03/02/2026
JE UTADAI VIPI FIDIA BAADA YA KUSABABISHIWA AJALI BARABARANI KIZEMBE:
Hatua za kisheria za kuchukua unapogongwa kwa uzembe.
Ajali kati ya magari mawili hutokea mara nyingi barabarani kwa uzembe wa dereva mwingine,usijisikie huna msaada pindi unaposababishiwa ajali,unayo haki kudai fidia dhidi ya madhara uliyopata kutokana na ajali hiyo.
HATUA MUHIMU ZA KISHERIA UNAZOPASWA KUFANYA BAADA YA KUSABABISHIWA AJALI KIZEMBE:
> Ripoti polisi, hakikisha ajali inapotokea hausogezi gari eneo la tukio, na ajali hiyo inaripotiwa mara moja polisi. Hapa polisi watapima na itaandaliwa police report, sketch map.Pia ni lazima ujaze fomu PF3.
> Matibabu, k**a umepata majeraha hakikisha unaenda hospitali na hifadhi rekodi zote za matibabu ikiwemo fomu PF 115.
>Hakikisha dereva aliyesababisha ajali anafunguliwa kesi ya jinai kwa kuendesha gari kwa uzembe.
>Hakikisha unawasiliana na kampuni ya Bima ya dereva aliyesababisha ajali na unapata fomu PF 90
> Hakikisha unapata msaada wa kisheria: tafuta wakili atakayeweza kukufungulia kesi ya madai, hakikisha fidia unayodai inalingana na madhara uliyopata.
NYARAKA UNAZOPASWA KUWA NAZO KABLA YA KUFUNGUA KESI YA MADAI:
>PF 90
>PF3
>PF 115
> Hukumu ya kesi ya jinai aliyofunguliwa dereva mzembe
MAAMUZI YA MAHAKAMA KATIKA KESI YA KUDAI FIDIA KUTOKANA NA AJALI ILIYOSABABISHWA NA DEREVA MZEMBE
Ivi karibuni mahak**a kuu kanda Arusha imemuamuru dereva mzembe pamoja na mwajiri wake na kampuni ya bima kulipa fidia gari iliyogongwa kutokana na uzembe wa dereva katika kesi ya LEOPARD TOURS LTD Versus LODHIA STEEL INDUSTRIES LTD AND OTHERS.(civil case No 28359 of 2023) [2026] TZHC 88 ( 30 January 2026)
Kesi hii ilikuwa inahusiana na madai yaliyofunguliwa na kampuni ya utalii (leopard Tours) wakidai kulipwa fidia na kampuni ya Lodhia ambapo gari la kampuni ya Lodhia liligonga gari la kampuni ya leopard kwa uzembe uliosababishwa na dereva wa gari la lodhia. Ajali hiyo ilitokea maeneo ya kikakatiti.
Kampuni ya leopard iliweza kuthibitisha madai yake na Mahak**a kuu Kanda ya Arusha ikaamuru kampuni ya lodhia, dereva na kapuni ya bima kulipa fidia kwa kampuni ya leopard pamoja na gharama zilizosababishwa na ajali hiyo ya kizembe.
NB. usikubali haki zako zipotee. Ikiwa gari lako limegongwa kwa uzembe, chukua hatua za kisheria na hakikisha unapata fidia stahiki.
"Je umewahi kudai fidia baada ya gari lako kugongwa ? Tueleze uzoefu wako``