25/03/2026
NASAHA JUU YA NDOA 💍
Alhamdulillah 🤲
Tunampongeza ndugu yetu kwa hatua hii njema ya ndoa. Mwenyezi Mungu aiweke ndoa hii katika kheri, upendo na utulivu. Ameen.
🕌 Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an:
"Na katika Ishara Zake amekuumbieni wake zenu ili mpate utulivu kwao, na akaweka baina yenu mapenzi na rehema."
(Surat Ar-Rum 30:21)
✨ Ndoa si jambo la starehe tu, bali ni ibada, ni jukumu, na ni njia ya kujilinda na maasi.
📖 Pia Allah (Subhanahu wa Ta'ala) anasema:
"Na waozesheni wale wasio na wake miongoni mwenu... ikiwa ni masikini Allah atawatajirisheni kwa fadhila Zake."
(Surat An-Nur 24:32)
💡 Ujumbe kwa vijana ambao bado hawajaoa/kuolewa:
Jiandaeni kwa ndoa kwa njia halali
Muombe sana Allah akupe mwenza mwema
Epukeni zinaa na mambo yanayopelekea maasi
Kuwa na subira, muda wa Allah ni bora kuliko wetu
🤲 Dua:
Allahumma barik lahuma wa barik ‘alayhima wa ajma’ baynahuma fi khayr
🌿 Mwenyezi Mungu atujaalie ndoa zenye baraka na atuwepushe na fitna. Ameen.