa mkataba.

Ila kuna hali inatokea humfanya mtu kushindwa kufungua kesi mpunakwisha
ukakwisha, mtu huyu anaweza kupewa nafasi na waziri mwenye mamlaka nusu ya
muda wa kufungua kesi za uvunjaji wa mikataba, lakin k**a anasababu maalumu
k**a ugonjwa, K**a ilivyoelezea katika kifungu cha 11 kwenye sheria ya kikomo (
law of limited Act).

ADHABU ZA UVUNJAJI WA MIKATABA.

Katikaa uvunjaji wa mkataba kuna adhabu nyingi tu ambazo mahak**a zaweza
kuzitoa kwa yule aliyevunja mkataba, miongoni mwa hizo adhabu ni k**a
zifuatazo:

1. Specific performance ( fanya k**a mlivyokubaliana).

Hii ni adhabu ambayo inatolewa k**a unaujuzi wa kitu fulani, kimfano mliingia
kwenye mkataba wa kujenga nyumba wewe ukiwa fundi na kulipwa pesa zako zote,
lakin ukavunja mkataba, mahak**a inaweza kukuamuru kwa kukupa adhabu ya
kuifanya kazi hiyo kwa kuimalizia nyumba ambayo ulioiacha ilhali kuwa kulipwa
tayari umeshalipwa.

2. Kulipwa vile unavyostahili

Hii inatokana k**a umeingia mkataba halafu ukafanya kazi, ila haukumalizia, na
kuuvunja mkataba, mahak**a itaamuru wewe kulipwa kwa kile ulichokifanya

25/06/2023

NAMNA DHAMANA YA POLISI NA MAHAKAMANI ZINAVYOTOLEWA

CC

Je Ni Sababu Zipi Zinazofanya Mrithi Halali kunyimwa Haki Yake Ya Kurithi?Yapo mazingira ambayo yanaweza kusababisha mri...
02/06/2023

Je Ni Sababu Zipi Zinazofanya Mrithi Halali kunyimwa Haki Yake Ya Kurithi?

Yapo mazingira ambayo yanaweza kusababisha mrithi halali kunyimwa haki ya urithi na marehemu. Vipo vitu au matukio yanayoweza kusababisha mwosia kumwondoa mrithi wake katika urithi hata k**a ni mtoto au mtu anayepaswa kumrithi kwa mujibu wa sheria za kimila au taratibu nyingine zozote.



Mazingira yanayosababisha kuondolewa kwa haki ya urithi

Katika mfumo wa mirathi kufuata mila, sheria za kimila na taratibu za mirathi zinaeleza juu ya mwosia kuwa na haki ya kumwondoa mrithi katika urithi wake. Sababu hizo ni k**a ifuatavyo;

1. Endapo mrithi ametenda vitendo vya zinaa na mke wa mwosia
K**a tunavyofahamu mfumo wa familia za kimila zinaweza kuhusisha ndoa ya wake wengi. Hivyo endapo mtoto wa mwosia akalala na mama yake mzazi au mama mdogo yaani mke mdogo wa baba yake basi baba ana haki ya kumwondoa mtoto husika katika haki ya kumrithi. Kitendo hiki ni cha kuchukiza na hakifai na mara nyingi adhabu yake ni kutengwa na familia au ukoo. Katika mila za kiafrika mahusiano ya karibu yaani ya ndugu au mtoto kwa mzazi hayakubaliki kabisa hivyo mtu anaweza kupoteza haki yake ya urithi k**a adhabu.

2. Endapo mrithi amefanya jaribio la kumuua

mwosia au kumpiga na kumsababishia majeraha makubwa.
Tumeshuhudia mara kwa mara vitendo vya watoto ama kutishia uhai wa wazazi wao au kuchukua hatua kabisa na kuwadhuru au kuwaua kwa sababu mbalimbali ikiwepo mali na masuala ya kishirikina. Sheria na taratibu za kimila zinaeleza kuwa endapo mrithi atachukua hatua za kumdhuru mwosia basi mwosia anayo haki ya kumwondoa mrithi husika katika haki ya kumrithi kutokana na vitendo vyake.

3. Endapo mrithi bila sababu ya msingi alishindwa kumuuguza mwosia au kumsaidia wakati wa njaa.

Yapo mazingira ambayo mwosia anaweza kuingia katika dhiki au ugonjwa na akahitaji msaada wa warithi wake. Endapo mrithi amekataa pasipo sababu za msingi kumhudumia mwosia wakati wa dhiki yake au ugonjwa wake basi mwosia anayo haki ya kimila kumwondoa muhusika kutoka katika wosia wake.

Utaratibu wa kumwondoa mrithi

Suala la kumwondoa mrithi katika haki ya kurithi kutoka kwa marehemu linatakiwa lifanywe na muhusika mwenyewe yaani mwosia. Mwosia akiwa na sababu kati ya hizo hapo anaweza kutoa wosia wake ikiwa kwa mdomo au maandishi juu ya sababu ya kumwondoa mrithi katika haki ya urithi.
Mrithi anayeondolewa haki ya kurithi anaweza kupewa nafasi ya kusikilizwa na familia au ukoo husika. Ikiwa mwosia bado yupo hai na tamko lake limetolewa la kumwondoa mrithi katika urithi, mrithi anaweza kuomba kusikilizwa na familia au kikao cha ukoo na kuwasilisha utetezi wake.
Endapo utetezi wake utakubalika na mwosia kuridhika au kupatanishwa basi tamko lile litabatilishwa, la endapo utetezi wake hautakubalika basi tamko la wosia ule litatekelezwa.

Je Ni Kweli Sheria Hairuhusu Mtoto Kushtakiwa Au Kuhukumiwa?Soma makala hii kujua ukweliSheria ya Kanuni ya Adhabu pamoj...
23/04/2023

Je Ni Kweli Sheria Hairuhusu Mtoto Kushtakiwa Au Kuhukumiwa?

Soma makala hii kujua ukweli

Sheria ya Kanuni ya Adhabu pamoja na kuainisha makosa mbali mbali imeainisha pia aina za utetezi ambapo mtuhumiwa anaweza kutumia kujitetea pale anaposh*takiwa mahak**ani. Mtuhumiwa kwenye makosa ya jinai ana haki ya kuleta hoja za utetezi ambazo zinaweza kumwondolea tuhuma zinazomkabili.

Hoja ya utetezi umri mdogo ni mojawapo wa sababu za kuweza kumsaidia mtuhumiwa kutotiwa hatiani kwa kosa analosh*takiwa nalo.

Katika makala ya Sheria Leo.36 tuliangalia mojawapo ya aina ya utetezi unaoitwa Dai la Haki kwa Uaminifu. Rejea makala hiyo upate kujifunza.

Maana ya Utetezi wa Kisheria kwa mujibu wa Umri

Huu ni aina ya utetezi unaohusiana na umri mdogo wa mtu anayetuhumiwa kutenda kosa la kijinai. Hatahivyo, utetezi huu hauwezi kutumika na watoto wote kwa kigezo cha kuwa chini ya miaka 18 k**a Sheria ya Mtoto ya 2009 inavyotoa tafsiri ya mtoto.

Kutokana na tafsiri ya mtoto kwenye Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inaeleza kuwa mtoto ni mtu aliye na umri chini ya miaka 18. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria ya Kanuni za Adhabu inaonesha kuwa si watoto wote wanaondolewa uwezekano wa kushtakiwa ikiwa wapo chini ya umri wa miaka 18.

Sheria ya Kanuni ya Adhabu imeweka mazingira ya mtoto anayeweza kutumia umri kuwa kigezo cha utetezi dhidi ya makosa au mash*taka ya kijinai katika mtazamo wa aina 3 k**a ifuatavyo;

Mtoto chini ya miaka 10 hawezi kutenda kosa la kijinai

Kifungu cha 15 (1) cha Kanuni ya Adhabu Sura 16 kinaeleza msingi na maana ya utetezi huu

Mtu mwenye umri chini ya miaka kumi anachukuliwa kuwa hawezi kuwajibika kijinai kwa kutenda au kutotenda kosa.

Sheria ya Kanuni ya Adhabu inaanisha kwamba mtu yeyote ambaye ana umri chini ya miaka 10 anachukuliwa hawezi kuwajibika kwa makosa ya kijinai. Hii ina maana ngazi ya msingi ya utetezi kwa makosa yanayofanywa na watoto wadogo ni kuangalia umri wao. Huwezi kumpeleka mahak**ani mtoto yeyote chini ya miaka 10 kush*takiwa kwa jambo lolote alilotenda au aliloacha kutenda.

Sheria ya makosa ya kijinai inachukulia umri huu kuwa mtoto hawezi kufahamu asili ya makosa au kujengeka fikra za kutenda kosa lolote la kijinai.

Mtoto chini ya miaka 12 anaweza kuwajibishwa ikidhibitika ana ufahamu juu ya makosa aliyotenda

Mtu mwenye umri wa chini ya miaka kumi na mbili hatawajibika na kosa lolote la kijinai kwa kutenda au kutotenda jambo, isipokuwa k**a itathibitishwa kwamba wakati wa kutenda au kuacha kutenda kitendo hicho alikuwa na uwezo wa kujua kwamba hapaswi kukitenda au kuacha kukitenda.

Sheria haimwajibishi kimash*taka mtoto mwenye umri chini ya miaka 12 endapo atatenda kosa au kutuhumiwa kwa kosa lolote. Hata hivyo dhana hii inakanushika endapo itadhibitika kuwa mtoto husika wakati anatenda kitendo cha kijinai alikuwa na ufahamu juu ya kile anachotenda kwamba ni kosa.

Mtoto wa kiume chini ya miaka 12 hawezi kutuhumiwa kwa makosa ya kujamiiana.

Mwanaume mwenye umri wa chini ya miaka kumi na mbili atachukuliwa kuwa hawezi kufanya tendo la ndoa.

Mtoto wa jinsia ya kiume chini ya miaka 12 hawezi kuwajibishwa kijinai kutokana na makosa ya kujamiiana. Sheria inamchukulia mtoto wa umri chini ya miaka 12 hawezi kuwafanya tendo la ndoa na mtu yeyote kutokana na umri wake kuwa mdogo.

Kwa kutazama utetezi huu wa kisheria ambao upo kwa ajili ya watoto na kupima hali halisi ya jamii zetu tunaweza kuona kuna utofauti mkubwa wa kile sheria inachoeleza na uhalisia wa jamii yetu.

Kwa siku za karibuni watoto wadogo hata wa umri chini ya miaka 10 wamehusika kwa sehemu kubwa katika kutekeleza matukio ya uhalifu hata makubwa sana ikuhusisha na mauaji. Tumeshuhudia mmomonyoko wa maadili na watoto wetu kuwa na uwezo mkubwa wa kutenda makosa na hasa wakiweza hata kudanganya kwa sehemu kubwa juu ya uhalisia wa maisha yao.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha kile sheria inachosema kuwa tofauti na uhalisia wa watoto wetu.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia; hii ni sababu kubwa sana ambayo watoto wadogo wameitumia kukuza fikra zao kuliko umri wao. Kwa sasa maendeleo katika kujifunza kupitia simu na television kwa watoto wanajifunza mambo mengi sana katika umri mdogo ikiwa ni mambo mazuri au mabaya.



Nafasi ya malezi kuwa finyu; wazazi wa sasa tunatumia muda mwingi sana katika kutafuta masuala ya kiuchumi kuhusiana na familia zetu kiasi cha kuacha uangalizi na malezi ya watoto chini ya walezi wa nyumbani yaani ‘house girls’. Kwa kuangalia mfumo wa maisha ya hawa walezi wa nyumbani tunajikuta watoto wetu wanakusa msingi mzuri wa kukua kimaadili kwani wanaowalea pia ni watoto wenzao na wanawalea kwa kufuata mkumbo wa maisha ya mjini.



Ongezeko la watoto wa wasio na makazi maalum; hawa jamii yetu imewapachika jina la ‘watoto wa mitaani’ ingawa hakuna mtaa unaozaa watoto bali wanazaliwa kutokana na baba na mama zao ambao kwa njia moja au nyingine wameacha kutimiza wajibu wa malezi. Tunakutana na watoto wadogo sana wakiwa barabarani wanaomba fedha. Katika mazingira haya ni wazi tabia za kijinai zinaweza kujijenga tangu wakiwa wadogo.

Hitimisho

Leo tumeangali utetezi kutokana na umri mdogo yaani chini ya miaka 12 ambapo mtoto anaonekana hawezi kutenda makosa ya kijinai. Hatahivyo mfumo wa kijamii kwa sasa unadhibitisha vinginevyo. Ni vyema sheria zikatazamwa upya na kuona namna bora ya kuweka mazingira ya watoto vizuri na hasa jukumu kubwa la kisheria linapaswa kuwa kwa wazazi endapo mtoto ataonekana katika umri mdogo anatenda matendo yanayoashiria jinai basi mzazi au mlezi awajibike katika vyombo vya kisheria. Hii itasaidia sana kutukumbusha wajibu wa kuwalea watoto kwenye maadili mema na kujiwekea akiba ya jamii ya baadae ya kulijenga taifa.

Ni rai yangu pia kwa wazazi na walezi hata na watu wengine katika umri wa utu uzima kuwalinda watoto kutokana na mitandao , vipindi vya televisheni na pia kujiepusha na kuwatendea makosa mbalimbali k**a kuwadhulumu utu wao, kuwaingilia na kufanya vitendo viovu dhidi yao kwani tunawajengea taswira mbaya sana katika mustakabali wa maisha yao ya baadae.

Mtoto aliyefanyiwa mambo ya ukatili katika maisha yake ya utoto ikiwa ni kupigwa, kunyanyaswa kwa sababu ya jinsia yake, kubakwa, kulawitiwa ni wazi mtazamo wake akiwa mkubwa utakuwa hivyo hivyo juu ya watoto wengine na atashiriki kutenda hayo hayo.

Umiliki Wa Ardhi Kwa Njia Ya UvamiziK**a tulivyowahi kuzungumza katika makala zilizopita kuwa uvamizi wa maeneo ni kinyu...
07/02/2023

Umiliki Wa Ardhi Kwa Njia Ya Uvamizi

K**a tulivyowahi kuzungumza katika makala zilizopita kuwa uvamizi wa maeneo ni kinyume cha sheria na ikibainika mvamizi anaweza kuchukuliwa hatua za kijinai pamoja za kimadai. Hatahivyo, sheria ya ardhi inatambua aina ya umiliki kwa njia ya uvamizi ambapo mvamizi anaweza kutambulika k**a mmiliki akikidhi baadhi ya vigezo ambavyo vimewekwa kisheria.

Leo tunakwenda kuangalia namna mvamizi anaweza kubadilika kuwa mmiliki halali katika eneo na mbinu ambazo zitamsaidia mmiliki halali kuhakikisha kuwa eneo lake halivamiwi na kusababisha umiliki wake kuhamishwa kwenda kwa mvamizi.

Tafsiri sahihi ya umiliki kwa njia ya uvamizi ni hali inayojitokeza kwa mvamizi wa eneo kuingia katika eneo na kufanya shughuli zake ikiwa za makazi au uzalishaji katika eneo pasipo ruhusa ya mmiliki halali na kuwepo hapo kwa kipindi kisichopungua miaka 12 pasipo kuingiliwa na mmiliki au wakala wake.

Kwa maneno mengine neno la umiliki kwa njia ya uvamizi linajulikana k**a ‘adverse possession’ kwa lugha ya kiingereza.

Utaratibu wa umiliki ardhi kwa njia ya Uvamizi

Katika utaratibu wa umiliki kwa njia ya uvamizi wa eneo yapo mazingira ambayo yanaweza kumsaidia mtu kuhalalisha umiliki wa maeneo husika.

Ufuatao ni utaratibu wa kupata ardhi kwa uvamizi eneo;-

1. Uwepo wa ardhi ambayo si milki ya mvamizi.

Ili umiliki kwa njia ya uvamizi uweze kupata uhalali jambo la msingi ni uwepo wa eneo ambalo halimilikiwi na mvamizi yaani ni milki ya mtu mwengine ambaye hawana uhusiano na mvamizi. Ardhi hii ni lazima iwe inamilikiwa tofauti na ile ambayo tulijadili katika makala iliyopita yaani ardhi ambayo ni pori halipo chini ya umiliki wa mtu au kikundi cha watu. Yapo maeneo kadhaa vijijini au katika miji yana umiliki wa watu lakini kwa taswira ni k**a yametelekezwa. Katika mazingira haya mvamizi anaweza kuingia kwenye eneo husika.

2. Mvamizi kuchukua udhibiti wa eneo

Hatua hii ya pili ni muhimu kwa ajili ya kujenga mazingira ya umiliki kwa njia ya uvamizi yaani mvamizi husika ambaye eneo hili si lake kuchukua hatamu za eneo kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji ikiwa ni kilimo au shughuli nyingine au kuweka makazi katika eneo husika. Mvamizi hawezi kupata uhalali mbele ya sheria endapo hajachukua hatua za kudhibiti eneo husika ambalo anataka ahesabiwe ni halali yake.

3. Mvamizi hapaswi kupata ruhusa au kibali

kutoka kwa mmiliki au wakala wake.
Mtu anayetaka kupata umiliki kwa njia ya uvamizi ni lazima asiwe na kibali au ruhusa kutoka kwa mmiliki au wakala wake. Watu wengi wanataka kuhesabiwa ni wamiliki kwa njia hii ya uvamizi lakini unakuta hapo awali walikabidhiwa eneo k**a walinzi au kuruhusiwa kufanya shughuli za uzalishaji au kuweka makazi na mmiliki au wakala wake. Sheria inatambua kuwa kitendo cha uvamizi hakihusiani na kupewa ruhusa au kibali na mmiliki.

4. Kuwepo katika eneo kwa muda usiopungua miaka 12

Mvamizi ni lazima aweze kudhibitisha kuwa yupo katika eneo husika la uvamizi kwa kipindi kisichopungua miaka 12 pasipo kuingiliwa au kuibuliwa mgogoro wa ardhi katika eneo hilo na mmiliki au mwakilishi wake. Mvamizi anapaswa adhibitishe uwepo wake katika eneo husika mfululizo katika kipindi kisichopungua miaka 12. Hii inatoa nafasi hata kwa jamii inayozunguka eneo husika kujua kuwa mvamizi husika ni mmiliki halali wa eneo hilo.

Ufafanuzi

Msingi wa sheria kuruhusu umiliki kupitia njia hii ya uvamizi wa muda mrefu ni kuondoa ile dhana ya watu kumiliki maeneo mengi pasipo kufanya shughuli zozote za maendeleo. Kumekuwa na tabia ya watu kumiliki maeneo mengi kwa lengo la kufanya biashara ya ardhi badala ya kuchukua hatua ya kuyaendeleza. Wengi wanamiliki maeneo na kuyatelekeza pasipo kufanya shughuli za uzalishaji. Kwa kuwa Serikali na jamii kwa ujumla inataka maendeleo ikiwepo na shughuli za uzalishaji uvamizi wa muda mrefu pasipo kuingiliwa na mmiliki au wakala wake unaweza kumpatia mvamizi haki ya umiliki kwani atakuwa na msingi wa kuendeleza eneo.

Hitimisho

Pamoja na kwamba njia hii ya umiliki kwa hali ya kawaida inaonekana k**a si halali lakini ni njia muhimu sana kuhakikisha ardhi haikai tupu pasipo kufanyiwa maendeleo ya msingi. Hii itasaidia pia kwa wamiliki kuchukua hatua madhubuti kutimiza masharti ambayo wamepewa ardhi husika ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi au kilimo au shughuli za viwanda wanapaswa kutimiza masharti hayo ndani ya muda husika. Ndio maana kwa sasa unasikia zipo hati za umiliki zinafutwa na Rais kutokana na wamiliki kutochukua hatua madhubuti kutekeleza shughuli zile ambazo wamepewa hati husika.

Nitoe rai kwa wamiliki wa maeneo kuhakikisha kila eneo wanalomiliki wanafanya shughuli ambazo zitaweza kuonesha maendeleo katika eneo na si kuyatelekeza kwa nia ya kutaka kuuza baaadae kwani kuna hatari ya kuvamiwa au kufutiwa hati za umiliki na mamlaka husika.

‘Pata ardhi, tumia ardhi kwa shughuli za maendeleo ya nchi’

02/12/2022

Je?, Una swali lolote kuhusu sheria mbalimbali au Haki, Uliza hapa nikujibu

NI UPI WAJIBU WA MWENYE NYUMBA/HAKI ZA MPANGAJI KISHERIA? mahusiano yanayojengwa baina ya mmiliki na mpangaji katika ard...
01/12/2022

NI UPI WAJIBU WA MWENYE NYUMBA/HAKI ZA MPANGAJI KISHERIA?

mahusiano yanayojengwa baina ya mmiliki na mpangaji katika ardhi ni mahusiano ya kisheria. Sheria ya ardhi imeweka mwongozo juu ya wajibu wa pande zote mbili na haki zao. Katika makala hii tunakwenda kutazama mambo ya msingi ya mmiliki anayopaswa kuzingatia k**a wajibu wake wakati wa upangishaji wa ardhi au jengo lake.

Wajibu wa Mmiliki wa ardhi katika upangishaji

(a). Wajibu wa kumpa mpangaji uhuru wa kutumia eneo alilopanga

Mmiliki wa nyumba au eneo la ardhi anapaswa kujua kwa kipindi kile ambacho eneo hilo amepangisha linakuwa chini ya umiliki wa mpangaji iwapo mpangaji atakuwa amelipa kodi ya pango na kuzingatia masharti yote ya upangaji. Mmiliki au wakala wake hapaswi kuingilia uhuru wa mpangaji kwa namna yoyote ile katika kipindi cha upangaji wake. Sheria inalinda uhuru wa mpangaji dhidi ya matendo yoyote ya mmiliki au wakala wake. Ipo tabia baadhi ya wamiliki kuingilia maisha au shughuli za wapangaji kwa kigezo wao ni wamiliki hii si sahihi kwani mpangaji anayo haki ya kutoingiliwa katika maisha yake au shughuli zake anazofanya alimradi zipo kwa mujibu wa sheria na kulingana na mkataba.

(b). Wajibu wa kuhakikisha eneo jirani haliingilii uhuru wa mpangaji kwa namna yoyote.

Iwapo mmiliki ana eneo ambalo ni jirani na la mpangaji inampasa kuhakikisha kuwa shughuli katika eneo hilo haziingilii uhuru wa mpangaji. Mmiliki anapaswa kuhakikisha eneo jirani na lile alilopangisha linakuwa katika mazingira mazuri ya kumuruhusu mpangaji kufurahia uhuru wa upangaji wake. Mmiliki ahakikishe njia inayoenda kwenye eneo la mpangaji inapitika vizuri.

(c). Kuhakikisha eneo lililokodishwa lipo salama na limerekebishwa ipasavyo kwa ajili ya lengo la upangaji.

Ni wajibu wa mmiliki kuhakikisha eneo la upangaji limerekebishwa kukidhi viwango vya upangaji kwa kusudi husika. Mpangaji hapaswi kuingia gharama za kurekebisha eneo la upangaji huo ni wajibu wa mmiliki. Tumeona migogoro mingi baina ya wamiliki na wapangaji inatokana na wamiliki kutotimiza wajibu wao kwa kuwaachia wapangaji uhuru wa kufanya marekebisho ya eneo kwa miadi ya kukatana kweny kodi na mwisho wake wanakosa maelewano.

(d). Kuhakikisha kodi za majengo na ardhi zinalipwa

Huu ni wajibu muhimu sana wa mwenye eneo yaani mmiliki. Tunajua kuwa ardhi ni mali ya umma na wamiliki wana wajibu wa kuhakikisha kodi ya ardhi na majrngo inalipwa ndani ya wakati k**a sheria zinavyoongoza. Mpangaji kwa kawaida hausiki na malipo ya kodi za majengo na ardhi mpaka pale kutakapokuwa na makubaliano vinginevyo.

Hitimisho

Mmiliki ana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa ili eneo lake linapopangishwa lisiwe katika migogoro ya aina yoyote baina yake na mpangaji au mamlaka za serikali na majirani. Wajibu wa mmiliki unapotekelezwa vizuri ni haki za mpangaji. Mmiliki akitimiza wajibu wake anastahili kupata kodi yake kwa wakati kutoka kwa mpangaji.

Address

Kinondoni
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ijue Sheria Na Haki Zako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ijue Sheria Na Haki Zako:

Share

Category